Chuki makazini huletwa na nini?

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari ya wakati huu ni matumaini yangu nyote mpo salama.

Moja kwa moja niende kwenye mada husika.

Najua binadamu tuko tofauti lakini ningependa kupata comments tofauti tofauti kujua nini hasa hupelekea. Chuki, visasi, roho za kutendeana ubaya, malipizi, na mengineyo yasiyopendeza huletwa na nini?

Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo?

Je, unajua zaidi yao na unaonekana kama tishio?

Au ni basi tu mtu anaamua kukuchukia bila sababu ya msingi na kukuombea kila uchwao ukumbwe na baya?

Ninakaribisha maoni.

Shimba ya Buyenze , Mshana Jr Watu8 , Omerta, @Da’Vinc , na wapendwa wengine karibuni.
 
Habari ya wakati huu..ni matumaini yangu nyote mpo salama.

Moja kwa moja niende kwenye mada husika.

Najua binadamu tuko tofauti lakini ningependa kupata comments tofauti tofauti kujua nini hasa hupelekea.

Chuki,visasi,roho za kutendeana ubaya,malipizi,na mengineyo yasiyopendeza huletwa na nini?

Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo?

Je, unajua zaid yao na unaonekana kama tishio?

Au ni basi tu mtu anaamua kukuchukia bila sababu ya msingi na kukuombe kila uchwao ukumbwe na baya?

Ninakaribisha maoni.
Shimba ya Buyenze , Mshana Jr Watu8 , Omerta ,@Da’Vinc, na wapendwa wengine karibuni.
Miafrika tulivyo ni mtu akishajua zaidi yako unaona ni tishio basi unataka kumuondoa.
Wakati wenzetu wadhungu ata uwe mweusi, pamoja na ubaguzi wao watakuchukua uwafanyie mambo yao
 
Jambo la kwanza, roho mbaya mtu huzaliwa nayo, na huwa inasubiri majira, nyakati na mazingira sahihi ili iweze kuanza kufanya kazi...

Binafsi katika kumtumikia kote mkoloni sijawahi kukutana na watu wa namna hiyo, isipokuwa nimekuwa nikipata kusikia visa hivyo toka kwa watu wa karibu...

Sababu ambazo nimekuwa nikizisikia huwa ni tofauti tofauti, lakini zote ni matokeo ya mtu kuwa na roho mbaya 'roho nyeusi'...

1. Ubinafsi - Hawa ni wale watu wenye umimi, kwamba kila kizuri kiwe chao na vibaya viwe vya wengine

2. Ufukara - Kuna watu ambao maisha yao yamegubikwa na ufukara wa mali, hivyo hujawa na chuki pale wanapoona mtu fulani yupo kwenye nafasi ya kupokea mkate mnono zaidi yao, au hata maisha yake nyumbani ni ya juu kuwazidi katika mali alizonazo

3. Kukosa weledi - Kuna watu waliopata vyeo au nafasi kwa ngekewa tu na wala sio kwa uwezo wa kiakili au taaluma, sasa kule kutokujiamini kwamba mtu anaweza akapokwa nafasi yake hufanya ajenge chuki kama njia ya kujilinda

4. Ukabila - Kuna maofisi ambayo watu wa kabila fulani ni kama wamechanjiwa kuwa wao ni wa ofisi hiyo tu, ikitokea wewe mwenyeji wa mkoa mwingine umeajiriwa au kupangiwa hapo, cha moto utakuona

5. Tofauti za kimaumbile/hulka/ulimbwende na utanashati - Imezoeleka kusikika kuwa watu wafupi huwa wakorofi sana, dhana hii ipo pia makazini ambapo kuna watu hukosa kujiamini kutokana maumbile yao, hujiona sii warembo au watanashati au hujiona wana kasoro fulani za kimaumbile ambazo zinawafanya wamuone mtu fulani kawazidi

6. Tofauti za kiimani - Kama ilivyo tofauti za kimaumbile, hata imani nayo huwa ni chanzo cha chuki baina ya mtu na mtu. Kuna ofisi ambazo imani fulani ya dini ina nguvu kuliko nyinginezo.
Pia kuna watu ambao huwa ni washirikina, hupelekea kuwachukia wale walio wacha Mungu.

7. Kuwa sehemu isiyo sahihi wakati usio sahihi - Isijekuwa pia upo mahali pasipo sahihi kwako iwe ni idara, ofisi au kitengo kiasi kwamba unazuia 'deals' za watu kufanikiwa, mathalani umezungukwa na wapigaji wakati wewe si mpigaji n.k

8. Mwisho, muhimu zaidi jichunguze wewe mwenyewe huenda una tabia isiyoridhisha inayosababisha watu kuwa na chuki nawe. Huenda chanzo ni wewe mwenyewe na si wengine.

Pitia huu uzi, utakusaidia kama umekumbwa na kadhia hii kwa sasa...
Thread 'Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki' Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki
 
Chuki nyingine ni kama tradition hazina sababu ni za kurithisha

Mfano japo sio relevant na ulicho uliza mimi jobless automatically lazima nikuchukie wewe mtumishi
 
Back
Top Bottom