Chuki dhidi ya mende... Nahau inayotufaa watanzania

Chuki dhidi ya mende... Nahau inayotufaa watanzania

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,146
Reaction score
48,382
Ufuatiliaji wangu mdogo wa masuala ya kisiasa, umenifanya nifahamu kuwa asilimia tisini na tisa nukta tisa tisa (99.99%) ya machafuko ya kisiasa na kijamii kwenye nchi zote duniani, husababishwa na wanasiasa walioko madarakani.

Lakini miongoni mwa nahau ambazo hutumiwa na watawala dhidi ya wanaowapinga, ni kuwaita watu hao Mende.

Nadhani watawala hutumia mende kuonesha uhalali wa kuwadhuru wapinzani wao kama vile kuondoa mende majumbani mwao.

Nimekutana na maelezo haya kuhusu mende. Kwenye bango hilo hapo chini, kuna maelezo kuwa chuki dhidi ya mende iliwafanya siafu wapige kura ili inyunyizwe dawa mende wafe na kusahau kuwa dawa hiyo itawaua na wao pia pamoja na walioacha kupiga kura.

Kwa kipindi kirefu mashambulizi ya kutaka kuiua CHADEMA toka kwa CCM yamekuwa yakichagizwa na vyama vingine vyenye kiwi cha macho kwa CHADEMA na watanzania "wema" wanaosema hawajishughulishi na siasa.

Hivyo vyama na hao watanzania wanaojiona kuwa wao ni wema wasiojishughulisha na siasa hawajui kuwa madhara ya kutokuwepo kwa CHADEMA, yatawadhuru na wao pia.

snaptik_7594911656732314936_0_v2.webp
 
Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya "Content creators" lakini Jiji kama la Dar halina maji safi na salama.
 
Back
Top Bottom