Nina chuki sana na wewe..Hunijui Sikujui achana na mimi....:eyebrows:Nadhani itakua wiki moja imepita sasa tangu niulize kwenye thread fulani kama inawezekana mtu akapata adui hapa JF kwasababu binafsi bado sijaona uwezekano wa kumchukia mtu ambae sijui yukoje in reality na wala hajanifanyia lolote baya hapa mtandaoni.
Naelewa kwamba huku mitaani hua inatokea mtu , hata ndugu yako au rafiki akawa anakuchukia bila sababu maalum.Yani unakuwa hujamfanyia lolote baya, tena inawezekana ukawa mtu wa kumsupport na kumsaidia sana.Chuki ya namna hii naamini mara nyingi hua inasababishwa na wivu,yani yule mwenye chuki anatamani alichonacho mwenzake kingekua chake (pesa,mpenzi mzuri, familia inayompenda, marafiki wanaomjali, kazi nzuri n.k). Na mara nyingi hali hii hua inapelekea hao wenye wivu kutafuta namna ya kumvurugia huyo mwingine hata kwa kusambaza maneno yasiyo na ukweli.Ila sasa naomba kuuliza, sehemu kama hapa JF, sehenu ambayo wengi hatufahamiani inakuaje mtu anakua na chuki tena kali na mwenzake? Tatizo ni nini? LIKE anazopokea? Thread anazoandika? Watu anaointeract nao jamvini? Muda anaospend online? Namna anayoandika? Mambo anayoonekana kujua? Kama jibu ni moja ya hayo hapo juu nini kinakusumbua wakati hatujuani hivyo na wewe unaweza ukatumia hata google kuandika kitu kizuri kikakubalika bila yeyote kujua hazikua juhudi zako mwenyewe?
Nimeona niandike hii mada baada ya ile incident ya Ashadii, taarifa zinazonihusu mwenyewe na wengine ambao hata hawafahamu kwamba wana maadui wasiowahitaji humu.
Wewe kama ni mmoja wa hawa watu wenye chuki na watu usiowafahamu embu chunguza tatizo lako lilipo. Na kama tatizo liko kwao (inawezekana kuna namna wamekuboa) wasiliana nao uwajulishe badala ya kuwachekea kinafiki huku roho yako ikilika taratibu kwa chuki na kujiabisha kwa kujipeleka kwa marafiki zao (watu wanaofahamu kiukweli) na kujifanya wewe unawajua wakati huwajui.
Wote tumekuja hapa kwa mapenzi binafsi, sio kufurahisha watu wengine bali kujifurahisha wenyewe.Ukiona unakosa hiyo furaha uliyofuata pumzika badala ya kuwatolea hasira watu wasiohusika na hasira yako. Usimchukie mtu usiye mfahamu, kwa sababu zisizo na kichwa wala vidole maana huwezi jua mtajakutana katika mazingira gani. Hii ni sehemu ya kupunguza stress na sio kuongeza, usijinyanyase kwa kutoitumia vizuri.
Jumanne njema.
Nina chuki sana na wewe..Hunijui Sikujui achana na mimi....:eyebrows:
Mimi huwa najiuliza mtu ana chuki na wewe hakujui wala humjui, je ikitokea bahati mbaya/nzuri akakutana na wewe atajifanya anakuchekea kinafiki, mara nyingi watu wa namna hii wanakuwa na low self esteem na kutokujiamini wao kama wao, imagine hapa JF mtu anatoka povu kweli anakusemea mbovu kweli but in real sense hakujui wala hajawahi kukuona but anajaribu ku-assume kuwa anakujua sanaaa...ohooo mara fulani hivi mara vile anavyoongea utafikiri labda ni mama yako aliyekuzaa... snitches get stitches

Hahahaha!! Sasa sisi wengine kama bandwidth zetu za kungaunga mara modem ya Tigo inachukua muda mrefu ku-load kwanini tusi-mind au wewe mwenzetu unachimba bandwidthSuck it up maana Nakujua, Unanijua , siachani na wewe.
Inashangaza kwakweli. Watu wa huku mtaani naweza jaribu kuwaelewa ila huku mtandaoni ambapo kila mtu anaingia kutokana na uwezo wa bandwith yake,sielewi kabisa.
Suck it up maana Nakujua, Unanijua , siachani na wewe.
Inashangaza kwakweli. Watu wa huku mtaani naweza jaribu kuwaelewa ila huku mtandaoni ambapo kila mtu anaingia kutokana na uwezo wa bandwith yake,sielewi kabisa.
:lol:Fidel bana sasa kama hauwezi kusoma umejuaje kama ndefuNaomba unifupishie nimeshindwa kusoma ndefu mno nipo kwenye tuktuk.
Hahahaha!! Sasa sisi wengine kama bandwidth zetu za kungaunga mara modem ya Tigo inachukua muda mrefu ku-load kwanini tusi-mind au wewe mwenzetu unachimba bandwidth
Hatuachani na wewe wala nini, mpaka uache kutumia slogan yetu.
Wenye chuki ni wanafiki na wasiowawazi. Mimi nikichukizwa na jambo lolote nakupa laivu kitu ambacho watu wengi huchukizwa nacho. Mimi nachukia matendo na maneno tu na wala siyo mtu.
Njoo nikusomeee.
@ Mr Rocky. . . . TUKO PAMOJA.
Heheheheh. . . . sipendi umbea.