Chuo cha urubani Tabata?

Chuo cha urubani Tabata?

Jamani mdau ametoa kama tahadhari tu! ni kweli haiwezekani useme unatoa kozi ya udaktari wakati hata hospitali (ambayo ni ya lazima) huna!!! yaani unatoa kozi ya urubani hata ndege huna, au wanafundishwa kwa picha za ukutani?

kweli "you can't be seruous"

labda anawafundisha kwa microsoft flight simulator.. lolz!!! then may be uko tabata anatoa theory course then when time reaches, atawapeleka wanafunzi airport na kukodi ndege ya mafundishio Cessna 152/172... lakini elimu ya urubani jamani sio kitu masihara uanzishe tu, private license tu ni almost 15000USD sasa ukazitoe katika chuo ata hakina hadhi ni kupoteza investment
 
Mkuu taratibu hii thread inaweza kuonekana kama umbea lakini kumbuka, kozi za fani muhimu kama urubani haziwezi kufundishwa kama jamaa alivyoeleza. Yaani kachuo kako kwenye kighorofa fulani hapo Tabata. Kimsingi hawa jamaa wanashusha hadhi ya elimu na utaalamu kabisa.

kweli kabisa, huwezi kufundisha ruban kama yule wa hotel management. hapo ni utapeli mtupu.
 
chuo cha urubani kiwe tabata u cant be seriaz khaaa

Wewe na huyo dumuzi madumuzi kweli! Mitanzania bwana tumezoea kuibiwa likisikia chuo kiko nairobi misikio yote inasimama
Eti chuo cha urubani kiwe tbt so what?
 
This is too much. ukiona na ujinga wote huu hachukuliwi hatua ujue CCm na wakuu wake wako nyuma yake
 
Wewe na huyo dumuzi madumuzi kweli! Mitanzania bwana tumezoea kuibiwa likisikia chuo kiko nairobi misikio yote inasimama
Eti chuo cha urubani kiwe tbt so what?

Kwa hiyo chuo kikiwa tz hata kama ni cha utapeli tusiseme? Mbona vingine vlivyopo bapa nchini hatuvisemi. Kuona ubovu na kukaa kimya hakujengi nchi.
 
Kuna jamaa amekuwa akinadi chuo chake, kwenye stesheni mbili za radio zinazomilikiwa na mashirika ya kidini kuwa kinafundisha kozi ya urubani na kozi nyingine za anga. Wadau chuo hicho hakifundishi kabisa kozi za urubani Pia yeye hujinadi kuwa ni rubani nayo sio kweli. Hukiita chuo university wakati hakina sifa wala hakitambuliki kama chuo kikuu. Ada za kozi zake ni za ulanguzi e.g. Airport ground handling ths 2.5million, Flight operatons and airline management 5 million, sare ambazo ni lazima laki 4. Kwa vyuo vlivyopo airport eg cha serekali CATC na cha Regional Aviation, ada kwa kozi hizo ni Kati ya laki 8 na 1 million. Huwarubuni wazazi kuwa vijana wakihitimu kozi ya flight operatons wakiajiriwa kwenye mashirika ya ndege watakuwa wakiruka kusaidiana na marubani, jambo ambalo sio kweli. Walimu wenye sifa za kufundisha kozi hizo hana. Walio kuwepo kwa muda mfupi waliondoka, na aliyekuwa principal aliacha kutakana na utapeli uliopo. Pamoja na ukurugenzi hujiita chief instructor, wakati hata leseni ya flight operatons officers hana. Huyo jamaa hulazimisha ngono kwa baadhi ya mwanafunzi wa kike. Aliisha fukuza wanafunzi wakiume kwa kuhisi wanamahusiano wanafunzi wa kike anowanyemelea. Mmoja wa mwanafunzi hao alipeleka malalamiko TCAA. Alimtimua mwanafunzi wa kike aliyekuwa hataki kuendelea kukaa kwenye hostel ya chuo, ambayo ni nyumba ya kupanga, kwa usumbufu wa huyo jamaa kumtaka ki ngono. Wadau chuo kipo Tabata magengeni kwenye jengo la crdb.

Ungeanza kuripoti polisi nadhani ingekuwa bora zaidi. Kuliko kuja kutangaza humu ilhali hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa kutokana na tuhuma hizo...
 
Jamani ee hebu taratbu kwanza, kuna kitu wachangia hoja hawajakijua mpaka sasa. Ngoja niwafahamishe, ni kwamba bwana charanga ameiona fursa na sasa anaichangamkia.
 
labda anawafundisha kwa microsoft flight simulator.. lolz!!! then may be uko tabata anatoa theory course then when time reaches, atawapeleka wanafunzi airport na kukodi ndege ya mafundishio Cessna 152/172... lakini elimu ya urubani jamani sio kitu masihara uanzishe tu, private license tu ni almost 15000USD sasa ukazitoe katika chuo ata hakina hadhi ni kupoteza investment

Mkuu kwenye mafunzo ya urubani hiyo simulator uliyo itaja haitambuliki kabisa, simulator zinazo ruhusiwa zimetengenezwa mfano wa cockpit ya ndege ukiingia ndani unakuwa kama uko ndani ya ndege. Bei ya kuzinunua huwa kubwa kuliko bei ya ndege. Kuna chuo kimoja cha private pale airport Dar wanayo. Simulator ulioitaja ni kwa ajili ya burudani tu ni pc game, japo inaweza kusaidia mtu kupata some idea in flying. Kwa kawaida mwanafunzi ili kufanya mtihani wa leseni ya private license lazima awe na masaa 40 ya kiruka. 8 mpaka 10 huwa kwenye simulator. Na hiyo smulator hata ukiinunua huwezi kuitumia chuoni mpaka iidhinishwe na TCAA.
 
Kwa hiyo chuo kikiwa tz hata kama ni cha utapeli tusiseme? Mbona vingine vlivyopo bapa nchini hatuvisemi. Kuona ubovu na kukaa kimya hakujengi nchi.

Tatizo lako wewe na Charanga hujatuambia! Na huu tunauita umbea!Hakuna hata mwanafunzi 1 wala mzazi aliye lalamka mpaka sasa! Unaleta thread hapa eti unahoji chuo cha urubani kiko tabata! Ndege wanafundishwa ubaoni! sijui ada milioni 8 Ujinga mtupu!!! Mashule ya Private yapo kibao Hamjasema watu wanalipa mamilioni ya pesa kupeleka watoto wao chekechea unashangaa mil 2.5 ya Ground handling!
Kama unaona anafaidi kafungue cha kwako
 
What i know mtu yeyote au taasisi inayoendesha au kutaka kuendesha mafunzo yoyote yanayohusu aviation industry hapa Nchini NI LAZIMA wawe certified na TCAA ambaye ndiye agent wa ICAO hapa Tanzania, na hakuna watu strict kwa viwango kama Icao. Hakuna kitu cha kutunga huko, kila la kufanya liko outlined kwenye Annexes.

Sasa kama jamaa huyo alianza zamani(mmesema alianzia huko Banana) inaonyesha kuwa alikuwa certified tayari.
Ila nimeshangaa mmoja amesema kuwa wanajeshi walikuwa wanafundisha hapo chuoni, labda kama walikuwa wanafundisha somo la urubani parse, maana Civil Aviation na Military Aviation ni mbalimbali kabisa.
Chuo kuwa Tabata siyo hoja jamani, cha msingi ni kama ana vifaa vyote vya msingi vya flight simulation, na inapofikia muda wa field ni ishu ya kwenda uwanjani JNIA na kufanya mazoezi.
Ijapokuwa chuo kinapokuwa palepale kiwanjani advantage ni kubwa zaidi, maana wanafunzi wanaanza kuyasikia ma'reversal thrust toka kwenye ndege zinazotua wakiwa darasani, hivyo inawawia rahisi field.
 
Ungeanza kuripoti polisi nadhani ingekuwa bora zaidi. Kuliko kuja kutangaza humu ilhali hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa kutokana na tuhuma hizo...

Mkuu this was my observation ili wazazi wafunguke na wenye kazi zao wafuatilie. Nadhani sijakosea.
 
Mkuu this was my observation ili wazazi wafunguke na wenye kazi zao wafuatilie. Nadhani sijakosea.
Mkuu hujakosea.
Masomo ya aviation ni ghali hivyo ni muhimu sana mzazi akapata Value for Money anayoinvest kwa mwanae, vinginevyo hela hiyo ni bora akaifungulia hardware kule Kinyantila.
 
Wanatumia flight simulator apps za Ipad kufundishia
 
Duhhhhh utakuwaje CFI na huna instructors rating. ?
Tuna Mengi ya kujifunza .
 
Mimi binafsi nilishawahi fika pale TAUC (Tanzania Aviation University College),Tabata- Magengeni. ''Honestly'', ni ''college'' ambayo bado ipo kwenye matengenezo. Kwa taarifa tu, awali hawa jamaa walikuwa Banana karibu na Airport kabla ya kufukuzwa huko!Nilikwenda pale kwa lengo la udadisi na kutaka kupata ukweli kwani nilivutiwa na maelezo ya huyu mhe. Chara*** ,Mazingira yake: kulikuwa na mlundikano wa makaratasi kwenye mapokezi, fotokopi mashine hapohapo,eneo la mapokezi ni dogo lkn pia kulikuwa na wanafunzi darasani pembeni na hako kasehemu ka mapokezi. Kwa kweli nilipokelewa vizuri, nilikutana na kijana mmoja ambaye alisema kuwa amemaliza UDSM lkn ni mkufunzi pale. Alinieleza mambo mengi kuhusiana na field hiyo ya Aviation, si haba nilijifunza kitu.Lakini cha kushangaza siku hiyo hiyo nilipewa form ya Admission(udahili) kitu ambacho kilinipa mashaka. Aliyenipokea alinieleza kuwa kuna watoto wa mawaziri wanasoma pale lkn sio rahisi kuwatambua na kuna wakufunzi toka jeshini huja pale kufundisha.

Kwa msingi huo, nilikwenda Airport kuna chuo cha serikali i.e CATC ( civil Aviation Training college) Nilipata maelezo ya kutosha. Bahati nzuri nilikutana na mkufunzi ambaye tulizungumza naye ofisi kwake tukabadilishana mawazo maana tuliweza kuelewana kutokana na level zetu za elimu, aliniambia siku hizi huchukua watu wa degree kwa mafunzo ya urubani tofauti na zamani ambapo walikuwa wanachukua F6 leaver. sababu ni kuwa wanaopanda ndege ni watu wenye Elimu tofauti (prof,Dr, n.k)so ni vema awepo mtu mwenye elimu walau ya chuo kidogo ili mazungumzo yawe mepesi, maana F6 akisikia Profesa anaanza kufikiria ni mtu wa ajabu sana kumbe ni binadamu kama wengine tu.
Mwisho alisema ..'' watanzania wengi hawapendi kutafuta taarifa sahihi mahali sahihi'' akaongeza wapo waliokuja wakasema kuna chuo cha anga huko tabata.. kwa nini wasiende mamlaka ya Anga TZ kuuliza!

Ushauri: kama unataka kusoma fani yoyote ya Anga, zipo nyingi sana ...nenda Mamlaka ya Anga TZ. utaishia kuliwa na wajanja hela zako. Jana huyoo mhe. aliulizwa chuo hicho ni cha serikali au private? akaanza kuuma maneno!

Mwisho: Mkurugenzi wa hicho chuo amesoma HGL, hana degree yoyote(NB: sisemi kwamba kutokuwa nayo kunakunyima nafsi ya ukurugenzi )!

c.c dumuzi, LIKUD,m 23,mopaozi,Katufu, Earth on heaven,stata mzuka ,LORDVILLE
kwa leo naishia hapa....

umeongea vizurisana zamani nilikuwa na wazo la kuwa rubani na his kama umenikumbusha kitu?vp wanachukua degree ya aina gani kuwa rubani.
 
Ungeanza kuripoti polisi nadhani ingekuwa bora zaidi. Kuliko kuja kutangaza humu ilhali hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa kutokana na tuhuma hizo...

Kutoa taarifa hapa JF ni namna mojawapo pia ya kufikisha ujumbe kwa wahusika kwani naamini baadhi ya informers wao ni members wa JF. Kumbuka hata swala la Lwakatare inasemekana source yake ilikuwa JF.
 
Back
Top Bottom