Chuo cha A3 Institute mnaanzaje kumtoa mwanafunzi kwenye Mtihani?

Ngambako

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
315
263
Wadau,

Nimepokea simu asubuhi kutoka kwa kijana wangu, mtoto wa dada yangu ambae napigania apate elimu ili ajitegemee kwa maisha yake ya hapo baadae.

Kinachonisikitisha ni kuwa bwana mdogo katolewa kwenye mitihani ambayo wameanza toka jana eti tuu kwa sababu hajakamilisha ada, na ada yenyewe imebakia sh laki moja tu kwa muhula wa kwanza, na cha ajabu kijana jana amefanya mtihani na wakati wanamtoa leo wamemwambia na mitihani alofanya jana wanamfutia.

Naombeni ushauri nifanye nini kwenye hili? je ni haki kumtoa kijana kwenye mtihani wakati inaendelea?
 
Duh! Shule za binafsi & Vyuo vyao wana ka tabia hako. Wanakusubiria siku ya paper wanakuzuia. Poleni sana!

Nilisoma chuo cha Serikali, na pale mtu alikuwa anadaiwa ada au chochote; Ataruhusiwa kufanya mtihani ILA matokeo yatashikiliwa mpaka alipe (Withheld).

Nadhani na wale wa binafsi wafanye hivyo. Mtoto afanye mtihani lakini washikilie matokeo mpaka mzazi/mlezi awe amelipa. Hii ndio njia fair kabisa kwa pande zote.

Kumnyima mtu kufanya mtihani wakati amesoma muhula au semister nzima sio haki.
 
Mbona ni kawaida vyuo ving tu uwez kufanya mtian bila kulipa ada we nenda kalipe ada aje afanye mitian ya special
 
Nakushauri ukalipe ada ili kijana wako amalize masomo yake,vinginevyo hapa utapoteza muda tu
 
Ksribu vyuo vyte.. hio ndio sheria yke... chuo sio kama secondary... mm naona hawajamuonea ila ndo sheria
 
Weka namba yako ya mtandao hapa tukuchangie buku buku tukichangia hii thread wakati kijana anakosa mtihani haina maana tuko wengi humu laki moja fasta kijana arudi kwenye pepa
 
Back
Top Bottom