Clouds FM kuweni makini

Clouds FM kuweni makini

Observer2010

Senior Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
195
Reaction score
44
Japokuwa najua ni redio ya kidaku zaidi, ila ni vyema Clouds FM kuwa makini wanapotoa habari zenye umuhimu na maslahi ya Taifa.

Najua kuna mambo mengi tu wanayamislead, ila hapa nitatolea mfano mambo mawili waliyotokea hivi karibuni,

1. Wakati wa mabomu ya Gongo la Mboto, Clouds fm wakatangazia umma ya kuwa Mabomu yanalipuka katika kambi ya Mkuranga.

2. Ilipotokea ajali ya 5 Star maeneo ya Morogoro, clouds fm wakangazia umma kuwa ajali imetokea maeneo ya Kibaha.

My concern ni kuwa kama hawana uhakika wa tukio si waseme watalitolea maelezo ya kina watakapopata uthibitisho wa habari. Huu ni ukiukwaji wa taratibu na taaluma ya uhandishi wa habari.

:smow::smow::smow::smow::smow:
 
we unawasikiza wa nn wkt unajua hawako makini? dont waste your time kuwasikiza.
 
leo asbh nilikuwa nasikiliza PB wkt wa michezo wakaweka mazungumzo ya shafii dauda sjui yule mtangazaji/mchambuzi wao wa michezo akiongea na paulsen/kocha wa stars...yaani ilikuwa aibu tupu..yule shafii aanamuuliza paulsen "when did you requested the players"...abu tupu..sjui kingreza cha wapi..."did you requested"..lol..
 
Japokuwa najua ni redio ya kidaku zaidi, ila ni vyema Clouds FM kuwa makini wanapotoa habari zenye umuhimu na maslahi ya Taifa.

Najua kuna mambo mengi tu wanayamislead, ila hapa nitatolea mfano mambo mawili waliyotokea hivi karibuni,

1. Wakati wa mabomu ya Gongo la Mboto, Clouds fm wakatangazia umma ya kuwa Mabomu yanalipuka katika kambi ya Mkuranga.

2. Ilipotokea ajali ya 5 Star maeneo ya Morogoro, clouds fm wakangazia umma kuwa ajali imetokea maeneo ya Kibaha.

My concern ni kuwa kama hawana uhakika wa tukio si waseme watalitolea maelezo ya kina watakapopata uthibitisho wa habari. Huu ni ukiukwaji wa taratibu na taaluma ya uhandishi wa habari.

:smow::smow::smow::smow::smow:

Jitahidi uwe unasikiliza redio za maana, zipo nyingi tu hapa nchini.
 
Hii ni redio ya umma pamoja na udaku wao lakini wanatakiwa wawe serious. Kuna wakati wanachemka hadi kupitiliza mtu unajiuliza hawa jamaa wanajua wanachokifanya kweli. Huwa siwasikilizi ila redio yangu ni ya kizamani kwa hiyo wakati natafuta station nyingine huwa napitia frequency zao basi naweza kusikiliza by the way. Lakini kuna kile kipindi cha jumapili kinaitwa njia panda, hicho huwa nasikiliza.
 
haswa huyu kibonde ni mmbea mnafiki na fedhuli, lakin pia sambamba na huyu mpuuzi ni vyema wakatambua kuwa pamoja na kuwa na mambo mazuri ambayo wanayatoa kwa wasikilizaji na umma wote kwa ujumla, kuna baadhi ya watangazaji ambao wakisikia ishu hata pasipokuwa na uhakika wanairusha hewan, mi nawaomba waache la cvyo muda c mrefu watapoteza wasikilizaji wengi sana
 
Hii ni redio ya umma pamoja na udaku wao lakini wanatakiwa wawe serious. Kuna wakati wanachemka hadi kupitiliza mtu unajiuliza hawa jamaa wanajua wanachokifanya kweli. Huwa siwasikilizi ila redio yangu ni ya kizamani kwa hiyo wakati natafuta station nyingine huwa napitia frequency zao basi naweza kusikiliza by the way. Lakini kuna kile kipindi cha jumapili kinaitwa njia panda, hicho huwa nasikiliza.

Kwenye blue ni Kweli?? Hivi inatanagza kutoka Mkoa gani,Mimi nipo TZ lakini mbona siijui.Inapatikana masafa gani na wapi au ni zile redio zilizojaa dar zinazoishia Kibaha.
 
Redio ya umma si tbc zamani rtd na uhuru jamani? Hii ni radio ya watu binafsi sio ya umma (serikali).
 
May be alikuwa anamaanisha " the peoples station"...radio ya watu..Kwa ufupi sio clouds peke yenye mapungufu kwenye kutoa taarifa radio nyingi tu za bongo ila tatizo la Clouds inasikilizwa na wengi kasoro hizo ndogo ambazo zinarekebisha ishu kubwa ilikuwa ni taarifa ya ajali iliyotokea huenda mtoa habari wa mwanzo Muimbaji wa taarab mwanahawa Ali huenda alikuwa ameweweseka nakusema vingine
 
we unawasikiza wa nn wkt unajua hawako makini? dont waste your time kuwasikiza.

Sometimes inatokea upo sehemu ya public kama kwenye daladala, kwenye saloon au hata kwenye pub na wakawa wametune hiyo radio, huwezi ziba masikio, na kiustaarabu huwezi ukawaambia wabadili station wakati kuna watu wengine umewakuta wanasikiliza. The key point ni kuwa makini katika kutoa taarifa especially zenye ambazo zina public interest. Maana hata usiposikiliza wewe, wengine wanaosikiliza zitawa mislead.
 
Email address zao ni eti pb@cloudsfm.co na wanatangaza kila siku wakati inatakiwa kuwa pb@cloudsfm.co.tz

Huwezi pata hiyo website ni ya zamani. wamebadili na wana website kiboko sana ambayo umeikanusha kwa makosa ambayo ni www.cloudsfm.co hivyo basi ukitaka kuwasiliana na vipindi kama leotena una address leotena@cloudsfm.co Hawa watu to be fair wana vipindi vizuri ukiondoa Jahazi ya sasa ikiwa na Kibonde na wanawake 2 wanaocheka cheka - wote watatu wana hulka ya kujipendekeza na kupindisha ukweli. Wasikilize Dinnah na Gea utafurahi na vpindi vingine ukitoa Jahazi ya sasa.
 
Power breakfast sio mbaya sana, ila kuna kipindi siku hizi kinaitwa amplifaya (amplifier), hiki ni cha dogo mmoja anaitwa mirlad ayo aliyahama kutoka radio one, ndani yake kuna kipengele kinaitwa 'habari bila wasiwasi na wasiwasi mwabulambo' hicho ukisiliza lazima utapike, jamaa anaboa hakuna mfano, habari zinazopaswa kuwa za kusikitisha yeye anazisoma kama anashangilia vile na lugha ya mtaani inayotia kinyaa, jaribuni kusikiliza kuanzia saa 12 jioni mpaka saa tatu usiku, halafu kipondi chenyewe nadhani hawakufanya utafiti wa kutosha, kuna wakati wanaishiwa habari basi wanafululiza mziki mapak unasahau ni kipindi gani.
 
Halafu clauds fm wapunguze ushabiki wao wa kisiasa. CCM hata wakifanya jambo baya wenyewe kazi kuiremba na kukejeli wapinzani. Mwisho watageuka kuwa ze comedi.
 
Power breakfast sio mbaya sana, ila kuna kipindi siku hizi kinaitwa amplifaya (amplifier), hiki ni cha dogo mmoja anaitwa mirlad ayo aliyahama kutoka radio one, ndani yake kuna kipengele kinaitwa 'habari bila wasiwasi na wasiwasi mwabulambo' hicho ukisiliza lazima utapike, jamaa anaboa hakuna mfano, habari zinazopaswa kuwa za kusikitisha yeye anazisoma kama anashangilia vile na lugha ya mtaani inayotia kinyaa, jaribuni kusikiliza kuanzia saa 12 jioni mpaka saa tatu usiku, halafu kipondi chenyewe nadhani hawakufanya utafiti wa kutosha, kuna wakati wanaishiwa habari basi wanafululiza mziki mapak unasahau ni kipindi gani.

hapa kweli namimi nakuunga mkono....kwakweli kama ni picha, sehemu hii ni unfocused
 
ni kweli jamani warudishe africa bambataa ndo mana hata matangazo ya biashara yamepungua hasa jahazi na amplifier duuuuuuuuuu
kusaga fanya uchunguzi wa hilo,wanaotoka makazini wanataka kuburudika sio kusikiliza bored vipindi bwana :bored: :bored: :bored: :bored: na ukizingatia uko kwenye foleni ndo kabisaaaaaaa utajuta :bored::bored::bored:\
twataka viburudisho jamani ohoooooooo:msela: :majani7: :dance:
 
Redio ya umma si tbc zamani rtd na uhuru jamani? Hii ni radio ya watu binafsi sio ya umma (serikali).

Na wewe ni walewale wanaodhani kwamba mpaka leo Rais ni Nyerere, aliekudanganya kwamba Redio uhuru ni redio ya umma ni nani? kha! safari bado ndefu kweli.
 
Back
Top Bottom