Chuo Kikuu Huria katika kashfa ya bilion 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu Huria katika kashfa ya bilion 2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lutayega, Jul 9, 2012.

 1. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  TAARIFA KWA UMMA

  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) kinakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Kiswahili la kila Jumatano, Mwanahalisi, ambazo zinadai kupitia toleo lake namba 301 la Julai 4- 10, 2012 kwamba kuna ufisadi mkubwa unaodaiwa kufikia Shilingi Bilioni Mbili.

  Katika taarifa hiyo isiyokuwa na chembe ya ukweli gazeti hilo linadai fedha hizo ziliibwa kati ya mwaka 2008 na 2012. Kumekuwa na mlolongo wa taarifa za uzushi
  na uongo kwenye baadhi ya magazeti, likiwemo Mwanahalisi, zenye nia ya kukichafua Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) na viongozi wake wa ngazi za
  juu. Taarifa hizo, kwa kiasi kikubwa, zimekuwa zikishabikia watu wanaoshukiwa kuhusika na upotevu wa rasilimali za Chuo, ikiwemo fedha.

  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) hutumia njia mbalimbali zilizoainishwa katika Hati Idhini ya Chuo ya 2007 na kadiri ya sheria husika za nchi kuhusu kutoa taarifa rasmi za mahesabu yake ambayo kila mwaka hukaguliwa na CAG na taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya chuo ya mwaka 2010/11 imeishatolewa na Chuo kimepata hati safi. Taarifa hizo zitapelekwa Bungeni hivi karibuni na hakuna sababu ya mtu mwingine au gazeti kama Mwanahalisi kutengeneza mahesabu ya Chuo nje ya utaratibu huo rasmi ambao ndio unatumika na Baraza la Chuo kusimamia matumizi ya fedha na raslimali zote za Chuo kama msingi wa utawala bora.

  Mtindo huu wa gazeti la Mwanahalisi kutengeneza mahesabu yake ya Chuo ni uvunjaji wa sheria za
  nchi nani Kinyume kabisa na matarajio ya uandishi adilifu na una nia ya kuupotosha umma na kushirikiana na mafisadi. Ni matumaini ya chuo kwamba vyombo husika vitachukua hatua mbalimbali kulizuia gazeti hili kuendeleza kuandika uzushi.

  Chuo Kikuu Huria Tanzania kinasema kuwa mlolongo wa taarifa zinazochapishwa katika magazeti haya ni za uongo, uzushi na zenye lengo la kuchafua jina zuri la
  chuo chetu chenye kutoa elimu nafuu na bora ya masafa kwa jamii.

  Ni ushauri wetu kwa uongozi wa magazeti husika kuwa endapo watahitaji taarifa sahihi kuhusu uendeshaji wa chuo ni bora kuwasiliana na wasemaji wa chuo katika
  njia muafaka.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano na Masoko,
  CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
  Kwa Mawasiliano Zaidi;
  Albert Z. Memba, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania S.L.P 23409, Dar es Salaam, Tanzania.
  Tel. + 255 22 2668445; Fax. + 255 22 2668779;
  E‐Mail: dcm@out.ac.tz
   
 2. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mi mwenyewe nakubaliana na makala ya mwanahalisi kuwa kuna wizi ambao unafanywa na viongozi wa chuo kikuu huria kwa sababu michango inayotolewa na wanachuo haiwasaidii kupata mahitaji ya kimasomo km lecture notice, ila usipokamilisha michango hauruhusiwi kuingia kwenye mitihani, je michango wanayotoa inatumikaje km hakuna uhujumu unaofanyika.
  Mwanahalisi wapo sahihi na ukweli mzima mda si mrefu utakuwa wazi
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa mwandishi wa mwanahalisi haku balance story.
  Naamini Albert Z. Memba mkurugenzi wa habari wa chuo yupo sahihi.
   
 4. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukuta wa uzio wa chuo hicho ulijengwa kwa ufisadi, na kampuni iliyojenga ni ya kigogo wa chuo hicho tuanzie pale.
   
 5. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Another silly story. Nia ni kutuhamisha kutoka kwenye burning issues na kutuletea issues za kitoto ili tusi-concentrate kuulizia mipango ya serikali iliyofichuliwa ya kutaka kuwaua Dr. Slaa na Mnyika.
   
Loading...