CIA yaionya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CIA yaionya Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280




  *Wazalishaji wachache wanalisha kundi kubwa lisilozalisha
  *Kundi kubwa la watu halina uwakilishi katika vikao vya maamuzi
  *Mwenendo ukiendelea, ipo hatari ya Taifa kukosa viongozi
  Na Waandishi Wetu
  TANZANIA inakabiliwa na pengo kubwa la kizazi (generational gap) ambalo baadaye litajitafsiri katika ukosefu wa viongozi katika kipindi kifupi kijacho, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) limeonya.
  Shirika hilo, katika mtandao wake, linasema Tanzania ni nchi ya kwanza duniani ambayo ina Taifa changa, kwa maana ya kwamba zaidi ya nusu ya raia wake wana umri chini ya miaka 15.
  Kwa kuwa na watu wengi wenye umri wa chini ya miaka 15, ina maana kwamba sehemu kubwa ya raia wa Tanzania inategemea kupatiwa mahitaji muhimu kutoka kundi dogo la wananchi wake, na hivyo kusababisha matatizo makubwa katika uzalishaji wa chakula na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu.
  Kwa mujibu wa shirika hilo, zaidi ya asilimia 90 ya vijana wanaoangukia katika kundi hilo, wapo chini ya umri wa kwenda shule au wapo katika shule za msingi, na kwa hiyo si wazalishaji.
  Takwimu za shirika hilo zinaonyesha kwamba Watanzania wenye umri wa miaka 0 hadi 14 ni asilimia 44.3 wakati wenye umri wa kati ya miaka 15 na 64 ni asilimia 53.1. Aidha, takwimu hizo zinasema idadi ya Watanzania wenye umri wa kuanzia miaka 65 na kuendelea wanafikia asilimia 2.6, wakati wenye umri wa miaka 0 hadi 29 ni asilimia 70.
  “Zaidi ya nusu ya watu wanaoangukia katika kundi la pili la watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 64 ni wategemezi,” linasema shirika hilo.
  Chini ya mfumo wa elimu wa Tanzania, vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 20 wapo katika hatua mbalimbali za elimu yao ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Mfumo wetu wa elimu unamtaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 kuwa kidato cha kwanza, wakati yule mwenye umri wa miaka 20 anamaliza kidato cha sita.
  Hata shirika hilo la ujasusi la Marekani linashangaa ni kwa vipi Tanzania imeweza kuwa na pengo kubwa la namna hiyo la kizazi, ingawa lilijaribu kueleza kwamba ukimwi unaweza kuwa umechangia kwa kiwango kikubwa, lakini likatoa takwimu zinazoonyesha kwamba kwa Tanzania, ukimwi si tishio kubwa kwa maisha ya Watanzania kiasi cha kusababisha uwiano usio sawa kati ya vijana na wazee.
  Wakati katika nchi nyingine kama Lesotho ukimwi umepunguza kwa kiasi kikubwa mategemeo ya kuishi (life expectance) ya raia wa nchi hiyo na kufikia wastani wa miaka 38, kwa Tanzania shirika hilo linaonyesha umri wa Mtanzania wa kuishi ni miaka 51.4. Katika takwimu hizo, wanaume wanatarajiwa kuishi kwa wastani wa miaka 50.06 wakati wanawake wanatarajiwa kuishi kwa wastani wa miaka 52.88.
  Kwa umri huo wa kuishi, Tanzania ni nchi ya 206 duniani. Nchi ya kwanza kwa umri mrefu wa kuishi ni Maccau, ambayo ni sehemu ya China. Wastani wa watu kuishi katika nchi hiyo ni miaka 84.36 wakati nchi ya mwisho, yaani ya 224 kwa wastani wa kuishi, ni Angola ambayo wastani wa watu kuishi ni miaka 38.20. Haya ni makadirio ya mwaka 2008 ambayo kimsingi ndiyo makadirio mapya yaliyopo.
  CIA inasema sehemu kubwa ya nchi zinazokabiliwa na tatizo hilo ni zile ambazo watu wake wanazaa sana. Na katika kundi hilo la nchi ambazo zimeshindwa kudhibiti uzazi wa watu wake, Tanzania ni nchi ya 39 kati ya nchi 224, ikiwa na wastani wa kila mwanamke kuzaa watoto watano katika kipindi cha uhai wake. Nchi zilizo juu ya Tanzania ni pamoja na Niger ambayo ni ya kwanza na wastani wa kuzaa ni watoto 7.75.
  Nchi nyingine, idadi ya watoto wanaozaliwa kwa mwanamke mmoja ikiwa katika mabano ni pamoja na Uganda (6.77), Mali (6.62), Somalia (6.52), Burundi (6.33), Burkina Faso (6.28), Congo DR (6.20), Angola (6.12), Ethiopia (6.12), Congo (5.84), Liberia (5.79), Sahara Magharibi (5.61), Afghanistan (5.60), Malawi (5.59), Oman (5.53), Mayotte (5.50), Benin (5.49) na Sao Tome and Principe (5.33).
  Nchi nyingine zenye kuzaa watoto wengi ni Chad (5.31), Guinea (5.20), Msumbiji (5.18), Zambia (5.15), Madagascar (5.14), Rwanda (5.12), Guinea ya Ikweta (5.08), Gambia (5.04), Ukanda wa Gaza (5.03), Sierra Leone (5.00), Yemen (5.00), Senegal (4.95), Nigeria (4.91), Comoros (4.84), Togo (4.79), Eritrea (4.72), Gabon (4.65), Guinea-Bissau (4.65), Kenya (4.56) na Sudan (4.48).
  Ingawa taarifa za kiafya zinasema kuwa ugonjwa wa ukimwi unaweza kuwa chanzo cha hali hiyo ya kuwa na watoto wengi zaidi ya watu wazima, hata hivyo idadi kubwa ya watu wanaotajwa kufa kwa ukimwi ni vijana, na hiyo ingekuwa sababu kwa takwimu za vijana kuwa chini ikilinganishwa na hali halisi ya sasa ya nchi.
  Lakini pia, shirika hilo linaonyesha kuwa asilimia 5.7 ya Watanzania wanaishi na virusi vya ukimwi, miongoni mwao wanawake wakiwa asilimia 6.6 wakati wanaume wakiwa asilimia 4.6. Hiyo ni sawa na jumla ya watu milioni 1.6 wanaohisiwa kuishi na virusi vya ukimwi
  Pamoja na kwamba kuna uwiano mkubwa wa vijana katika wakazi wa Tanzania, wingi wa vijana haujionyeshi sehemu nyeti na muhimu za Taifa, na hasa zile za uwakilishi wa wananchi bungeni na katika baraza la wawakilishi.
  Kwa mfano, wakati vijana wenye umri wa kati ya miaka 0 na 29 nchini ni asilimia 70, kundi hili lina uwakilishi 0 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuna hata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 29 aliyemo katika Bunge la Tanzania.
  Tangu lilipoingia madarakani Bunge la sasa, 2005, ni vijana watatu tu waliokuwa na umri huo wa chini ya miaka 29. Hao ni Mhonga Luhwanya wa Chadema (Viti Maalumu) na Amina Chifupa CCM (Viti Maalumu) na Kabwe Zitto (Chadema – Kigoma Kaskazini). Amina Chifupa sasa ni marehemu.
  Kutokana na uwakilishi tenge, vijana wengi wa Tanzania wamekuwa hawana mwamko wa mambo ya siasa na hasa mambo yanayoendelea katika Bunge la Tanzania. Wengi wao wanayaona kama ni mambo ya wazee.
  Hoja chache zinazotolewa na vijana wa kizazi kinachokaribiana na wao, ndizo zinazosikilizwa na kujadiliwa na vijana hata waliopo vijijini. Kwa mfano, hoja zinazohusu madini, zimewagusa vijana kwa sababu ya misukosuko iliyomkumba Zitto Kabwe alipotoa hoja ya kukosoa utaratibu wa Mkataba wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Umri wa Zitto ni miaka 33 sasa.
  Uchaguzi mkuu ujao, unatarajiwa kupanua pengo la uwakilishi bungeni iwapo azma ya kuwa na uwakilishi wa wanawake wa asilimia 50 itafanikiwa. Inatarajiwa kwamba wanawake watakaoingia bungeni kwa utaratibu huo, wengi ni wale wenye umri wa zaidi ya miaka 30, na hivyo kufanya pengo hilo la uwakilishi wa vijana kuwa kubwa zaidi.
  Kwa sasa, asilimia 70 ya Watanzania haina uwakilishi katika chombo chao cha kutunga sheria kwa sababu hakuna mbunge hata mmoja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye umri chini ya miaka 30. Mbunge mdogo kuliko wote kwa sasa, ni Mhonga, mbunge wa Viti Maalumu Chadema, ambaye ana umri wa miaka 31.
  Shirika hilo linasema nchi zote zinazoangukia katika kundi lenye watoto wengi kuliko watu wazima, linakabiliwa na mzigo mkubwa wa kuelekeza nguvu zake katika ujenzi wa taasisi za elimu kwa kuwa sehemu kubwa ya watu katika kundi hilo ama hawajaenda shule au wamo ndani ya elimu, lakini ngazi ya shule za msingi.
  CIA yaionya Tanzania
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hawa wanatakiwa kupuuzwa.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nasisi tubinafsishe na usalama watu kwani kama kila kitu tunangoja kuambiwa na marekani sasa nini tunachoweza
   
 4. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,428
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa hali hiyo kupata maendeleo ni kazi kubwa sbb kiwango cha wategemezi ni kikubwa mno. Kumbe ndo maana tunalalamika uchumi mgumu!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Upuuzi mtupu ni CIA hao hao wameua kiwanda chetu cha Nyumbu, ni hao hao wanaisambaratisha DRC, n.k. watuache na mambo yetu wenyewe.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kumbe habari yenyewe ni kutoka gazeti la Rostam Aziz.....hovyo!!
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  tobaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,379
  Trophy Points: 280
  Mambo yanahusu takwimu si ya kupuuzwa, ila uchambuzi wa takwimu nayo ni fani inayojigemea kwa Tanzania bado tuko nyuma ndio maana Redet wanaitisha kura yao ya maoni, wanawahoji watu 2000 kati ya zaidi ya milioni 40 waliopo kuwa JK yuko juu, na Ikulu wanatoa statement kuipongeza Redet.

  Binafsi sikubaliani na matokeo ya takwimu hizi za CIA, hawa jamaa ni wapishi wazuri wa mambo fulani, ukiona wanaizungumzioa nchi fulani kuhusu hali yake kiusalama, ujue chungu kiko jikoni, chakula kikiiva kitapakuliwa tule.

  Kabla ya kuivamia Iraq, walitoa documents iitwayo "Axis of Evil", wakaziweka nchi mbalimbali zikiongozwa na Iraq. Wakajaribu kuitumia UN kuidhinisha udhalimu wao wakashindwa, wakasemezana wao kwa wao (Nato), wakaivamia kwa kisingizio cha kusaka WMD, wakaivamia Iraq, hakuna cha WMD wala cha nini. Ni kweli Saddam kaua Wakurd kwa mamia, lakini Marekani imeua maelfu kwa maelfu!

  Hivyo mkishaona tunatajwa tajwa na Marekani, enda ikawa tayari wana uhakika na mafuta yetu, hilo la tawimu ni zuga tuu ama danganya toto.
   
 9. stanluva

  stanluva Senior Member

  #9
  Jun 7, 2010
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  We have to be very carefull maana hao jamaa ni noma! Wana propaganda za hatari sasa tukiwa na kiongozi ambaye hana msimamo au uchungu na wananchi wake! Haaa tumekwisha!
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,183
  Trophy Points: 280
  Huhitaji CIA kujua kwamba asilimia ya watu tegemezi Tanzania ni kubwa. Hata hao wenye umri wa kufanya kazi, uzalishaji ni mdogo, wengi wao bado wako katika subsistence farming na umachinga, wengine wengi wako unemployed etc.

  Katika uchumi wa subsistence na "living off the land" kuwa na watoto wengi ni fahari na uwekezaji katika free labor.Katika uchumi wa dunia ya sasa ni a ticking timebomb.
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Wameuaje kiwanda cha Nyumbu acha ubabaishaji bwana? tule wenyewe then tusingizie CIA
   
Loading...