Chozi la Damu

Munyaluganda

Member
Jul 13, 2022
7
21
Sheheni za siraha, dunia uwanja wa fujo,
Atomiki makombora, jehanamu ya fumbo,
Kisiwa cha miba, wenye nguvu ulimbombo,
Utu umetoweka, mauaji kila uchao.

Kiburi chao pesa, zilizofungwa kwenye fuko,
Pesa dhihaka ya dunia, li wapi chimbo,
Siraha za kisasa, mikogo yao matambo,
Binadamu gunia sifa, ukuu wake Mungu.

Mauaji kila kukicha, wachache washangilie ubwenyenye,
Pesa msaliti imeandikwa, ibada sadaka na semina posho,
Siraha nzito kwa mataifa, kumuondoa mwanadamu ndio lengo,
Ni ukichaa wa wasomi, na sio dhana ya kweli ya elimu.

Laana gani wanadamu kuuana, ndizo nyakati za mwisho,
Mungu shusha neema, machozi ndo letu bubujiko,
Wazee wetu fufuka, mkauone uozo wa dotikomu,
Kuuana kizazi cha nyoka, kila nafsi itaonja mauti.
 
Back
Top Bottom