Chumba cha maajabu kilichopo juu ya dunia

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,126
2,000
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali Duniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo hivyo kumuwezesha mtalii kuona kama vile yupo juu ya Dunia.

Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani umbali wa mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji (NADHANI WATAKUULIZA BARUA KUONESHA UMEAGA KWENU).

 

gbefa

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
3,500
2,000
Mkuu nilidhani kinaelea kumbe kimeshikizwa kwa mlima sio mbaya na sisi tunaweza kufanya hivyo easy tu kwa selikali hii
 

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,996
2,000
Bado Hakina Utaalamu wa aina yake .. Nadhani Wangebuni kwa Kuweka Fito ndefu zaid Chumba Kisogee Katikati kabisa Kule..Hapo ndipo kingeleta Mantinki.
 

Willy Johnson

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
318
250
Mi wazungu hapa ndio wananiacha hoi hivi ukiwa juu angani ndio upo juu ya dunia na ukiwa aridhini ndio upo chini ya dunia na dunia ina umbo kama yai.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom