Makampuni ya simu yanatumika vibaya, hasa katika siku za hivi karibuni. Ni mfumo wa kifisadi bado unaendelea. Leo hata wewe ukitaka hela kiulaini, unakwenda kwenye kampuni yoyote ya simu, unakubaliana kutumi mtandao wao kuwafikiwa watu kwa njia ya ujumbe. Wao ( Makampuni ya Simu) yanagharama zao za msg. Wewe unachotakiwa kufanya ni kukubaliana nao kulipa gharama za msg, say Sh. 60/=. Sasa wewe utawatoza wanaotaka huduma hiyo ya kijinga sh. 200/= au 300 au 500/= na nyingine hata 1000/=. Utawatumia ujumbe wa kuwahamasisha wajiunge na mpango wako wa kijinga hata bila kuwafafanulia hasara zinazoambatana na mpango huo. Na kwakuwa wengi wetu hatupendi sana kudadisi kabla ya kufanya chochote tunaishia kujiunga haraka haraka. Bahati mbaya zaidi, unapewa namna ya kujiunga. Hupewi maarifa ya kujitoa. Machungu ya kukatwa pesa yanapokelea ndio akili ya kujitoa inapokuja. Kwakuwa makampuni ya simu yanatengeneza faida, hayashtuki sana unapolalamikia kujitoa. USHAURI WANGU NI KUWA, NI VYEMA KUWA MWANGALIFU NA MPANGO WOWOTE UNAOTANGAZWA, KABLA YA KUJIUNGA HAKIKISHA UMEJUA NINI HASARA ZAKE. Binafsi sijawahi kujiunga kwa taarifa za habari, vichekesho, afya, biblia/korani, caller tune na mengine mengi ya kiwiziwizi yanayofanana nayo.