SoC02 Chuki isiyo na shabaha

Stories of Change - 2022 Competition

SamNah

New Member
Aug 29, 2022
4
1
CHUKI ISIYO SHABAHA.
Makala hii inalenga jamii kwa ujumla kutengeneza chuki zisizo na lengo/dira visababisi, madhara, na namna ya kuondokana na Chuki isiyo Shabaha, Fuatana nami SamNah.

Chuki kwa maana ya kimandhari ni kitendo cha kutopenda tabia fulani au jambo fulani, kwa ufupi unaweza kusema fulani anauchukia mpira (haupendi mpira). Hii sii maana ya moja kwa moja kutoka kwenye Kamusi bali kwa nadharia ya Mazingira.

Shabaha kwa Maana ya kimandhari ni lengo/dira.

Kumekuwa na ongezeko la uadui usio na sababu za msingi katika jamii zetu unaotokana na chuki zisizo na ukweli ndani yake, Mbaya zaidi hii imeingia katika nyanja zote za maisha, kwenye uchumi, siasa, kijamii na hata kitamaduni, Mtu anaeneza taarifa za kitu kisicho sahihi kwa mtu mwingine, au kundi lingine, na huyo mtu au kundi linaingiwa na chuki juu ya huyo mtu bila sababu za msingi.

Kwa mfano, Mtu anaeneza uzushi wa tajiri furani na pesa zake, mtu anaepokea taarifa anaingiwa na chuki wakati hata uhalisia wa yule tajiri haufahamu, mfano mwingine ni mahari pa kazi, mtu anaeneza uzushi juu ya mfanyakazi mwenzake au kiongozi mahara pale, watu wanaingiwa na chuki juu ya yule mfanyakazi au kiongozi bila sababu za msingi au bila uhalisia wowote.

Nini kinapelekea Jamii zetu kuwa na Mihemko juu ya wasikiayo pasipo kufanya utafiti au kuujua ukweli na kuingia kwenye Chuki.

1. Uvivu, uvivu ni kitendo cha kutotaka kushughurisha akili au Mwili, hii inatukumbuka sana kwenye jamii zetu, unalolipokea ndilo unaloliamini, unakuwa huhitaji hata kufikirisha akili au kutaka kuujua ukweli wa jambo husika. Hii inapelekea watu kuchukia watu wengine kwa kusikia pasina kujua walichosikia ni halisi au uvumi tu.

2. Ujinga, kitendo cha kufanya jambo bila weledi au kutokuelewa jambo, hii pia inaikumba jamii yetu watu kushadadia jambo kwa kufuata upepo wa watu wengine pasipo kujua ukweli au uhalisia.

3. Wivu, pia jamii inakumbwa na chuki, kwa sababu tu, mtu hataki mtu fulani awe vile alivyo, inaweza kuwa pengine amekuzidi katika jambo fulani au na ile Roho tu, mtu hataki mtu fulani awe vile, hapo zitasambazwa habari hata ambazo si za msingi ili mradi tu Chuki izalishwe.

4. Ugumu wa maisha, hii inawakumba sana vijana, kwa sababu wengi wao wanaamini katika kusaidiwa huku wao hawataki kujishughurisha, kumekuwa na wimbi kubwa kwa vijana kupenda wepesi, pale akwamapo huzalisha chuki juu ya watu ambao anafikiri wanaweza kumsaidia na hawajafanya hivo, hapo ndipo chuki ataieneza hata kwa watu wengine.

Yapo Mengi ambayo ni visababishi vya Chuki isiyo Shabaha hayo ni miongoni tu.

Madhara au matokeo ya Chuki isiyo na Shabaa kwa jamii zetu kwa ujumla katika nyanja zote.

1. Kupungua kwa upendo, hii inatokea pale ambapo umeambiwa kitu fulani kuhusiana na mtu fulani pasipo kujua uhalisia unakuta mtu anaingia kwenye janga la kutotoa ushirikiano kama ilivyokuwa awali kulingana na uvumi au uzushi aliousikia, imewakumbuka sana watu waliopo kwenye uhusiano, mahali pa kazi, hata katika kazi mbali mbali zinazofanyika katika jamii zetu.

2. Kuvunjika kwa Udugu au Urafiki, kwa sababu tu ya maneno ya kuyasikia ambayo huleta chuki, na chuki huzaa umauti ambao ni kuvunjika kwa undugu na urafiki.

3. Inadhoofisha ushirikiano katika jamii zetu, mtu anashindwa kushirikiana na mtu Au kundi la watu kwa sababu ya maneno ya kusikia.

4. Kurudi nyuma kwa Maendeleo( Umasikini). Watu wanashindwa kushiriki vizuri shughuri za kimaendeleo kwa sababu ya uvumi au uzushi, muda mwingi unakuwa unaongelewa umbeya ambao unapelekea wao kushindwa kujihusisha na mambo ya msingi au ya kimaendeleo, lakini pia wengine hukata tamaa kwa sababu ya uvumi au uzushi ambao unawakatisha tamaa katika shughuri zao za kila siku. Yapo Mengi lakini hayo ni baadhi ya madhara au matokeo ya Chuki isiyo na shabaha.

Nini kifanyike, Makala hii inapendekeza kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo inatakiwa jamii iyazingatie ili kutoingia kwenye mtego wa Chuki isiyo na Shabaa kwa sababu tumeshaona madhara au matokeo kwa Jamii, hivo kuna haja ya kuepukana nayo;

1. Kuutafuta Ukweli, waswahili husema japo ni Tiba ukweli unauma, pia Wahenga walisema dawa Chungu/kali ndio hutibu, hivo sisi kama jamii tusikimbilie kuchukia pasipo kuujua ukweli tusikimbilie hitimisho la maamuzi ya mwisho pasipo kujua uhalisia, pamoja na kuwa unaweza kuzalisha mambo mengi lakini utakuwa salama na Chuki isiyo na Shabaha.

2. Tuache kasumba ya kufuata mkumbo wa uwingi au upepo wa lisemwalo ijapokuwa kweli yenyewe hatuijui, hapa jamii yetu inachangamoto kubwa kwa kuwa asilimia kubwa Kwenye jamii zetu uongo au uzushi unaenezwa kwa kasi na unakubalika kwa urahisi kuliko ukweli wenyewe watu tunapenda sana uvumi na uzushi kuliko kawaida, tumejijengea utamaduni huo kitu ambacho si sawa kabisa, tafadhri inatakiwa tubadirike ili tusijenge Chuki isiyo na Shabaha.

3. Tujenge utamaduni wa kuzishughurisha akili zetu, tusijidekeze kwa kukaa kupokea kila tunalolipokea la hasha tujiridhishe kwa kuzifanya akili zetu zifanye kazi kwa kina itatusaidia kuondokana na Chuki isiyo na Shabaha.

Misingi ya jamii yetu ni Upendo, udugu, Ushirikiano, Waneni hunena Undugu ni kufaana na si kufanana, Tuijenge jamii yenye kuishi kwenye uhalisia na ukweli na si vinginevyo.

Asante kwa kufuatilia Makala/Andiko hili karibu kwa Andiko lingine.
 
Back
Top Bottom