Chonde-chonde chadema msituangushe tuliopoteza matumaini!

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Naingiwa na hofu kila ninaposikia migogoro ya aina mbalimbali ndani ya CDM. Zito, mitazamo yake na ukaribu wake na Tiss (waliojipa majukumu ya kuilinda CCM dhidi ya wananchi walioichoka kwa udhaifu na uchafu wake CDM majority wakiwa wamojawapo), John Shibuda na kauli zake na hii ya Madiwani wa Arusha ni mifano inayonitia hofu sana tu.

Kingine ambacho si wengi watapenda kukisikia ni jazba na kuendekeza mipasho Bungeni. Katika hili ninahofia baadhi ya taarifa zinazotolewa na Mh. Lema kama mahala alipotoa taarifa baada ya Mh. Machali kumkejeli Membe (Naamini kijana huyu hakuwa serious) kwamba anatarajiwa na wengi kuwa rais wa nchi hii. Taarifa aliyoitoa Lema haikuwa na ulazima saana na kimsingi haikuwa taarifa na hata Mwenyekiti wao aliona hivyo. Katika hili nahofia kwa sababu tunaofuatilia Bunge kwa ukaribu tumejenga imani kwamba mara nyingi anaposimama Mbunge wa CDM hata kama ni kuomba mwongozo wa spika panakuwa na hoja ya msingi. Kwa ufupi miongoni mwetu unapotaja CDM watu tunawaza "Umakini" pengine ndiyo maana Dr. Slaa anaheshimika sana. Kwa hili naomba mshauriane vizuri ili tuwe na wabunge wenye umakini wa Lissu, Mnyika, Mbowe, Zitto na wote ambao wana JF wengi tunawaona na kukubali kazi zao.

Pamoja na yote hayo naomba CDM waelewe kwamba mpaka sasa wao si malaika wa siasa hapa nchini bali ni chaguo pekee kwa wote tuliochoka na magamba. Hii ni kusema kwamba wasipokuwa makini na watu wanaokuwa nao chamani na kutatua tofauti zao kwa njia ya ustaarabu tutakata tamaa na sijui nini kitatokea. Msishangae badala ya kupata wabunge zaidi na ikiwezekana rais next election kura zinapungua na ikitokea hivyo siwafichi nchi inakwisha. Lowasa, Karamagi, Rostam, JK, Chenge nk wameshapora vya kutosha na ikitokea wakapata mtu wa kuwalinda madarakani 2015 nchi itakuwa inaandaa mafisadi wakubwa wengine kama vile akina Sitta, Membe, Nnape na wengine wanaohangaikia Ikulu sasa hivi. Hawa watakuwa bize kupora wakati huo and it will all be your fault.

Mpaka muda huu CCM ndiyo kikwazao kwa maendeleo ya taifa. Wao wanaporushiana maneno hadharani na kupitia vyombo vya habari tunajua kinachowasumbua ni matumbo yao kwa kuwa ndiyo sifa yao kubwa, sasa iweje na nyie mfuate mkumbo huo kwa matatizo madogo madogo? Kama Shibuda ni mamluki basi hilo ni tatizo lenu kung'ang'ania idadi ya viti Bungeni pasipokujali ni nani anapewa tiketi yenu wala tabia yake. Swala la Zitto pia sijui tatizo ni nini kama ni tofauti za mitazamo ni bora mkae pamoja myamalize.

Please guys pull yourselves together and go to work while they are still fighting for their bellies! Msijekusema sikuwaambia!

Chonde chonde jamani! Kungekuwa na chama kingine chenye japo 0.25 ya uwezo wenu ningewashauri wajipange lakini hakuna. Acheni migogoro isiyo ya lazima....Please!
 
The Analyst,

Kwa kweli umetoa mawazo mazuri,kweli wewe ni rafiki wa mabadiliko tuyatarajiayo...nitashangaa sana kama kuna atajiita mpenda mabadiliko wa kweli atakayekuja hapa na kukukejeli.Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo na ni jukumu la anayeshauriwa kupima na kuchukua hatua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom