Chombo chatumwa kutafuta uhai Mars

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,501
28,703
Chombo chatumwa kutafuta uhai Mars

Wataalamu wa anga za juu wa Ulaya kwa ushirikiano na wenzao wa Urusi wamerusha angani chombo cha anga za juu kitakachofanya utafiti kubaini iwapo kuna uhai sayari ya Mirihi, kwa Kiingereza Mars.

Chombo hicho kwa jina ExoMars Trace Gas Orbiter (TGO), kimepaa kutoka Baikonur nchini Kazakhstan saa 09:31 GMT.

Chombo hicho kitafanya uchunguzi kubaini iwapo gesi ya Methane ambayo imepatikana katika anga ya sayari hiyo inatokana na shughuli ya kijiolojia au inatokana na viumbe hai.

Mambo yote yakienda ilivyopangwa, wataalamu wanapanga baadaye kurusha mtambo wa kusafiri juu ya sayari, kwa kimombo rover, ambao utatumiwa kuchimba chini ya ardhi ya Mars.

Mtambo huo, utaunganishiwa nchini Uingereza, unaweza kurushwa mwaka 2018 au ukichelewa mwaka 2020.

Inakadiriwa kwamba itachukua roketi iliyobeba chombo cha TGO saa 10 ili kujiweka kwenye njia sahihi ya kuelekea sayari ya Mars.

Safari ya chombo hicho hadi Mars inatarajiwa kuchukua miezi saba, na sehemu ya chombo kwa jina Schiaparelli inatarajiwa kutua Mars tarehe 19 Oktoba. Sehemu ya setilaiti ya chombo hicho itazunguka sayari hiyo ikikusanya maelezo muhimu kuhusu hewa na gesi zinazopatikana katika sayari hiyo.

Safari ya chombo hicho inafuatiliwa na wataalamu wa Shirika la Anga za Juu la Ulaya mjini Darmstadt, Ujerumani.
Mradi huo wa TGO ndio wa kwanza kabisa kufanywa na Ulaya na Urusi kwa pamoja kuelekea sayari ya Mars, ambayo ndiyo ya nne kutoka kwenye jua.

Uchunguzi wa awali wa setilaiti zinazozunguka dunia na rover ya Curiosity ya Marekani umebaini kuwepo kwa haidrokaboni ingawa za vipimo vya chini sana katika sayari hiyo.

Moja ya mambo yanayoweza kuwa yanachangia kuwepo kwa gesi hizo ni shughuli za kijiolojia ndani ya sayari hiyo ambapo maji yanaweza kuwa yanachanganyikana na mawe na kuzalisha gesi ya haidrojeni ambayo baadaye inageuka na kuwa methane.

Jambo jingine linaloweza kuwa linasababisha kuwepo kwa gesi hiyo ni kuwepo kwa viumbe hai.

Sehemu kubwa ya gesi ya methane duniani hutokana na viumbe hai.
4b321be544f5c089decc982d556e8718.jpg
 
shughuli za kijioloji
miezi saba....
kitatumia masaa takribani 10 kujiweka sawa..
what a project

anyway ngoja tuvumilie huwenfa kuna viumbe wenzetu huko na huwenda wakawa wanaongea lugha inayo karibiana na ile ya kwenye migodi iliyo mingi....
 
iko siku watapata wanachokitafuta.....na hapo ndio watamjua Aliewaumba ana Nguvu Kiasi gani,maana wanampima...
 
Sisi Tanzania bado tuna shida ya madawati mashuleni..na ukosefu wa vyoo vya kutosha kwenye shule zetu ha ha ha ha , alie tuloga kafa.
 
Back
Top Bottom