Clouds fm inaliangamiza taifa

Clouds fm inaliangamiza taifa

malimwengu

Member
Joined
Aug 29, 2011
Posts
21
Reaction score
12
Radio Clouds isipoangaliwa italiangamiza taifa. Radio hii inayojinasibu kuwa ni radio ya vijana haina jambo la maana zaidi ya kuwajrngea watanzania utamaduni wa kitumwa, utamaduni wa kuthamini utamaduni wa nje hasa wa Marekani na watu wa Marekani. Utamaduni ambao umepelekea vijana wengi wa ktanzania kuiita nchi yao jalalani.

Radio hii pia inajenga msingi wa kuwatenga vijana kimatabaka. Imejipa taswira ni radio ya vijana wa ushuani ambao wana nafasi nayeyote anayetaka kuonekana ameendelea ni sharti ajiunge nao. Radio hii inawafundisha vijana tabia ya kujipendekeza kwa wakubwa kwa hali yoyote ile hata kama hao wakubwa wanatenda mambo ya ovyo na bahati mbaya sana kuna baadhi ya wakubwa wenye nydhifa za kitaifa wanaliunga mkono hili kiasi cha kukubali hata kununuliwa keki zao za birthday na radio hii.

Radio hii haiwapi mwongozo vijana inaodai kuwalenga washiriki kikamilifu katika kuamua na kusimamia ustawi wa taifa lao badala yake wamejengwa kuwa wapokeaji na wanaosubiri kudra kutoka kwa wanaotoa neema.

Watangazaji wa radio hii wanajikweza na kujilazimisha kuwa macebreties wakiwa kwenye vipindi wazungumzie magari yao, wawataje watu maarufu ili kuonekana nao ni muhimu na pia wana uhusiano na watu mashuhuri ili kijipa uhalali wa wao kuendelea kuwahadaa na kuwatia kiini macho vijana na wananchi wa Tanzania.

Radio hii inafika mbali kiasi cha kuwafanya watangazaji wao kuwa watu maarufu na mashuhuri hata kama wakiwa watupu vichwani kiasi kwamba wanatumia umaafurufu huo kujipatia nafasi mbalimbali za uongozi katika vyama vya michezo na baadae kuchukua uongozi wa kisiasa.

Radio inawatenga vijana kutokana na wapi wametokea na nasaba zao ni zipi. Inajihusisha zaidi na matajiri na endapo kama watajuhusisha na mtoto wa uswazi basi jua kuwa huyo ana kipaji na wanataka kumtumia kwa manufaa yao.

Radio hii inapandikiza chuki ya makundi na matabaka ndani ya vijana. bahati mbay zaidi wanasiasa wariho wenye kutaka sifa wanajisogeza karibu na radio hii kwa uchu wao na tamaa zao za kisiasa.

Tanzania yetu sote. Wote tulikuwa katika hali ya usawa na kupendana kabla wenzetu wachache walipoanza kuiba na kufuja. Huko hakuwafanyi wawe na haki ya kidhihaki na kuwacheka wengine kwani hicho wanachoringia ni mali yetu sote. Wale vijana wanoipenda nchi wakaamua kwenda shule na kuijenga nchi kupitia njia stahiki, halali na zinazoeleweka wasidhihakiwe na kuonekana wajinga. So vijana wote wa kitanzania wenye kutaka kufanya mzee Juma mwapachu anachokiita Bongoism na si vijan wote baba wakwe ama mama wakwe zao wan music systema za kuwafanya wapige kwenye matamasha na si vijana wote wenye Ma God father wa kupewa kazi ambazo malipo yake ni makubwa kuliko uhalisia wa kazi yenyewe. Clouds wanapaswa walifahamu hili na pia wajue kuwa wanjukumu la kuwaelimisha vijana wa kitanzania kuhusu haki zao na kuwasaidia kuwatangaza pale wanapozidai na si kuwabeza kama vile walipowabeza vijana wa chuo kikuu walipodai kuongezewa posho zao.

Kama kuna jambo ambalo naliiona lapaswa kuangaliwa kwa macho mawili basi ni hili la kuwepo kwa radio zenye kuwafanya au kutaka kuwafunza watanzania hasa vijana utumwa wa fikra na Clouds Fm yapaswa kuangaliwa kwa macho mawili na kama zipo radio nyingine za namna hii basi kwa pamoja tuseme walichokipanda chatosha, sasa basi.
 
Naheshimu maoni yako. Lakini ukumbuke hizi ni zama nyingine i.e. Freedom of press/expression. Kila nchi dunia hii kuna chombo/vyombo vya habari ambavyoo kinakuwa kero kwa watu wengine na at the same time kinakuwa ni raha kwa upande mwingine.
Kuna watu ambao hatupendi :Big Brother Africa, Rush Limbaugh, Sean Hannity, Fox News, Glen Beck, Lura Ingraham etc. lakini at the same time kuna mamilioni ya watu hupenda. Ndizo zama za freedom of press/expression.
 
Dah mkuu umefunguka! You have a point anyway! Whats the way foward? Given that kuna uhuru wa vyombo vya habari!
 
Ukisikiliza Clouds Fm kwa muda mrefu lazima uwe punguani..kuna watangazaji pale uwa nashindwa kuelewa wanafanya nini;
Bonge wa PB
Gerald Hando
Barba Masoud
PJ
Kibonde nk
 
Tatizo lao ni ukimwi, sasa kwa vile ukimwi unasabaisha na mataizo ya kiakili basi hayo ndio tunayaona kwenye maongezi yao. Kuna mambo mengine yanaongelewa na baadhi ya watangazaji wao huwezi amini, lazima muongeaji ana matatizo ya kiakili hawezekani mtu mzima na mwenye akili timamu akaotoa comments hizo.
 
Clouds fm imejaa MAKANJANJA watupu nduguzangu wala msishangae wanayoyafanya leo hii
 
Nani kakuambia ni Radio ya watoto wa ushuani? , hii ni radio ya mabrazameni na ma sisterdo wa uswazi. Radio ya watoto wa ushuani ni Eas Africa Radio, (kizungu kingi na kuukataa Utanznaia) , ukienda kwenye shows mbili kati ya Prime Time na ile ya East Africa utakuta ya East Africa imejaa watoto wa ushuani zaidi. Napenda idea ya clouds ya utanzania zaidi ila sipenzi watuwake kuna Ruge wauaji wa vipaji!
 
Naheshimu maoni yako. Lakini ukumbuke hizi ni zama nyingine i.e. Freedom of press/expression. Kila nchi dunia hii kuna chombo/vyombo vya habari ambavyoo kinakuwa kero kwa watu wengine na at the same time kinakuwa ni raha kwa upande mwingine.
Kuna watu ambao hatupendi :Big Brother Africa, Rush Limbaugh, Sean Hannity, Fox News, Glen Beck, Lura Ingraham etc. lakini at the same time kuna mamilioni ya watu hupenda. Ndizo zama za freedom of press/expression.

MSNBC unaipenda?
 
Yes, but on the other side of the political spectrum. Fox leans right whereas Msnbc leans to the left (Obama's side).

But Msnbc they do allow some criticisms on Obama...and they are a real news network although they do favor democrats...
you cant say that with Fox news...
 
But Msnbc they do allow some criticisms on Obama...and they are a real news network although they do favor democrats...
you cant say that with Fox news...

How often do you watch FOX news? Obviously not a lot because you are oblivious to all the criticisms they dish out against Republicans.
 
How often do you watch FOX news? Obviously not a lot because you are oblivious to all the criticisms they dish out against Republicans.

Yes.not much ....but those few times.....i was puzzled...
remember when they call 'a terrorist bump' when Michelle went to 'THE VIEW'?????/
a terrorist bump????
 
Back
Top Bottom