Kijuram
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 513
- 374
Baada ya mchakato wa kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM kukamilika, Mh. Lowassa naomba nikusihi uendelee kusaidia jamii za watu mbali mbali kama ulivyokuwa ukifanya katika kipindi cha miaka mitatu iliopita. Uendelee kushiriki harambee za kuchangia ujenzi wa makanisa na misikiti, shule, uendelee kuwawezesha bodaboda na jamii nyingine mbali mbali. Bado tunauthamini na kuuhitaji mchango wako hata kama lengo la kuingia magogoni halikutimia. Hiyo yote ni mipango ya Mungu.