Chuo cha IPS Chanika sasa kutoa shahada ya ugavi


Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Exuper Kachenje


CHUO cha Ununuzi na Ugavi (IPS) cha jijini Dar es Salaam, kipo mbioni kutoa shahada katika fani hiyo.

Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dk Didas Masaburi, alipokuwa akimkaribisha Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha, katika mahafali ya tatu ya IPS, kilichoko Chanika Dar es Salaam.

"Tupo katika mchakato kuanza kutoa digrii ya ugavi katika mwaka huu wa masomo.Tunakuomba uishauri SMZ iendelee kutuamini, ituletee wanafunzi mwezi wa tisa tukianza," alisema Dk Masaburi.

Dk Masaburi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki alizishauri SMZ na Serikali ya Muungano kuwa makini wakati zikiingia katika utekelezaji wa soko la pamoja la Afrika ya Mashariki, ili Tanzania isigeuke kuwa soko la bidhaa feki na hasa katika elimu.

Akizungumza katika mahafali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Yusuf Omar Mzee, aliyemwakilisha Waziri kiongozi, alisema serikali itachukua tahadhari ili kuhakikisha Tanzania haigeuki na kuwa soko la bidhaa feki.

Alisema taaluma ya ununuzi na ugavi ni nyeti na kwamba inachukua asilimia 50 ya bajeti.

Hata hivyo soko la taaluma hiyo limeingia katika matatizo kutokana na tamaa miongoni mwa wanataaluma wake.

Pia alisema sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inayotumika sasa ina mapungufu na kwamba mchakato unafanyika kuwezesha irekebishwe katika kikao kijacho cha Bunge.

Aliwatahadharisha wahitimu na wataalam wengine wa fani hiyo kuwa makini na kudhibiti nafsi zao ili waepuke kuangukia katika tamaa na kuharibu kazi
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,370
Likes
1,619
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,370 1,619 280
Hiki chuo kitakuwa na wahitimi dhaifu kwasababu viongozi wao akiwemo huyo Masaburi wana shahada za kuchonga!! Watatoka wanafunzi na vyeti lakini hawatakuwa na elimu thabiti ya ugavi kwahiyo kama serikali itawaajili wahitimu hao mjue udhaifu katika manunuzi na tenda serikalini havitapata tija!!
 

Forum statistics

Threads 1,251,007
Members 481,556
Posts 29,753,990