Clouds FM acheni Utoto

afu mtoa uzi hujaelewa kitu. lady jay dee aliomba mwenyewe sauti yake,jina lake au nyimbo zake zisikike clouds. sasa hapo clouds wana kosa lipi.?
Mengine sijui

kwa hiyo wanapo mute sauti ya Jay Dee wanamkomoa nani? Jay Dee au wasikilizaji wa huo wimbo na wasikilizaji wa hiyo radio?. Kwa mtazamo wangu wanawakomoa wasikilizaji na sio JAy Dee. Na bila shaka huyo Jay hata hii radio haisikilizi kabisa. kimsingi clouds lazima wajitafakari ili ugomvi wao na Jay Dee usiathiri wasikilizaji wa radio yao. Mimi kama msikilizaji wa hii radio nahitaji kupata full burudani sio hapa sauti inatoka pale una mute, unanimutia msikilizaji wako kwani mimi nimekukosea nini. Kwani kama clouds ina mgogoro na Jay Dee basi huo mgogoro na wasikilizaji wa hiyo radio lazima waathirike? Ndio maana clouds inalaumiwa kuwa kuna mambo ya kitoto. Maana wao wanamfikiria mtu mmoja tu Jay Dee, badala ya kufikiria wasikilizaji wa radio ambao ndio wanafanya radio iwe hapo ilipofikia.
 
Mkuu umeeleweka hasa hapo bold pia ndio umenifanya nikuelewe zaidi maana mie niliangalia bifu kati ya taasisi na individual huku upande mwingine wa individual bifu kati ya msanii na msanii sikuliangalia. Sie wengine tupo outdated hatujui kinachoendelea kivile katika sekta ya burudani kutokana na kukosa muda wa kusikiliza radio hasa mida ya mchana japokuwa mambo mengi tunayapata kupitia kwenye mitandao ndio maana unaona tunahoji na si kwamba ninaichukia hiyo radio na si kwamba pia ninampenda JD nilichokuwa naangalia kwa jicho la mlaji (consumer) kwa kuwa pamoja na kwamba tuna radio kibao nchini hakuna radio inaweza ikamridhisha kila msikilizaji na ndio maana unaona watumiaji huwa tuna mtindo wa kuhama hama hasa pale unapoona kuna kipindi flani huvutiwi nacho.
 
afu mtoa uzi hujaelewa kitu. lady jay dee aliomba mwenyewe sauti yake,jina lake au nyimbo zake zisikike clouds. sasa hapo clouds wana kosa lipi.?
Mengine sijui

Ney nae pia alisema hayo
 
Umeeleweka mkuu
 
kubalini kataeni. clouds ndio kituo bora cha radio. wanamapungufu ya kiubinadamu. e fm naona wanajitahidi na kufikia clouds bado sana. millardayo mwenyewe alikimbia ipp media. mbona ipp media inawanyonya sana wafanyakazi haisemwi
 
Kama clouds waki mute basi sikiliza efm wataachia clouds ni media ya mtu binafsi siyo ya serikali na ndo Ruge akiamua leo piga gospel zitapigwa gospel mwanzo mwisho ila Kama wewe pera utaskiza tuu ata ipigwe mabata madogo wanaogelea
 

Acha kuwa mgumu wa kuelewa. Ikiwa nyimbo unaweza ku mute na bado ikasikilizika na kuleta maudhui yaliokusudiwa kwenye wimbo husika wata mute sauti ya JD na kupiga wimbo. Na ikiwa ukii mute inapoteza maudhui basi haitapigwa kabisa.
 

its more than that mzee.mimi nasimamia wasanii 2.mmoja ni mkubwa sana kuna mambo siwezi kuyaweka humu.AM IN
 
Unajua ndugu yangu, ni kweli kabisa kwamba hapa kuna wengine hawaelewi kabisa what's going on na hata kuhoji kwao wala hakuna maana yoyote mbaya kwahiyo sitashangaa kusikia hata wewe wala hukuwa na nia mbaya yoyote! Hata mleta mada mwenyewe, wala haielekei kwamba nae ana negativity na Clouds lakini hapa jamvini pia wapo members tena wengi tu, hawa hata siku moja hutawasikia wakisema zuri la Clouds... wao mara zote Clouds ni radio ya mashoga, au hili na lile... ukiwauliza ikiwa wamewahi kum'---- prenter yeyote wa Clouds hakuna hata mwenye jibu.... mbaya zaidi wengi wao hata presenter wenyewe wanaishia tu kuona picha zao kwenye mitandao ya kijamii au sana sana kwenye tv... lakini hapa watajifanya wanawajua mwanzo hadi mwisho lakini kuwajua kwao ni upande wa uovu peke yake... sasa mtu kama huyo sidhani kama tafsiri sahihi inayomfaa zaidi ya kuwa ni mtu aliyetawaliwa chuki! Nchi kuna wengine hawapendi kabisa kumuona mwenzao anapiga hatua... mfano mzuri chukulia mfano wa mwanamuziki Diamond (ikiwa ni mfuatiliaji)! Unakuta mtu anaonesha chuki ya wazi wazi wakat hata huyo Diamond mwenyewe hajawahi kumuona zaidi ya kusihia kumuona kwenye tv!

Kwa upande mwingine kuhusu hao Clouds, hapa kuna member wa kutosha tu ambao chuki zao dhidi ya Clouds inasukumwa na ushabiki wa kisiasa... hakuna lingine! Sie wengine tunaona ni ujinga kuchanganya masuala ya siasa na burudani na ndio maana ukumbi wa Billicanas unamilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA lakini sidhani kama kuna siku umewahi kusikia wafuasi wa vyama vingine wanaipiga vita Billz kwa sababu tu mmiliki wa ukumbi huo ni mwenyekiti wa chama kingine!
 
its more than that mzee.mimi nasimamia wasanii 2.mmoja ni mkubwa sana kuna mambo siwezi kuyaweka humu.AM IN
Sijakuomba unitajie nafasi yako kwenye music industry coz' hapa tunatumia fake ID kkwahiyo haisaidii! Nilichokutaka uniwekee huo utafiti uliofanya wewe coz' nimekujibu hoja zako kuhusu akina Dudu Baya na Juma Nature! Na kama kweli unasimamia wasanii basi unafahamu jinsi wasanii wengi wa Tanzania walivyo kimeo na ndio maana huwa nashangaa sana ninaposikia kwamba eti wanapewa stress na Clouds! Kama kweli unasimamia wasanii basi unafahamu kwamba majority ya wasanii ni wavuta ganja tangu huko walikotoka! Zamani sana, mwishoni mwa miaka ya 90 nilipoenda studio kwa mara ya kwanza nilishangaa nilipokuta bonge la fuko la ganja... haikuwa ya kuuza bali watu kuvuta! Sasa watu kama hao kesho na kesho kutwa wakigeukia drugs, lawama kwa Clouds kwamba eti wanawapa stress...? Kuna mtu hapa juzi kaleta uzi kuwalaumu hao hao Clouds kwamba eti wanajifanya kutangaza kifo cha Mez B wakati walikuwa hawapigi nyimbo zake... mtu unashangaa ni nyimbo zipi hizo!!
 
Hiv mtu akishirikishwa kwenye wimbo, unakuwa wa kwake? Hiv kwamba akisema nyimbo zake zisipigwe na hizo pia kazijumuisha?

Sasa c atakuwa na bifu hadi na waliomshirikisha? Au vp, kama kuna ufafanuzi zaidi naombeni.
 

Huko mimi nasikiliza kipindi cha NJIA PANDA tu vingine vyote tupa kule
 
Hiv mtu akishirikishwa kwenye wimbo, unakuwa wa kwake? Hiv kwamba akisema nyimbo zake zisipigwe na hizo pia kazijumuisha?

Sasa c atakuwa na bifu hadi na waliomshirikisha? Au vp, kama kuna ufafanuzi zaidi naombeni.

Ni kama kwamba imetokea siku wewe umegombana na jirani yako na hadi mkawa hamsalimiani, halafu rafiki zako wanapokuwa wanakuja kwako na wakamuona jirani yako(ambaye wewe umegombana nae) na wakawa wanamsalimia basi wewe hupiga kelele ili zile salamu zisisikike kwa sababu tu wewe una ugomvi na huyo jirani yako.
 

Hiyo nayo ni akili kweli, mtoa mada alivyosema UTOTO yupo sahihi kumbeeeee!!!
 
Hata kama Jdee alisema, Clouds sio kaz yk kujibizana ya mtaani.jenga chuki na maisha kw kufanya kazi, sio kujenga na wasanii kw kufanya uzandik wa kishamba.sio mpnz wa bongo flavr ila wanachokifanya ni uswahili, utoto, na ni primitivity.
 
Na hiyo unawatenga wasanii hakuna atakaeimba nae kwa kuhifia wimbo wake kuchezwa kutuoni hapo
 
Mi na clouds sijui vipi.? Kwanza ataiyo tv yao sijuagi wanaonyesha nini huko. Imeanzishwa mda lakin mpaka sasa haina vipindi bora vyakusema ukae chini utizame
 

Alichosema nyimbo zake zisipigwe, hiyo nyimbo ya alikufa kwa ngoma ni ya Mwana FA, JD kashirikishwa tu. Unapomute chorus kwenye nyimbo unaharibu taste ya wimbo wote. Wasipige zile ambazo ni za JD mwenyewe lakini siyo zile alizoshirikishwa
 
Alichosema nyimbo zake zisipigwe, hiyo nyimbo ya alikufa kwa ngoma ni ya Mwana FA, JD kashirikishwa tu. Unapomute chorus kwenye nyimbo unaharibu taste ya wimbo wote. Wasipige zile ambazo ni za JD mwenyewe lakini siyo zile alizoshirikishwa

Jd ashagombana na mwanafa hata hawasalimiani. Hivyo ukiacha ugomvi wa jide na clouds bado kuna ugomvi wa jide na mwanafa. Sijui unapata picha gani hapo? Ku-mute chorus ya jide kwenye wimbo wa mwanafa ni sawa kwani jide hana mahusiano mazuri na mwenye wimbo. Tatizo mmeshupaa kubishania jambo dogo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza ukimfundisha anakuelewa. Hapa ndipo mnanikumbusha ule msemo wa prof.Kabudi wa 'tofauti kati ya mjinga na mpumbavu'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…