Katika kipindi cha 45 minutes cha ITV leo jioni , mtoa mada alikuwa CD Msuya, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, enzi ya Mwalimu.
Kwa hakika amenikosha sana.
Bado ana data na current za kiuchumi-inaelekea nafuatilia sana current events
Hana papara wala jazba kujibu maswali, na alikuwa composed.
Lakini zaidi ya yote ameiasa nchi mambo makuu yafuatayp
Kwa jinsi alivyokuwa akijieleza kwa ufasaha, tofauti kubwa imeonekana , ukilinganisha na "Mawaziri vijana" wetu waliopo sasa.
- kuwawezesha wakulima kutukia mbegu bora, utaalam bora wakilimo, na mechanization
- ameishauri serikali kupunguza matumizi(kuachana na mashangingi)
- kuongeza uzalishaji mali-katika kilimo n.k. ili kuongeza pato la taifa nahatimaye kupunguza kuporiomoka kwa shilingi yetu
Walioona tupeni maoni, good or bad.
In fwakti hapa kuna ka pointi!!Hii thread nilivyoiona imekaa sana kusifia tu bila kutoa faida za Msuya! Hakuna cha zaidi hapa watu wanaosifia wengi wao wanatoka sehemu aliotoka Msuya, kwa upande wangu mimi sina cha kumkumbuka namuweka kundi moja na Kikwete tu
Tusiwe wabishi wa kila ki2. Mi naamini kila kitu kina changamoto zake. si vizuri kujadili mtu binafsi, tujadili point zenyewe, make baadhi wanachangiaji mjadala hawakuusikia, so wana hukumu moja kwa moja. AlisemaMimi sina tabia ya kusifu sifu mtu kwa kujibu vijiswali vya mtangazaji asiye komaa hata ktk taaluma yake.
Msuya alikuwa Waziri mkuu na alikuwa waziri wa fedha -Hizo ndo nyadhifa kuu mbili. Tuambieni alifanya nini hadi JF itoe sifa kwa msuya?
Najua alihamisha pesa kwa kutumia madaraka yake ili Mwanga wapate umeme.
Msuya ni sifa kwa watu wa Mwanga na haiwezi kuwa sifa ya kujivunia kwa wa-TZ
Kama ni ufisadi naye yumo. Atueleze jinsi COGEFA ya italy ilivyopewa tenda ya kujenga bwawa la Mtera. Tena alikwenda mpaka Italy kusaini mkataba maana tunadhani ni Karamagi tu aliyesafiria mkataba, hata Msuya alifanya hivyo na baada ya hapo ndo akapata vijisenti vilivyompa kiburi na kutuambia kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.
Tusiwe wabishi wa kila ki2. Mi naamini kila kitu kina changamoto zake. si vizuri kujadili mtu binafsi, tujadili point zenyewe, make baadhi wanachangiaji mjadala hawakuusikia, so wana hukumu moja kwa moja. Alisema
: Kipindi kile walikuwa na uwezo wa kukusanya kodi na kulipa mahitaji yote ya nchi, na ziada kidogo kwa ajili ya maendeleo je mkuu wa kaya saa hizi huo ubavu anao?
Pia alisema wao walikuwa wakielekeza mabwana shamba kuelimisha jinsi ya kutumia kilimo cha kitaalamu yaani upandaji wa mbegu kwa kutumia vipimo (kilimo bor) wakati wa sasa ni matrekta yamejazana kwenye yadi flani wakati huo utaalam wa kutumia hakuna.
Vilevile akashauri kuwa serikali ingepunguza matumizi ya kutumia magari ya kifahari kmvile Vx na badala yake zitumike gari za kawaida kama vitara. SASA HAPO KUNA KASORO GANI?
Mi ni mpinzani lkn, facts ziko wazi, other wise the problem is individualismiasis
Msuya was a technocrat who became a politician by accident. I have interviewed him several times and he knows his stuff. Kikwete is not the kind of leader who will search for advice from someone who was bigger before him. He just does not have that in his personality.
President Kikwete described Mzee Msuya as a "True reformer," of the Tanzanian economy whose leadership steered successfully, the transition of the country's economy from controlled to liberal market economy from mid to late eighties.
Mimi personally nimefanya nae kazi ni mchapa kazi mzuri saaaaaaaana.
Napenda kutoa ANGALIZO yeye alikuwa Waziri mkuu na makamo wa Pili wa Rais kwani makamo wa kwanza wa rais alikuwa ni Rais wa Zanzibar.
Tatizo lake kubwa Msuya na ambalo kwa wakti ule lilikuwa ni MKABILA sana. ...QUOTE]
Very true! Msuya ndie alifikia hatua yakuwabagua wapare wa Mwanga na wa Same. Mtakumbuka mgogoro ule wa kidini alikuwa akishinikiza usharika wa Same na Mwanga zitengane kwasababu; misaada mingi iliyokuwa inatoka nje yeye aliiomba special kwa watu wa Mwanga tu. Nilifanya kazi wilaya za Kilimanjaro kwa kipindi fulani. Nikiwa Same, wengi walimuona Msuya ndio kikwazo cha kukosa miradi mingi ya maendeleo; ukizingatia watu vijijini wanategemea miradi inayoletwa na makanisa. Nilipokua Mwanga wengi walimuona Hero. Otherwise nakubali ni mtu mchapakazi, na positives nyingine ambazo wengine wameshazitaja.
Mimi personally nimefanya nae kazi ni mchapa kazi mzuri saaaaaaaana.
Napenda kutoa ANGALIZO yeye alikuwa Waziri mkuu na makamo wa Pili wa Rais kwani makamo wa kwanza wa rais alikuwa ni Rais wa Zanzibar.
Tatizo lake kubwa Msuya na ambalo kwa wakti ule lilikuwa ni MKABILA sana. ...QUOTE]
Very true! Msuya ndie alifikia hatua yakuwabagua wapare wa Mwanga na wa Same. Mtakumbuka mgogoro ule wa kidini alikuwa akishinikiza usharika wa Same na Mwanga zitengane kwasababu; misaada mingi iliyokuwa inatoka nje yeye aliiomba special kwa watu wa Mwanga tu. Nilifanya kazi wilaya za Kilimanjaro kwa kipindi fulani. Nikiwa Same, wengi walimuona Msuya ndio kikwazo cha kukosa miradi mingi ya maendeleo; ukizingatia watu vijijini wanategemea miradi inayoletwa na makanisa. Nilipokua Mwanga wengi walimuona Hero. Otherwise nakubali ni mtu mchapakazi, na positives nyingine ambazo wengine wameshazitaja.
Du kweli kuishi kwngi... kuona mengi!
Ukijua huu.... wengine wanajua huuu.
Hizi ni comments zilizojirudia rudia sana katika thread hii
I do hope wale walio karibu na mzee wetu watmtonya uzuri na ubaya wake.
Hata hivyo his contribution was overall positive.
Wenzetu kama marekani wana sera zinazoliunganisha Taiafa bila ya kujali vyama vyao vya siasa vya republicans na democrats.Na ndiyo maana wako mbali kimaendeleo.Sisi bado sana kwasababu utofauti wa vyama pamoja na uongozi wa kisiasa vinaleta uadui mkubwa na ndio maana wanaoshika madaraka hawataki kuomba ushauri kwa vile wanaogopa ushindani wa kisiasa.Kama hawafuati hata yale mazuri tuliyoachiwa na viongozi waliopita,then usitegemee watawafuata kwa ushauri.Tatizo ni kwamba tofauti na ilivyo kuwa kwa Nyerere hawa viongozi wetu wastaafu wengi wana ushawishi kidogo mno kama wanao kabisa. Sidhani hata kama wanafuatwa kwa ushauri na kama wanafuatwa kutoa ushauri sina ushahidi wa ushauri wao kufanyiwa kazi. Wazee wetu hawa wamekua vyombo vya public relations kwa kualikwa tu kwenye hafla mbali mbali.
Mimi ninge washauri hawa wazee pamoja na kujitokeza kwa mahojiano kama hivi waandike vitabu vingi kuhusu maisha yao na utumishi wao.
wewe ndio bure kabisa kamuulize Christant Maji ya Tanga Mzindakaya ndo anajua Cleopa alifanya nini! Pia nina uhakika haya ulioandika hapa wakati yanatokea lbada hata mama yako alikuwa hajaolewa.leo anazungumzia kuwawezesha wakulima kutumia mbegu bora, kipindi kile alisema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe........
wanadamu wote tuna mazuri na mabaya,lakini bado naamini mzee huyu ni mmoja wa wazalendo wa nchi hii,ambaye mchango wake ktk ujenzi wa viwanda na uchumi hautasahulika kamwe. Vijana wengi waliweza kupatata ajira na maisha bora.