Chonde chonde TANROAD mkoa wa Tanga

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
400
665
Uongozi wa TANROAD mkoa wa Tanga amkeni usingizi huko mlipo au kama mpo likizo basi wanao kaimu pokeeni KERO hii na muifanyie kazi haraka.

Barabara ya kuunganisha mikoa ya Kaskazini kipande Cha Segera hadi KOROGWE maeneo ya Kijiji cha Mandera katika DARAJA linalounganisha Wilaya ya HANDENI(v) na KOROGWE.

Daraja hili limekuwa KERO kubwa kwetu wasafiri kwa ubovu uliopo unaopelekea kuharibu vyombo vyetu na pengine linaweza kuleta maafa kama halitashughulikiwa.

Kipande Cha kutengenezwa/kufanyiwa marekebisho ni kidogo sana kimejaa mashimo ,na tangu daraja hili kipande cha lami kuondolewa hakijatengenezwa hadi Sasa takribani miezi miwili imepita hakijafanyiwa kazi.

Msisubiri matatizo yajitokeze Kwa kusababishwa na ubovu huo ndiyo mjitokeze na kurekesha.
 
Back
Top Bottom