We Agustino Moshi, rudi darasani, msome Shivji huku umetulia, jamaa ni kama nabii fulani hivi, huu mgogoro wa mafuta na Zanzibar, aliutaja mwaka 1994 kwenye andiko lake la 'The Legal Foundation of Union Btn Tanganyika and Zanzibar'.
Unauliza kama kuna Class Strugle leo?. Hivi hujaona kuibuka kwa kasi kwa kundi la 'Petty Bourjuaguse'. Haushuhudii watu wanaoishi maisha ya ki-epa epa wakivunja sheria ni VIP cell ikifuatiwa na dhamana, huku mwizi wa kuku akipigwa hadi kufa.
Kwa taarifa yako, the gap between 'the have' and 'the have not' is widening in a striking speed, huku mtoto wa mmoja akisoma English medium academic school ya mamilioni, mtoto wa mkulima akikosa mkopo aweze kuingia chuo.
Kama una uwezo, nunua land ya mwanao na mwana wa mwanao sasa vinginevyo mwanao na mwana wa mwanao, ataishia kuwa mpangaji maisha yake yote, kwani mwenye nacho, ataongezewa na asiye nacho, atanyang'anywa hata kidogo alicho nacho.
Toka nje usiku, zamani biashara ya usiku ilianzia club maarufu ya Margott, ikaja night clubs na Kinondoni Makaburini, leo nenda Magomeni kwa Macheni, Buguruni kwa Mnyamani, Sinza Kona Bar ushuhudie jinsi wajasiliamali wa miili yao walivyo bize, tena sio mpaka usiku, ni asubuhi, mchana, jioni na usiku ndio usiseme.
Wakati mshahara wa kima cha chini ni 150,000/= kuna watu wanalipwa dola 10,000 kwa mwezi, Tanzania hihi hii!.
Je bado unauliza kama Class struggle zipo?.
'maisha ni struggle for exsistance, survival for the fittest'.