Chuo kikuu UDSM maringo kibao ila hamna lolote

Chuo kikuu UDSM maringo kibao ila hamna lolote

mkuu bwana mimi sitaki mabishano na wewe napenda kuongelea reality sikufichi ule utegemezi wa udsm haupo tena na sikusema kwamba wanatoa elimu mbaya hapana ila wamezidisha masifa na maringo na kama uamin kwa hizo sifa wanazozipata sidhani kama kuna mtu au taasisi ingeajiri mwanafunzi kutoka kwenye vyuo vingine zaid ya udsm. ila kuna vyuko viko poa na vinajulikana. kila chuo kina sifa yake sasa kwa mambo ya IT udom naamin wako vizuri, pia St joseph wahind wako vizur sana kwa elimu zao sijui kama umewahi ulizia hiyo engnieering ya st joseph dzm, cheki muhas, bugando kcmc, sua, mzumbe n.k nakuhakikishia udsm ni miaka hiyo siyo sasa saivi ushindani umeongezeka kila chuo kinataka kujikuta bora. pia narudia tena sikusema udsm mbaya hapa bali ni overcredited
Ukitaka kujua chuo gani bora Africa au Tz tembelea website ya WEBOMETRIC
 
mkuu unajua nini samahani sana hakuko kwenye mashindano ya kuandika, hivo ni vitu vidogo vidogo sana kikubwa nilikua nataka ujumbe ueleweke tuweze kuzungumzia hili swala.
Kwa uelewa wako wewe ni vitu vidodo Sana mkuu..
Hongera!
 
Nafikiri unawaonea UDSM, wanafunzi wanapo omba UDSM huchagua wale wenye vigezo vyao pamoja na cut off point yao. Halafu huwapanga kwa point kuanzia mwenye nyingi hadi chache kabisa thereafter wanaangalia wana nafasi ngapi. Kitu kizuri kuhusu UDSM wanaweka mtandaoni majina ya wale watakaowadahili na wale ambao wamepelekewa na TCU lakini wao wameamua wasiwadahili na hutoa sababu. Huanika kila kitu toka form 4 performance and form 6 performance. Na hawachukui div 1 na 2 pekeyao, inategemea na ushindani na cut-off yao. Wanafunzi kwa sababu moja au nyingine kwa program fulani hugombania kwenda UDSM hivyo itakuwa haina maana chuo kuchukua mwenye ufaulu mdogo na waache mwenye ufaulu mkubwa. Pia lazima minimum vigezo vya programu vizingatiwe. Kama huyo dogo uliyemuelezea amekuwa na vigezo walivyoweka na hakuchukuliwa wakati nafasi ipo una haki ya kulalamika vinginevyo si sawa. Swaga za vijana waa UDSM mimi sitaki kuzizungumzia.

hapo kwenye redi ndo jazba yangu inapotokea niliona kama ubaguzi flan ivi pia nilishawahi kukuta lawama kama hiyo humu ndani
 
Kwa hili, nadhani wanaochagua UDSM ya kwanza ni wanafunzi wanaotokea mikoani (vijijini) ambao wanaona kwenda Dar kama ni adventure! Lakini ki ukweli kabisa, heshima ambayo UDSM imebaki nayo ni sawa na ile ya mzee. Kuna ule msemo kwamba "uzee dawa". Tunawaheshimu mababu tukiamini kuwa wana busara na hekima lakini hawa watu siyo productive.
Wengi ni vipofu,viziwi,vibogoyo,....... Siyo energetic wala competitive! Hii ndiyo UDSM iliyobaki.

Kimsingi nimekutana na wanafunzi wabovu kabisa wa UDSM na wanafunzi wazuri sana kutoka vyuo vingine. Kuna vyuo vizuri tu hapa Tz ila huwezi kusikia kelele za majivuno. Vipo SUA, MUHIMBILI, NELSON MANDELA,......
UDSM ni kama timu ya Uingereza. Vyombo vya habari , hasa vya Uingereza (BBC,SKY NEWS,..) vitaipamba weee lakini ikiingia kwenye michuano ni kuchezea kichapo tu. Biashara ni matangazo.......!

Uzi huu nimeuchangia kwa jumla jumla kwa kuwa kuna kitu nataka kukifanya, ila usipofutwa ntarudi tena.
pamoja mkuu kuwa nawatu wenye deep knowledge kama wewe ni raha sana, waambie hao zama zinabadilika kwa sasa haiwez tena kuwa tegemezi kama zamani sababu zaman si ilikua peke yake, sasa hivi ushindani upo
 
Yaani ndugu yangu kumbe ni kisirani kukosa nafasi udsm hivi je,huyo mtu wako angepata mafasi ungeyasema hayo?Chuo hicho achana nachoaana historian yake ni kubwa,unaposema hayo unaoneka km hujitambui,sasa kwanini ulikuwa unaomba nafasi hapo kama unajua hakina sifa?
hapana mkuu ni overcredited, majivuno kibao wakati ni cha kawaida tuu, sasa zama zimebadilika pia sikusema kwamba ni kibaya hapana nachokasirika hapa ni majivuno
 
Kuna ukweli fulani katika andiko lako, lakini kuna vitu unavichanganya na vingine unaharibu.
Mf ni kweli kabisa kuwa chuo chetu tegemezi kinabebwa na historia ya elimu ya nchi yetu. Zaidi ya hapo hakuna utofauti mkubwa wa wanafunzi wanaohitimu UDSM na wale wa vyuo vingine.

Hatusikii tafiti za maana katika sayansi, mawasialiano na teknohama, uandisi, n.k. Tulitegemea chuo cha kimataifa angalau tuwe na devepment projects kwenye engineering, artificial intelligence, software engineering, computer science, physics, angalau tungesikia hata circuit ya redio basi ikiwa katika development, lakini hakuna. Hata saa ya mkono imetushinda wanaUDSM.

Raisi wetu kasomea Udsm na amekaa UDSM tangu undergraduate mpaka doctorate, kama emamua Warwanda waje kutusaidia IT jua kabisa anafahamu kilichoko hapo UDSM.

Wakati huo huo wanafunzi wa UDOM kitivo cha CIVE wanazidi kupasua anga kimataifa. Juzi myocoo kashika namba tatu Cape town S. Africa. UDOM nzima wanatumia SR- ambayo ni students record system na ni kazi wa vijana wa UDOM. Ile ARIS sijui nani katengeneza. Nimefatilia project za mwaka huu engineering ya CIVE imejitahidi sana. Watu wanaonesha ubunifu wao kwa vitendo.

Nafikiri tufike sehemu tuanze kuviainisha vyuo vyetu kwa kazi wanazofanya na si alama zinazowapeleka chuo. Mf mwaka 2013 kuna software company ilitoa kazi za IT, walihitaji watu 10 na 7 kati yao ni vijana wa CIVE UDOM. DIT nao wamekuwa wakijitahidi kuonyesha kazi zao pia.

Mawazo yangu ni kuwa kila chuo kinafanya vizuri katika kitivo fulani.

Mfano,
Ukizungumzia sheria utakuta UDSM na MZUMBE wako vizuri kuliko vyuo vingine;
UALIMU-UDSM
TEKNOHAMA NA MAWASILIANO- UDOM
KILIMO-SUA
UDAKTARI- MUHIMBILI
ENGINEERING- DIT, UDSM
SOSHIOLOJIA- UDMS

Kwa hiyo kuna mahali vyuo vingine vinafanya vizuri kuliko UDSM japo UDSM inafanya vizuri katika fani zilizo nyingi.

Cha msingi tufanye kazi tuache maneno matupu. Labda tunapaswa kujiuliza "why do 'A' graduates work for Cs and why Bs work for government after their studies?"

Alafu hili somo la communication skills LG 102/101 (WRITTING, reading and listening) ni muhimu sana. Tusilidharau kama tunataka kuwa wanataaluma.
hizi ndio hoja nazozitaka mkuu, samahani nlikua natumia simu sijaweza pata mda wa ku type vizur, ule utegemezi wa udsm haupo tena ushindani ni mkubwa sana. pika kila chuo sasa kina sifa yake
 
Ukitaka kujua chuo gani bora Africa au Tz tembelea website ya WEBOMETRIC
sawa mkuu huko nako nitapita sababu mimi sipend kugusia vitu juu juu napenda pitia practically na facts nakupa, embu jaribu kupita pita halafu n=uniambie watu gani wanafanya vizur katika fani, uliza hata human resource manager wa sehemu mbali mbali watakwambia na utaona mwenyewe. inshort sasa kila chuo kina sifa yake
 
Kuna ukweli fulani katika andiko lako, lakini kuna vitu unavichanganya na vingine unaharibu.
Mf ni kweli kabisa kuwa chuo chetu tegemezi kinabebwa na historia ya elimu ya nchi yetu. Zaidi ya hapo hakuna utofauti mkubwa wa wanafunzi wanaohitimu UDSM na wale wa vyuo vingine.

Hatusikii tafiti za maana katika sayansi, mawasialiano na teknohama, uandisi, n.k. Tulitegemea chuo cha kimataifa angalau tuwe na devepment projects kwenye engineering, artificial intelligence, software engineering, computer science, physics, angalau tungesikia hata circuit ya redio basi ikiwa katika development, lakini hakuna. Hata saa ya mkono imetushinda wanaUDSM.

Raisi wetu kasomea Udsm na amekaa UDSM tangu undergraduate mpaka doctorate, kama emamua Warwanda waje kutusaidia IT jua kabisa anafahamu kilichoko hapo UDSM.

Wakati huo huo wanafunzi wa UDOM kitivo cha CIVE wanazidi kupasua anga kimataifa. Juzi myocoo kashika namba tatu Cape town S. Africa. UDOM nzima wanatumia SR- ambayo ni students record system na ni kazi wa vijana wa UDOM. Ile ARIS sijui nani katengeneza. Nimefatilia project za mwaka huu engineering ya CIVE imejitahidi sana. Watu wanaonesha ubunifu wao kwa vitendo.

Nafikiri tufike sehemu tuanze kuviainisha vyuo vyetu kwa kazi wanazofanya na si alama zinazowapeleka chuo. Mf mwaka 2013 kuna software company ilitoa kazi za IT, walihitaji watu 10 na 7 kati yao ni vijana wa CIVE UDOM. DIT nao wamekuwa wakijitahidi kuonyesha kazi zao pia.

Mawazo yangu ni kuwa kila chuo kinafanya vizuri katika kitivo fulani.

Mfano,
Ukizungumzia sheria utakuta UDSM na MZUMBE wako vizuri kuliko vyuo vingine;
UALIMU-UDSM
TEKNOHAMA NA MAWASILIANO- UDOM
KILIMO-SUA
UDAKTARI- MUHIMBILI
ENGINEERING- DIT, UDSM
SOSHIOLOJIA- UDMS

Kwa hiyo kuna mahali vyuo vingine vinafanya vizuri kuliko UDSM japo UDSM inafanya vizuri katika fani zilizo nyingi.

Cha msingi tufanye kazi tuache maneno matupu. Labda tunapaswa kujiuliza "why do 'A' graduates work for Cs and why Bs work for government after their studies?"

Alafu hili somo la communication skills LG 102/101 (WRITTING, reading and listening) ni muhimu sana. Tusilidharau kama tunataka kuwa wanataaluma.
mkuu nashukuru kuona unatambua mchango wetu wana CIVE,hii ni college bora kabisa ya IT hapa tz.Nami nilikuwa mmoja wao wa waliohudhuria hizo project za final year hakika ni project bora kabisa.CIVE ndio tegemeo la IT taifa hivi karbuni na miaka mingi ijayo.Mimi ni mwanafunzi wa CIVE nipo hapa nasoma Bsc.TE ila nikiri kuwa shule inayopigwa hapa si lelemama kama wengi wanavyoiongelea UDOM.Nadhani kuna haja ya wanaoiongelea UDOM wawe wanatumia EXCEPTIONAL case ya CIVE katika mabaya yote ya UDOM.Pia nikukumbushe mkuu kuwa umesahau kuongelea huu mtandao wa kijamii unaoitwa 2daysky uliotengenezwa na mwanafunzi wa CIVE Elisha.Mtandao huu uliwahi kutengenezewa thread humu .Ni hayo tu mku na tegemea mengi sana kutoka CIVE yanakuja.
 
Vipanga gani mpaka div 3 baadhi ya course wapo au nawao ni vipanga,sema mnabebwa na historia kama vile ilivyokuwa Azania kuilinganisha na Tandahimba kila mtu angeona Azania ni shule bora zaidi.
POLE sana mkuu...
Kozi ambazo zina hao unaosema wana div 3 kwa pale UDSM ni zile ambazo watu waliofanya maombi ni wachache kulinganisha na idadi inayotakiwa...
Karibu UDSM mkuu...
Pia kama una ndugu yako mwenye div 3 anataka kuchukua degree,mwambie afanye maombi ya kwenda UDSM...
naamin atapata NAFASI...!
 
mkuu nashukuru kuona unatambua mchango wetu wana CIVE,hii ni college bora kabisa ya IT hapa tz.Nami nilikuwa mmoja wao wa waliohudhuria hizo project za final year hakika ni project bora kabisa.CIVE ndio tegemeo la IT taifa hivi karbuni na miaka mingi ijayo.Mimi ni mwanafunzi wa CIVE nipo hapa nasoma Bsc.TE ila nikiri kuwa shule inayopigwa hapa si lelemama kama wengi wanavyoiongelea UDOM.Nadhani kuna haja ya wanaoiongelea UDOM wawe wanatumia EXCEPTIONAL case ya CIVE katika mabaya yote ya UDOM.Pia nikukumbushe mkuu kuwa umesahau kuongelea huu mtandao wa kijamii unaoitwa 2daysky uliotengenezwa na mwanafunzi wa CIVE Elisha.Mtandao huu uliwahi kutengenezewa thread humu .Ni hayo tu mku na tegemea mengi sana kutoka CIVE yanakuja.
waambie baba
 
hapo kwenye redi ndo jazba yangu inapotokea niliona kama ubaguzi flan ivi pia nilishawahi kukuta lawama kama hiyo humu ndani
Swaga za hawa vijana wa UDSM (baadhi yao) zisikusumbue. Kuna areas ambazo chuo chao kiko nyuma na areas nyingine wako vizuri. Uwepo wa vyuo vingine unawapa watu choice. Tatizo wengi huangalia chuo hata kabla ya kuangalia program wanayotaka imekaaje kwenye vyuo tofauti.But as long as vijana wengi wanataka kwenda UDSM cut off point yao itakuwa juu lakini pia vyuo vingi havijitangazi ya kutosha wengine hata prospectus huzipati kwenye mitandao yao au unakuta ni version za zamani. UDSM wako vizuri kwa hili na kama nilivyoeleza hapo juu admission zao naziona ni za uwazi zaidi.
 
waambie baba
Punguzeni HASIRA ndugu zetu wa DODOMA...
maGAP yapo tu,tangu enzi za MABABU zetu...
Ila Nina wasiwasi na hii CHUKI mnayoijenga dhidi ya wana DARUSO...
Taratibu musije mukaWADHURU mkikutana nao huko kwenye harakati za MAISHA kama field na kwingineko..!
 
Swala la Chuo, Degree, Masters, Phd..They are nothing at all, kama havijaweza kubadili maisha yako. Katika Kampuni, Utendaji serikalini, Whatever you are doing....Tunafanya evaluation.
Plan
Do
Check
Act
Kama umesoma Chuo chochote kile duniani hata Harvad, we do not care! We need output! we are less concerned with input, we need performance at work, performance to change your life,
Mnanipa Hasira sana,
Elimu itakuwa haijawasaidia kama Malengo ya hiyo elimu hayajafikiwa, kwa mfano:
Objectives or Goals za elimu ni:
1.Kuondoa ujinga
2.Kupambana na Maradhi
3.Kukusaidia kubadili na kutawala mfumo wa maisha
4.Kuweza kufanya analysis na kutoa majibu sahihi yatakayotusaidia kuondoa au kupunguza matatizo

suggestions:
Wale vipanga wa habari chukueni hii:
Ili elimu ya Tanzania ikidhi mahitaji napendekeza Iuedwe tume ya Elimu kuangalia upya yafuatayo:
1.Kufanya upya tathmini, elimu ya Tanzania kuanzia Kindergaten mpaka University Degree kama Mitaala iliyopo inakidhi soko la ajira, soko la kujiajiri
2.Tume ijifunze Mitaala ya Marekani, China, Israel, Japanese, India..Kuhusu Mitaala yao Juu ya Elimu ili Tuone kama Nchi yetu elimu yake iko wapi mpaka sasa, haiwezekani tuazime wataalamu wa IT au toka Korea kwa ajili ya Matumizi yetu, Siri zetu zitabebwa sasa,
3.Serikali ya Tanzania Itoe Wanafunzi kwenda kusoma at least kila mwaka wanafunzi 500 tu, kwa mfano
kada ya Udaktari Bingwa 100, Utaalamu wa Mawasiliano 100, Engineering 100, Geologist 100, Uhasibu 100
Hii ina maana baada ya Miaka 10, Tutakuwa na wataalamu wasiopungua 5000.
4.Serikali Iwekeze Zaidi katika Mambo ya Gesi na Oil, Madini na Nishati, kwa sababu sekta hii itatusaidia sana siku za usoni, Nina uhakika zaidi ya 70% ya ardhi ya Tanzania ni Rasilimali, yani Madini, na Gesi, Acha MAji ambayo yanaonekana
so tunataka wataalamu wetu.
5.Kila Tunachotaka kukifanya, Nashauri sana Tufanye utafiti wa kutosha ili Tukiamua basi Tufanye angalau mpango wa Miaka 100 ili Tuokoe Vizazi vijavyo zaidi, Mimi nashauri tusibanguane! uwe Mzumbe, Udsm, SUA n.k hivi ni vyuo tu wala havina issue sana na maisha yetu, Acheni hayo mambo! Je waliosoma HARVAD WASEMEJE??
 
Kwa hili, nadhani wanaochagua UDSM ya kwanza ni wanafunzi wanaotokea mikoani (vijijini) ambao wanaona kwenda Dar kama ni adventure! Lakini ki ukweli kabisa, heshima ambayo UDSM imebaki nayo ni sawa na ile ya mzee. Kuna ule msemo kwamba "uzee dawa". Tunawaheshimu mababu tukiamini kuwa wana busara na hekima lakini hawa watu siyo productive.
Wengi ni vipofu,viziwi,vibogoyo,....... Siyo energetic wala competitive! Hii ndiyo UDSM iliyobaki.

Kimsingi nimekutana na wanafunzi wabovu kabisa wa UDSM na wanafunzi wazuri sana kutoka vyuo vingine. Kuna vyuo vizuri tu hapa Tz ila huwezi kusikia kelele za majivuno. Vipo SUA, MUHIMBILI, NELSON MANDELA,......
UDSM ni kama timu ya Uingereza. Vyombo vya habari , hasa vya Uingereza (BBC,SKY NEWS,..) vitaipamba weee lakini ikiingia kwenye michuano ni kuchezea kichapo tu. Biashara ni matangazo.......!

Uzi huu nimeuchangia kwa jumla jumla kwa kuwa kuna kitu nataka kukifanya, ila usipofutwa ntarudi tena.
Mimi ni mkazi wa Dar miaka mingi ila chaguo la kwanza lilikuwa UDSM na bahati nzuri nikapata.
Siungi mkono kuwa ni wale wa vijijini.
 
naweza kusema kulingana na ukongwe wa chuo kikuu cha UDSM kimekifanya kijulikana sana ndani na nje ya nchi pia watu maarufu wakiwemo marais, watoto wa marais na wasomi wengine wamesoma hapo.
ni kwa nini wamesoma hapo sababu ni kwamba bado nchi yetu ilikua changa miaka hiyo ya zamani na kilikua ni chuo pekee kuanzishwa hapa nchini inshort watanzania walikuwa wanakitegemea.
umri wake kama chuo kinachotegemewa na wananchi enzi hizo lakini sio saivi kimeweza kuzaa branches kibao ikiwemo SUA, ARDHI, MUHAS, hivi sasa vinajitegemea venyewe, pia kuna campas vingine kibao bado zipo chini ya chuo cha taifa enzi hizo kama mkwawa, must, duce, n.k
ukiangalia kulingana na hali yetu ilivyokua kama taifa changa wengi walisoma hapo, mawaziri, viongozi wengi wa kiserekali na wataalamu mbali mbali hii ni sababu tosha ya hiki chuo kupata sifa lukuki na ni sawa kabisa sababu majority wamepitia hapo.

kuanzia miaka ya 1990 hadi sasa kuzaliwa vyuo kibao vya serikali na vya binafsi, hivi vyuo vimepunguza ule utegemezi wa UDSM na sasa hivo vyuo vinatoa taaluma kibao na katika ngazi tofauti tuanzie certificate, diploma, degree, master hadi phd.
sasa hivin hakuna ule utegemezi na hivi vyuo ni imara mfano bugando, kcmc, st joseph ya engineering iliyopo Dar es salaam na vingine kibao vinavyoongozwa na mashirika ya kidini kama Ruco, makumira, theofilo kisanji, tumain sasa university of iringa, saut yani ni vingi mno, pia vipo udom, josia kibra, imtu, kampala archbishop james, mihayo, hubert kairuki, university of arusha, mzumbe, chuo cha ushirika moshi, pia zipo taasisi kama ditn nit n.k halafu kule zanzibaree sijaongelea bado.
na sasa ushindani upo waajiri wanabase sana kwa baadhi ya vyuo kupata wataalamu sababu wanajua viko poa.
nimejaribu kutafuta sababu ya udsm kupewa sana sifa sijaona sababu ila ubaguzi wao ndo unao waweka hapo wa kuchagua division one na two ila kiuhalisi kuna vyuo vinafanya vizuri mno na vinatoa wataamalu wazur utakuta watu wanaiponda udom wakat tukija kwenye hali halisi ndo inatoa IT expert wazuri na wameunda baadhi ya mitandao ya kijamii tunaiona.
pia kama nyie sio mna matatizo waliosoma hiyo udsm ndio malecture katika vyuo mbalimbali hapa nchini halaf vyuo vya kidini na hivi vya kibinafi vina wageni weni wengi wenye elimu nzuri wanatoa elimu kwa wanafunzi. wana partnership nzuri mno na sapoti ya kifedha.

my take udsm ni miaka hiyo sio sasa saivi vyuo vipo vingi na vinatoa elimu nzuri mifumo ya kisasa ya kufundishia masomo kwa vitendo na theoretically.
udsm saivi ni magofu chuo na mifumo mizima haijafanyiwa ukarabati wanafunzi wanatumia oudated machines halaf mnaanza kubwabwaja hapa na hao wanafunzi wenu tukikutana nao kazini hata kwenye mafunzo kwa njia ya vitendo mbona hawaja jipya iweje tuwe level moja kama kweli wao ni bora?
watu wenye uelewa wao hapa watasema kweli na wanayoyaona kwa hao graduate wa udsm wanajitapa sana. waache ubaguzi kuna dogo alikua anaomba chuo mwaka juzi alikua ana divisio three alikua anaomba kozi moja inahusiana na mambo ya fishing chakushangaa zilikua zimebaki nafasi kama 5 lakin hadi mwisho dogo hakupata, kitendo hiki kiliniuma sana na nikasema ngoja nainze kufatilia kwa umakini kuna nini huku hadin naadika huu uzi hamna lolote maringo tuu, nataka uongozi mzima utoe nafasi kwa wote kusoma na sio kubagua.
historia inawabeba tuu na ni kweli hakuna ubishi ni chuo kikongwe kwenye taifa la tanzania lazima historia iheshimiwe, ila sababu ya jina isiwe sababu ya kuwa overcredited wakati kila university private na government nyingine zinafanya vizuri mno baadhi ya nyanja wenyewe mashahidi.

UDSM will always be UDSM
 
Back
Top Bottom