BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
Unajua mkuu heshima mbele,
Yaani sasa nimeanza kuchoshwa na hii drama, I mean ni nchi gani duniani watu wenye ushahidi dhidi ya watuhumiwa, na watuhumiwa wenye ushahidi dhidi ya wanaowatuhumu, wanashauriwa wasiende mahakamani, hivi umemsikia hata balozi mmoja toka nje akisema msiende mahakamani?
Amani itapungua? Hivi ni amani ipi hiyo wanayoisema? Mwananchi anakuwaje na amani wakati haiamini serikali yake? Mimi nilifikiri huu ndio wakati wa CCM kujisafisha na kujiweka sawa maana ni kwenda mahakamani kushinda na kuwamaliza kabisaa upinzani, I mean kweli unahitaji kuwa political science professor kuelewa kuwa kama kweli hawa viongozi waliotuhumiwa hawana makosa as of their claim, basi CCm ni kuwasafisha na kuwa-bulldoze tu upinzani for the rest of their political life au career?
Yes huu ndio utakuwa mwisho wa Zitto, na upinzani kwa ujumla iwapo watashinda mahakamani, maana kama hakuna ushahidi dhidi yao basi ni kuwafungulia Treason Charge kina Dr. slaa na Zitto, tena kwa kuhatarisha amani yetu hebu niambie ni mtu gani duniani atakayelalamika?
Tunawaambia wanayamaze, lakini hawasikiii, what a drama? Hawa walikuwa wamezoea kujificha nyuma ya Mwalimu, that party is over, mambo yawekwe hadharani tu, next stop Mahakamani tukamkome nyani mchana kweupe!
Mkuu, Watanzania wengi tungependa sana kuona hao waliochafuliwa heshima zao wanafungua hii kesi. Kama kweli hakimu atakayeendesha kesi hii akiwapa uhuru pande zote mbili katika kesi hiyo basi tunaweza kusikia mengi mno ambayo yanaweza kabisa kutuacha Watanzania midomo wazi kwa maovu tutakayosikia.
Wakati huo ukumbuke jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta alipokuwa anastaafu alitamka kwamba mahakama imejaa rushwa ya hali ya juu kiasi kwamba alikuwa anakosa usingizi kwa rushwa jinsi ilivyokithiri. Mahakama bado ni zile zile na hakujafanyika chochote ili kupambana na uozo huo. Hivyo rushwa katika kesi hiyo itakuwa kama kazi na mwenye pochi kubwa katika kesi hiyo (tunawajua ni akina nani) watashinda bila matatizo yoyote na kutuacha Watanzania bado na majonzi chungu nzima kuhusiana na hali halisi ya nchi yetu.