GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwapongezeni sana Clouds fm na E fm kwa kuja na UBUNIFU wa aina yake hasa katika vipindi vyenu vya michezo. Kitendo chenu cha kuwajumuisha watangazaji wa kike katika hivyo vipindi vyenu vya michezo kumewaongezeeni sana Watu wanaowasikiliza na kuwafuatilia.
Mabinti hawa ambao ni Watangazaji wazuri na mahiri wa habari za michezo Fatma Likwata wa Clouds fm na Tunu Hassan Shemkome wa E fm ama hakika wanafanya Kazi yao vizuri sana na nisiwaficheni sisi Wanamichezo MABAZAZI wote sasa hatubanduki katika hizo redio zenu hasa vipindi vyenu vya michezo vinapoanza.
Na kizuri zaidi ambacho ndiyo mmetuweza kabisa ni kuwa hawa Mabinti wote ni WAREMBO wa hali ya juu kiasi kwamba tunahisi pengine wakati mnawaajiri mliweka pia na Kigezo cha UZURI au MVUTO kwani kwa UZURI wao nawafananisha na MALAIKA wa mbinguni.
Angalau nyie Clouds fm na E fm mmeweza kuajiri hao Mabinti wa Utangazaji wa Habari za michezo wawili hadi kuwashinda wale wenzenu wa mkabala na Bamaga ambao wana Mtangazaji wao mmoja wa kike ambaye kwanza hajui kutangaza na hata akitangaza anatangaza Kibabe sana halafu amenenepeana kusikofaa.
Kutokana na UFANISI wa hawa Watangazaji Fatma Likwata wa Clouds fm na Tunu Hassan Shemkome wa E fm na UELEDI wao mkubwa katika TASNIA nzima ya Utangazaji na Uandishi wa Habari naomba muwaongezee Mishahara minono na muwapende sana kwani hao ndiyo wanatufanya TUTEGESHE misikio yetu huu mikubwa kusikiliza hizo redio zenu.
Kama hamtojali pia si vibaya mkaweka tu hapa namba zao za Tigo Pesa au M Pesa au Airtel Money ili na sisi wasikilizaji wao tuweze kuwatunuku pia kwa pesa kutokana na umahiri wao na mkiweza pia ili kutusaidia zaidi tungependa pia mtuelekeze hadi wanapoishi na mtuambie kama wameolewa au bado wanatafuta wachumba ili kama vipi masela " wajilipue ".
Ukiwasikiliza hawa Watangazaji wawili na zile sauti zao nzuri na tamu ama hakika unaweza hata ukasahau kuwa unatakiwa kufanya kazi nyingine na badala yake unawasikiliza tu wao " wanavyotiririka ". Hofu yangu tu ni kwamba Watangazaji hawa msipowajali au kuwaongezea mishahara vyombo vya habari vikubwa hasa vya Ulaya vitawachukua halafu vipindi vyenu hivyo vya michezo vitadoda na sisi MABAZAZI wa michezoni tutawakimbia.
Lifanyieni Kazi tafadhali na waongezeeni Mshahara upesi na wapeni marupurupu na huduma zingine zote stahili kwani TUNAWAKUBALI sana.