Chukua Tahadhari Corona bado Ipo

Chukua Tahadhari Corona bado Ipo

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
341
Reaction score
303
Mtindo wa maisha wa watanzania tulio wengi ni kana kwamba Corona haipo tena duniani. Tunaishi kipekee na tofauti na mataifa mengine ulimwenguni wakati huu wa janga la Corona.

Utofauti huu unatokana na watanzania kuyaamini, kuyaweka moyoni, na kuyaishi maneno ya Rais wetu mpendwa Magufuli aliyetangaza mwaka jana mwenzi Juni kwamba Tanzania tumeishinda Corona kwa njia ya maombi pamoja na kujifukiza.

Kauli ya Rais ilitoa hofu mioyoni mwa wengi na kupelekea watanzania kuishi bila masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Kwa sasa watanzania walio wengi hawakumbuki tena bei ya barakoa na wanaovaa ni 1/10 kwa utafiti wangu usio rasmi.

Shughuli na matukio yetu ya kijamii yanaendelea kama kawaida na wiki hii Haji Manara anapigia debe kwa nguvu zote mashabiki wa Simba waende kuujaza uwanja wa taifa kwenye mashindano ya Simba Super Cup.

Siku ya jana Jumanne tarehe 26/01/2021, nilipata bahati ya kusoma barua ya Rais wa TEC na Askofu Mkuu wa mbeya, Askofu Gervas John Nyaisonga kwenye mitandao ya kijamii akiwataka maaskofu pamoja na waumini wote wa dhehebu la Katoliki kuchukua tahadhari juu maambukizi mapya ya virusi vya Corona(COVID-19).

Nikinukuu baadhi ya maneno ya barua hiyo yanasema hivi:
“Nchi yetu sio kisiwa. Hatuna budi kuzingatia hekima ya wahenga kuwa ‘mwenzio akinyolewa wewe tia maji’. Hatuna budi kujihami, kuchukua tahadhari, na kumlilia Mungu kwa nguvu zaidi ili janga hili lisitukumbe.”

Barua hii imekuja wakati muafaka kwani dunia kwa sasa ipo katika taharuki kubwa ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona vya aina ya Aina ya Afrika Kusini pamoja na Uingereza ambavyo pia vinajulikana kama(B117).

Japo barua hii haijaweka wazi uwepo wa Corona nchini lakini imetoa mwanga na tahadhari kubwa kwa watanzania.

Serikali yetu inaendelea kusimama na msimamo wake kwamba Corana haipo nchini na hata leo tarehe 27/01/2021 Rais JPM akizungumza katika uzinduzi wa shamba la miti huko Chato alisikika akisema;

“…sisi Tanzania hali ya Corona haijawa kubwa na haipo, iko chache sana, wakati wenzetu wapo kwenye lockdown tuutumie muda huu kulima..”. Rais pia aliendelea kuwasihi wananchi kuendelea kuomba pamoja na kujifukiza.

Ndugu zangu wahenga walisema “mwenye macho haambiwi tazama”. Kumbuka uhai wako ni muhimu kuliko kitu chochote kile na unalojukumu la kuulinda afya yako kwa nguvu zako zote

Wote tunaona jinsi mataifa ya wenzetu yanavyoteseka na janga hili la Corona. Hiyo ni ishara tosha kwamba inatubidi tuendelee kuchukua tahadhari ya kulinda afya zetu na maambukizi ya virusi vya Corona.

Padre Charles Kitima alipokuwa akihojiwa na BBC News Swahili kutolea ufafanuzi barau ile ya Maaskofu alisikika akisema;

“…..kwa mfano vifo parukia flani, parukia za miji mikubwa nishazoea labda kuna misa ya mazishi moja kwa wiki lakini saivi unakuta kila siku, utakuta msikitini kuna msiba, kuna mazishi kuna mazishi.
Tunaona hii siyo kitu cha kawaida na wakati tunasubiria wanasayansi na wizara yenye mamlaka watuambie, lakini sisi tunaendelea kukusanya watu kila wiki na kila siku lazima tutoe tahadhari kwa watu.”

Wiki iliyopita serikali ya Uingereza ilipipa marufuku wa wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia Uingereza. Tukumbuke hili sio tukio la kwanza kwani siku kadhaa zilizopita wasafiri wawili kutoka nchini Tanzania walipoingia nchini Denmark walikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Ndugu yangu hata kama huamini kama Corona ipo ni vyema kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
Inatupasa kwa sasa tukumbuke kuvaa barakoa, kunawa mikono kila wakati pamoja na kujizuia na mikusanyiko ya watu wengi isiyokuwa na ulazima.
 
parukia ndiyo nini?

Corona mbona kawaida tu, kama mafua mengine: nyie mnaopenda maisha ya kizungu shauri zenu! "sisi tunajifukizia, tunakunya mchaichai, limau na tangawizi, kashwagala kwa sana, tunakunya maji ya moto kwa sana n.k, maisha yanaendelea.

Na Nukuu:

"Tutaendelea kuchukua tahadhari za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukiza huku unamuomba Mungu unaswali, unasali huku unapiga zoezi la kulima ili ule vizuri ushibe, Corona ashindwe kuingia mwilini”- Rais wa Tanzania, John Magufuli
 
Sio kwamba bado ipo, yani ndiyo kwanza imeanza upyaaaa.
Hatari sana na tatizo viongozi wetu hawapo tayari kusema ukweli kwa wananchi wote. Juzi tumeona waziri wa fedha akiwaambia wafanyakazi wa wizara yake wachukue tahadhari ya kujikinga na Corona kama kwamba wao ndio watanzania sisi wengine hatuna haki ya kuishi nchi hii.
 
Hivi nawezaje kuzuia huu usenge wa Jumbe za Corona kwenye simu yangu jamaniiii..#Tusitishane corona sio issue
 
Nikikumbuka hali tuliyofikia mwaka jana miezi ile April hadi June, sitaki kabisa kusikia tahadhari... maisha yalijawa hofu mno.
 
Nikikumbuka hali tuliyofikia mwaka jana miezi ile April hadi June, sitaki kabisa kusikia tahadhari... maisha yalijawa hofu mno.
Nadhani ni vyema kutazama yanayotokea kwa wenzetu na kujifunza. Sio lazima kufuata kila kitu wanachofanya wao lakini ni vyema sana kuzingatia kanuni za WHO.
 
Magufuli ameinanga chanjo ya Corona na kusema Wazungu hawana nia nzuri na bara la Afrika. Jana WHO imesema inataka serikali ijiandae kupokea chanjo ya Corona.

Vipi wewe utakubali kupata chanjo ya Corona itakapofika nchini?
 
Back
Top Bottom