Honest One
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 235
- 274
Habari zenu wana JF, nipende na mimi kutoa la moyoni kuhusu hili suala linalowahumiza walimu wa sekondari masomo ya sanaa. Kusema ukweli baada ya kutolewa lile tangazo walimu tajwa hawana raha kila muda ni kuwaza namna ya kuhepuka hiki kikombe.
Kwakuwa serikali imeshaamua hivi na sisi hatuna la kufanya basi tunawaomba huu mchakato ufanywe na wataalamu toka TAMISEMI au wizara ya elimu kuhepusha vitendo vya rushwa,upendeleo na kujuana kutoka kwa maafisa elimu na wakuu wa shule.
Hapa vingewekwa vigezo ambavyo vitaondoa lawama na vitendo viovu nilivyovitaja awali.
Mapendekezo yangu ya walimu ambao wangepelekwa shule za misingi ni kama yafuatayo;
i) walimu walioazimwa 2009 zilipoanzishwa shule za kata. Hawa walikuwa walimu wa shule za misingi kutokana na upungufu uliokuwepo kipindi kile ilibidi wapelekwe sekondari kwakuwa walikuwa wameshajiendeleza.Hili kundi lingefaa sana na ni ngumu kutekelezwa ikiwa ni maafisa elimu watachagua kwa sababu wengi washapewa madaraka mbalimbali wengine ni wakuu wa shule kabisa.
ii)walimu wa diploma,hawa hawana tofauti sana na walimu wa grade A,hata vyuo wanasoma pamoja hivyo na walimu wao ni walewale lakini pia itakuwa ni matumizi mabay ya rasilimali watu ikiwa wa degree anaondolewa anabakizwa wa diploma kwakuwa hata SERA ya elimu ya 2010 inaeleza wazi kuwa mwalimu mwenye stashahada (diploma) inabidi afundishe kidato cha kwanza hadi cha pili tu. Sasa hawa watu bila maofisa kutoka huko juu si rahisi kupelekwa msingi kwa sababu ndo wanaopendwa na maafisa elimu na wakuu wa shule kutokana kujipendekeza kwao na unynyekevu wa hali ya juu jumlisha na janja janja zao.
iii)Kuna wale waliosoma degree kipindi mh. Kikwete, unakuta mtu ana E mbili na subsidiary moja anaenda chuo kikuu. Hawa nao ni wakuangaziwa sana.
iv)Kuna wale waliosoma kwa kuungaunga sana,unakuta o'level anavyeti vitatu inamaana amerisiti mara kibao, au mtu amepiga QT mwanzo mwisho,hawa nao si wakufumbia macho. Tunao huku makazini haya mambo ya kitaaluma hawayawezi kabisa.
Kwakweli mkifuata vigezo hivi na bila kuwashirikisha maafisa elimu na wakuu wa shule,vilio vitapungua sana kwasababu mtu ataona alistahili kabisa.
Nasisitiza tena wakuu wa mashule na maafisa elimu wasishirikishwe na waonevu na wala rushwa wakubwa(pesa na ngono),vile vile watatumia hii fursa kama adhabu kwa wale walimu wasioelewana na wakuu wao au wale wasiowanyenyekea.