CIA walimtaka Chifu Thomas Mariale, Fabian Society walimtaka Chifu Kidaha, Jesuit wakamtaka Julius Nyerere

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 chini ya Fabian Society za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jeisuti za mwaka 1942 kupitia kwa Kasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka, tangu hapo walimbatiza pale Tabora na kumbadili jina na kuitwa Julius Kambarage Nyerere, hii ilikuja baada ya kifo cha Chifu Burito, awali kulikuwa na mwendo mrefu wa kumshawishi Chifu Burito akubali mtoto wake ajiunge nao lakini mzee yule alipinga, .

Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia....

Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Kwa undani zaidi wa haya unaweza kusoma Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,
+255715865544/+255755865544

FB_IMG_1517176483187.jpg
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 chini ya Fabian Society za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jeisuti za mwaka 1942 kupitia kwa Kasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka, tangu hapo walimbatiza pale Tabora na kumbadili jina na kuitwa Julius Kambarage Nyerere, hii ilikuja baada ya kifo cha Chifu Burito, awali kulikuwa na mwendo mrefu wa kumshawishi Chifu Burito akubali mtoto wake ajiunge nao lakini mzee yule alipinga, .

Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia....

Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

[HASHTAG]#Kitabu[/HASHTAG]: Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

0715865544
0755865544

Na Yericko Nyerere

View attachment 686640

latest
 
Acha kuongopa CIA haikuwa na maslahi yoyote hapa kwetu labda kama unachanganya na Kongo, isitoshe Nyerere aliandaliwa na Waingereza kuja kukabidhiwa nchi tangia mwanzo, huyo Mareale kwanza siyo Chief wa Wachaga bali Wamarangu usichanganye mambo, Wakibosho au Wamachame hawamjui na wala hawakuwa na mpango naye!
 
Uyu wasasa alitakiwa na kina nani Mkuu....?

Tafadhali usije leta mambo ya kibantu, sijui Nyankole, sijui Ubelgi......

Vip pia waliopita Baada ya Mtoto Wa burito....?

Kujua umetokea wap, upo wap ni jambo la muhimu sana....!
 
Acha kuongopa CIA haikuwa na maslahi yoyote hapa kwetu labda kama unachanganya Kongo, isitoshe Nyerere aliandaliwa na Waingereza kuja kukabidhiwa nchi tangia mwanzo, huyo Mareale kwa siyo Chief wa Wachaga bali Wamarangu usichanganye mambo, Wakibosho au Wamachame hawamjui na wala hawakuwa na mpango naye!
Nakupa na nyaraka lakini unaacha kuisoma unabeba hisia zako na kuweka jibu kijana?
 
Unajitahidi sana kuandika, ila mapungufu yako makuu ni kukosa ueledi wa kupambanua story za kweli na vijiweni.

Nguvu unayoitumia kuamini story za vijiweni ka a ungeitumia kufanya utafiti angalau hata kidogo tu basi ungekuw mwandishi mzuri sana.

Hakuna uandishi mgumu kama ule wa kihistoria na ule wa kiuchunguzi.

Mwaka 1942 Nyerere alikuwa na miaka chini ya 25.
 
Unajitahidi sana kuandika, ila mapungufu yako makuu ni kukosa ueledi wa kupambanua story za kweli na vijiweni,
Nguvu unayoitumia kuamini story za vijiweni ka a ungeitumia kufanya utafiti angalau hata kidogo tu basi ungekuw mwandishi mzuri sana
Hakuna uandishi mgumu kama ule wa kihistoria na ule wa kiuchunguzi,

Mwaka 1942 nyerere alikuwa na miaka chini ya 25
Umeshaambiwa Jeisuti walianza kumfuata akiwa mdogo kabisa kule kijijini kwao, wakaja kufanikisha baada ya miaka 20 huko tabora... Sasa kinachokushangaza ni kipi?
 
Hisia gani? Huyo Mareale alikuwa hakubaliki na hao wanaojiita Wachaga, kwanza hata Watu Rombo jirani yao walikuwa hawamtambui sasa angemuongoza nani?
Huo ndio ufinyu wakufikiri kijana, mimi nakupa kile mashirika hayo mumiani yalichokuwa yakifikiri... Wewe unaleta mahaba yako binafsi.... Pole sana hukutarajia kusikia hili ndugu....

Yupo mzee wako anaitwa Mohamed Said ngoja aje aanze kulialia hapa akisikia habari hizi..
 
Unajitahidi sana kuandika, ila mapungufu yako makuu ni kukosa ueledi wa kupambanua story za kweli na vijiweni,
Nguvu unayoitumia kuamini story za vijiweni ka a ungeitumia kufanya utafiti angalau hata kidogo tu basi ungekuw mwandishi mzuri sana
Hakuna uandishi mgumu kama ule wa kihistoria na ule wa kiuchunguzi,

Mwaka 1942 nyerere alikuwa na miaka chini ya 25
Wewe nawe ni kiumbe wa ajabu, kwa hiyo mtu akiwa na umri chini ya miaka 25 hawezi kuandaliwa kuwa kiongozi? Haujui kuwa talents za watu huwa zinajitokeza mapema? Tatizo umekurupuka kumjibu Nyerere bila kutafakari nakujikuta ukiandika pumba tu.
 
Huo ndio ufinyu wakufikiri kijana, mimi nakupa kile mashirika hayo mumiani yalichokuwa yakifikiri... Wewe unaleta mahaba yako binafsi.... Pole sana hukutarajia kusikia hili ndugu....

Yupo mzee wako anaitwa Mohamed Said ngoja aje aanze kulialia hapa akisikia habari hizi..

USA hawakuwa na maslahi yoyote hapa kwetu hivyo wasingeweza kujali au kujihusisha na nani angekuwa Raisi, na ndiyo maana TZ imesalimika na conflicts nyingi zinazolikumba bara la Afrika kwa sababu Wazungu hawana maslahi makubwa kiivyo hapa kwetu kulinganisha na nchi kama Kongo, Somalia au hata Kenya na Uganda na wengineo!
 
Hawana maslahi kivipi,kila siku kuna foundation toka western zinaletwa bongo kuchota maliasili sema sisi sio threat kwao pia ni base yao katika kazi zao nchi zenye machafuko!!muulize mwanaccm mwenzio Prof.Kabudi atakwambia TZ ndio nyonga ya Afrika baada ya congo
 
Pole sana.... Jitahidi kusaka taarifa usiishi kwakukariri......
 
Back
Top Bottom