Chungu Na Tamu Ya Kusom Vitabu

Quinine Mwitu

JF-Expert Member
Oct 19, 2014
5,528
6,085
Habari Wananzengo(wananchi)
Niende kwenye Mtizamo Moja kwa moja,Wakuu nimekua kidogo na ka ulevi ka kusoma Vitabu mbalimbali hasa baada ya kubaini kuwa elimu ipo popote na siku zote unatakiwa kuelimika. Ila wakuu usomaji wa vitabu una faida zake kubwa sana,Mwalimu,kiongozi au Mtu yoyote yule mwenye maarifa mengi ndio anayetawala fikra za wengi wasio na elimu,kama wanavyosema kuwa ukitaka kuwahadaa watu kuwa na maarifa zaidi yao.
Ukija kwenye upande Mwingine vitabu vinataka uwe mvumilivu sana,maana kuna ukweli unaouma sana na ili uwe na maarifa mengi inakubidi usome hadi vitabu vinavyopingana au vinavyokukosoa wewe labda jinsia,dini,mila nk,Mfano jinsi gani viongozi walio wengi wa kiafrika wanavyochota mapesa WB na kuliingiza deni kwenye deni la Taifa,deni linalokuja kulipwa na walalahoi wanao kula mlo mmoja kupitia kodi,Matajiri wengi si walipaji wa kodi kama anavyothibitisha George Bush,kuwa hakuna haja ya kuwalipisha matajiri kodi kwani wanambinu nyingi za kukwepa kodi, Au unasoma kitabu kinachoeleza Jinsi gani ''Mababa wa Ulimwengu'' wanavyotuhadaa kila uchwao kupitia ujinga tulio nao watu wengi.Au jinsi mauwaji yanavyofanywa duniani na kupoteza maisha ya mamilioni ya watu kwa ajili ya kukidhi matakwa ya kikundi kidogo sana cha watu lakini sisi tusio na maarifa na uwezo wa kung'amua kinachoendelea huwa hatuwezi kulipinga jambo husika
Wakuu nilichokuja kugundua mimi 60% ya vitu tunavyovisikia,kusoma mashuleni,nk Haviko kama vinavyoonekana,ni propaganda na hadaa tuu '' wajanja'' wanatuchagulia kipi tukijue na kipi tusikijue,Siri na maarifa mengi ya Ulimwengu huu upo kwenye vitabu japo ukweli ungine unauma ila jikaze ili ujue mengi,
95% ya walimwengu hawana maarifa,wanategemea 5% ya watu ndio wafikiri kwa ajili yao,ingawa pia hawajui jee hawa 5% ni salama kwa wao(wasiokuwa na maarifa) kuwa wategemewa katika maarifa yao?
 
thread nzuri sana.. mkuu Quinine Mwitu.. Karibu kuweka Paragraph mkuu. Wengine wakiona ivo tuu hata kusoma hawata taka tena, Halafu nitarudi tena
Nilitaka niiweke iwe kimahaba zaidi ili ivutie watu wengi lakini nikasema wacha niiweke open only bright people watausoma
 
Back
Top Bottom