Chonde Chonde Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde Chonde Kikwete!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Oct 7, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mchakato wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu unaonyesha ccm na hasa kikwete imepata upinzani mkubwa sana ambao hawajawahi kuu-experience na wala hawakuutegemea, imekuwa 'surprise' nakuleta ' a big shock' kwa ccm.

  Upo uwezekano mkubwa wagombea wa vyama mbadala wakapata ushindi dhidi ya ccm na Kikwete kama uchaguzi na uhesabuji kura utakuwa wa haki bila kuchakachuliwa.

  Tunahitaji amani katika nchi yetu na ni katika hili namuomba Kikwete awe sehemu ya historia nzuri ya taifa letu kwamba ahakikishe kura haziibiwi kabisa , iwe kwa faida yake ama ya wapinzani wake. tuachiwe wapiga kura tuamue na kuchagua viongozi tunaowataka.

  Kama Kikwete akishindwa basi akubali kukabidhi serikali kwa amani; Atakuwa amejiweka kwenye historia nzuri sana ya Tanzania na kuweka msingi mzuri sana wa kubadilisha uongozi wa nchi kwa amani kama nchi za Marekani na Uingereza na nyingine nyingi tu. Hakika katika hili hatasahaulika hata kwa vizazi vyetu vijavyo kwa sababu atakuwa ni raisi wa kwanza Tanzania kukubali demokrasia ifuate mkondo wake.

  Mkapa, akiwa bado madarakani katika awamu yake ya pili alishawahi kuulizwa kwamba 'Jee atagombea tena uraisi kwa awamu ya tatu?' alijibu kuwa katiba ya Tanzania hairuhusu mtu kuwa raisi kwa vipindi zaidi ya viwili na wala hakugombea tena kwa awamu ya tatu; hii ilimpa heshima kubwa kwamba kwa kipengele hiki aliiheshimu katiba. Kikwete tunaomba ufanye vivyo hivyo.

  Hali kadhalika, kama Kikwete ataamua kung'ang'ania madaraka hata kama demokrasia itakuwa imeamua vingine, bado atakuwa amejiweka kwenye historia lakini sasa itakua ni ile mbaya kama ya Robert Mugabe na ambayo pia haitasahaulika hata kwa vizazi vijavyo kwa sababu uamuzi wake huu(kama atafanya) utaiingiza nchi katika machafuko ambayo kwa kweli hatuyataki. Funguo za amani au machafuko ya nchi yetu anazo Kikwete.

  Tukirudi nyuma Kikwete alikuwa miongoni mwa wasuluhishi wa mgogoro ulioikumba Kenya baada ya uchaguzi ambapo alitangazwa kuwa mshindi, ushindi uliolalamikiwa sana na wakenya hata kufikia kumwaga damu . Je Kikwete yuko tayari kumwaga damu ya watanzania kwa kutufanyia yale yaliyompeleka Kenya kuwasuluhisha akina kibaki na Odinga? Je anajua kuwa jumuiya ya kimataifa pamoja na Kibaki na Odinga aliokuwa akiwasuluhisha wanafuatilia kwa makini mchakato wa uchaguzi wa Tanzania? Je atajibu nini atakapoamua kufuata yale ya kibaki na Mgabe?

  Chonde chonde Kikwete muogope Mungu fuata haki na Mungu akusaidie
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,347
  Likes Received: 22,199
  Trophy Points: 280
  Sasa wana mpango wa kuchakachua kura, hivyo basi wamewatuma jeshi na polisi kuujulisha umma kuwa wajiandae kwa wizi wa kura ambao CCM wataufanya.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona wanataka Koffi Anan aje kutusuluhisha.
  WHAT A SHAME KWA WOTE WATAKAOSABABISHA FUJO
   
Loading...