afisa kilimo kumiliki duka la dawa baridi za binadamu sio kujiajiri kupitia sekta ya Afya? afisa ughani wengi wameajiriwa na kujiajiri kupitia kilimo isipokua wengi hawafanyi kwa ukubwa kulinganisha na maarifa waliyo nayo
2/hoja ya kuajiriwa kwa co na DGA ni ukweli CO wana shavu sana ila kwa kujiajiri DGA ni short cut
Ngoja nikujibu hoja zako hapa.
1/Mtu yoyote yule anaweza kuanzisha biashara yaa duka la dawa baridi kama mmiliki, lakini uendeshaji wake unahitaji kisheria ulazima wa Mfamasia au mtaalamu wa Afya. Hivyo lazima uajiri tena mtaalamu wa Afya kukufanyia biashara hiyo.
Bado sioni uhusiano maalum wa moja kwa moja wa Afisa kilimo na kuanzisha biashara ya duka la dawa baridi. Na Ukizingatia kuwa, maafisa kilimo wengi wanapaswa wawe vijijini kuliko mijini, na biashara za duka la dawa baridi hazilipi kabisa Kijijini.
2/Huhitaji kuwa Afisa kilimo ili kuweza kujiajiri kwenye sekta ya Kilimo. Mtu yoyote ule anaweza kujiajiri kwenye Kilimo.
3/Sio jambo rahisi kabisa kwa Msomi wa Kilimo, kutumia kisomo chake pekee kama mtaji wa kujiajiri. Sehemu kubwa ya kilimo hapa Tanzania inafanywa vijijini tena kienyeji sana, katika mazingira hayo Afisa kilimo wa serikali mmoja anahudumia kijiji kizima vizuri kabisa tena bureee. Unajiajiri vipi? Kuuza mbegu? Kuuza mbolea? Kuuza mazao? Dili zote hizo zinapigwa na wajanja wa kawaida kabisa ambao huenda hata darasa la Saba hawakufika.
3/Tuwe wakweli na tuwe wa wazi kabisa, Ushindani wa Kupata nafasi ya kusomea Diploma ya Clinical Medicine(Clinical Officer) ni mkubwa sana kuliko Diploma karibu zingine zote. Wengi waliokosa nafasi ya kwenda kusoma Clinical Officer, basi ndio utafuta alternative ya kusomea Agriculture general nk. Hilo jambo halitokei kwa bahati mbaya, ni matokeo ya fursa zilizopo baada ya kumaliza masomo.