Choo inapokuwa Bora kuishi kuliko Sebure!

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Kwenye hotuba ya Dr. Slaa wakati akizungumza na vyombo vya habari majuzi, alifananisha kitendo cha Mh. Lowasa na Sumaye kutoka CCM kwenda CHADENA kama Kuchota kinyesi chooni na kukipeleka sebureni.

Naona hilo CCM wanakubaliana nalo na ndiyo maana waliandaa vijana kwa kuwavalisha T-shirt za Chadema na kuwataka waandamane ili kuunga mkono hotuba hiyo. Kukubalika kwa hotuba hiyo vilevile kunadhihirishwa na kurudiwa rudiwa mara kwa mara kwa hotuba hiyo katika vyombo vya habari vya TBC1, Star TV na Clouds TV ambao ni wakala wa CCM na pia jitihada za kutaka kumpa muda zaidi wa hewani katika vyombo vya habari ili aendeleze kazi hiyo.

Kwa hatua hiyo basi tukubaliane kwa pamoja kwamba CCM ni Choo na CHADEMA ni Sebure.
CCM na Vyombo vya habari vya TBC, Star TV, Clouds TV vimekomalia saana kitendo cha bonge moja la kinyesi kutoka chooni kwenda sebureni na kunyamazia lundo la vinyesi vilivyojaa chooni. Hoja kwamba Lowasa alitajwa katika orodha ya mafisadi ya Mwembe yanga na katika kashfa ya Richmond.

Hebu angalia baadhi ya waliotajwa katika orodha ya Mwembe Yanga ambao kwa mujibu wa Dr. Slaa ni vinyesi vilivyobaki chooni.

1. DR. DAUDI T.S. BALALI
Dr. Daudi Balali alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997 hadi 2007. Inasemekana alifariki akiwa matibabu Marekani. Kifo chake kina utata na wanaodai ukombozi wa nchi hii kupitia UKAWA na hata walio nje ya UKAWA, kwa njia ya mabango kwenye mikutano ya kampeni ya uraisi 2015 wanamtaka mgombea wao Lowasa akiingia madarakani amrejeshe nchini.(Kama kweli alifariki, Mweyezi Mungu Amuweke mahala panapostahili, Amen!)

2. ANDREW J. CHENGE
Mheshimiwa Andrew Chenge anagombea Ubunge wa Bariadi Magharibi kwa tiketi ya CCM kwa mara nyingine.Wakati orodha inatolewa Chenge alikuwa ni Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa "mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria…." Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili,

3. BASIL P. MRAMBA
Mheshimiwa Basil Mramba alikuwa Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo. Wakati orodha ya mafisadi inawekwa hadharani alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha.

4. GRAY S. MGONJA
Bwana Gray Mgonja alikuwa Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile alikuwa Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na alishikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ilihusishwa na ufisadi uliomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge.

5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA
Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Wakati wa kutolewa kwa orodha ya mafisadi Bwana Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited.

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO
Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji kwa tiketi ya CCM na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali iliainisha kuwa Benki Kuu alikuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60.

7. BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Kufuatana na maelezo ya List of Shame, ufisadi wote ulioelezewa hapo juu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Kuna ushahidi kwamba akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi.

8. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kufuatana na maelezo ya List of Shame, kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi ikiwemo mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited, Kahama Mining Corporation Ltd,IPTL na bado kuna minong'ono ya kashfa za Ricmond, Simba Trust ya Australi n.k.



  • Makada wengine nje ya List of shame:
Lakini bado kuna makada wengi ambao hawakutajwa katika orodha hiyo ambao walijitokeza katika kasfha zilizofuata, mfano:

Kashfa ya Escrow:
Kuna ushahidi kwamba Harbinder Singh alishirikiana na ikulu na ccm kuiba fedha za Escrow. Mtu huyu anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North', jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara

Pamoja na huyo kuna Chenge, Muhongo na Tibaijuka wote wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM. Hawa ni mawaziri watarajiwa endapo CCM itaingia tena madarakani. Wengine waliopata mgao kupitia Stanbic bank hawajatajwa, lakini kwa vyovyote vile hawawezi kuwa wana UKAWA au hawawezi kuwa wapumbavu au malofa.

Wengine walishiriki kusafirisha wanyama hai kwa ndege nje ya nchi.

Hebu tumuangalie mgombea urais Mh. Pombe Magufuli:

Kashfa ya Bomoa Bomoa
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitoa hukumu katika kesi namba 80 ya 2005 iliyofunguliwa na Ndg Proches Tarimo na wenzake dhidi ya Wizara ya Ujenzi kupinga amri ya kuboma nyumba za wananchi zilizoko Mita 120 toka katika ya barabara pande zote; eneo la Mbezi Mwisho katika barabara kuu ya Morogoro. Amri hiyo ilitolewa na TANROAD mwaka 2004, ikidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria hiyo. Itakumbukwa kuwa amri hiyo ya TANROAD ilitolewa miaka mitatu tu baada ya Mhe John Magufuli kuteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Rais Benjamin Mkapa, ilihali wananchi hao wamekuwa wakiishi maeneo hayo mika nenda rudi pasipo usumbufu wowote. Huku Mhe John Magufuli akijigamba "kufuata, kulinda na kutetea sheria" ya "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967" Mahakama Kuu ilitamka kuwa ilipoteza uhai tokea mwaka 1999.; tokea mwaka 2002 Mhe Magufuli aliwasababishia wakazi waishio pembezoni mwa barabara nchi nzima madhara makubwa ya kisaikolojia, Kijamii na Kiuchumi kwa kuvamia maeneo yao. Wengine waliokumbwa na bomoa bomoa ambayo baadaye ililipwa na serikali nikituo cha mafuta cha Mwanza. Kwa nyakati tofauti Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda alimpiga stop kwa zoezi hilo na pia Mh. Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kumwambia aache ubabe katika zoezi la bomoabomoa. Kama sio hao Tanesco Ubungo ingekuwa chini, melium towers kijitonyama ingekuwa chini huenda hata wewe unayesoma hapa jengo lako lingekuwa chini.

Tafakari Uuzwaji wa nyumba za serikali, wanakigamboni kupiga mbizi, hasara ya meli na Samaki wa Magufuli, ufisadi wa fedha za barabara kwa mujibu wa riport ya CAG hayo yote yamejadiliwa vyakutosha na wananchi. Haya yote mchambuzi wa ufisadi Dr. Slaa hayaoni kwakuwa bado yako chooni hadi pale yatakapokuja sebureni.

Kumbuka hatujasikia Rostum Azizi akitoka CCM, hatujasikia Kalamagi akitoka CCM, hatujasikia Msabaha akitoka CCM. Bado wamejichimbia chooni.

Mimi naona UKAWA wana kazi ndogo tu. Kuwapokea wale waliojitambua kuwa wanaishi chooni, kuwapiga brush na povu la sabuni, tumia maji tu watakuwa tayari na sifa ya kukaa sebureni ambamyo ni CHADEMA.

UKAWA mwaacheni Dr Slaa na CCM wajiaminishe kwamba wanaoishi chooni wanaweza kuwa wasafi siku moja. Anasahau kwamba Mtu yeyoye kitoka sebureni akatumbukia chooni atachafuka tu na wala hawawezi kusema inawezekana mtu akaishi chooni akawa msafi haiwezekaniiiiiiiiiiiii! Lakini mtu akiokolewa toka chooni au akajiokoa mwenyewe toka chooni anasafishika, hilo pia halina ubishiiii!

Nasubiri sasa kusikia TBC1, Star TV, Clouds, Uhuru, Mzalendo mkisaidia kupigia kelele kwa waliobaki chooni wazinduke, watoke chooni waende bafuni wasafishwe ili hatimaye waingie sebureni kwa kazi moja tu; Kudai katiba mpya iliyozingatia Rasimu ya pili ya Jaji warioba na kupitia hapo kuleta mbadiliko na kujenga Tanzania mpya yenye kuheshimiana vyama vyote, vya sebureni na vya chooni.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ubariki UKAWA!
 
Ni Kheri kuishi chooni badala ya kuishi kwenye sebure inayonuka kinyesi - By Dr. Slaa
 
SIFA ZA VIGEU GEU

Dr. Slaa alipowashambulia mafisadi alikua shujaa wao CHADEMA ila leo wamehamishia kinyesi chumbani Dr.Slaa anawashambulia tena mafisadi wale wale anaonekana msaliti tuwaelewe vp ninyi?

Watu wakiandama kuwasapoti yanakuwa mafuriko
Wakiandama kuwapinga wanakuwa wamenunuliwa
😂😂😂😂

Hapa kazi tu
Chagua Magufuli ili tuepeuke usanii usiokuwa wa lazima
 
Kuna hatari wote tukanuka mavi maana huu ushabiki wa kivyama inafikia watu kujisahau kama Nchi ambayo ndio kiunganishi cha watanzania na sio vyama.
 
Huo ni mchezo mchafu na hatarishi Sana unaochezwa na majiz ccm. Siasa chafu zishapitwa na wakati, leta hoja ujibiwe kwa hoja sio mnacheza mchezo unaoweza kuvuruga amani ya nchi. Hao wanaoandamana tunajua kabisa ni uvccm ndio wanaocheza huo mchezo na wananchi wapo tayari wakiwaona watawashambulia kwa kipigo murwaa kabisa ili watie hadabu. Makufulu syo saizi ya Lowasa ata kidogo naona ccm wanajitekenya na kujamba wenyewe.
 
Back
Top Bottom