Chombo cha India chatua Mars

Chombo cha India chatua Mars

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,574
Reaction score
53,613


140924041007_mars_624x351_bbc_nocredit.jpg


India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari

India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari ya Mars


Wanasayansi wa anga za juu nchini India wanasema kuwa chombo chao cha safari za anga za juu kwa sasa kinazunguka sayari ya Mars.

Hii ndiyo mara ya kwanza kwa India kutuma mtambo wake kwenda kwa sayari hiyo, safari ambayo imepata umaarufu kutokana na gharama yake ya chini kabisa ya dola milioni 75 pekee.

India ndilo taifa la nne duniani kufaulu kufikisha chombo katika sayari ya Mars.
Mataifa mengine ambayo yamewasilisha vyombo vya utafiti wa anga za juu katika sayari hiyo ni Marekani Urusi na muungano wa mataifa ya Ulaya.

Chombo hicho ''The Mangalyaan robotic probe'' kinatarajiwa kuanza upekuzi na uchunguzi wa hali ya anga katika sayari hiyo nyekundu.

Waziri muu nchini India Narendra Modi ambaye alishuduia mafaniko ya chombo hicho kilichoanza safari yake miezi kumi iliyopita aliwapongeza wanaayansi hao kwa ufanisi huo mkubwa.


131105151107_mars_mission_india_ap_624x351_ap.jpg


Roketi ya India 'Mangalyaan iliyotua katika


Aliwaambia kuwa mafanikio ya safari za anga za ju nchini India ni mfano mwema wa hatua ambazo taifa hilo linaweza kupiga akisema kuwa ana mpango wa kuboresha kitengo hicho.

Shirikisho la anga za mbali la Marekani NASA ambalo lilifikisha chombo chake ''Maven'' katika sayari ya Mars Jumatatu wiki hii, liliwapongeza wanasayansi wa India kwa ufanisi wao.

Kupitia kwa ujumbe wa mtandao wa Twitter NASA iliandika kuwa ''Tunawapongeza @ISRO kwa kuwasili katika sayare ya Mars Mtajiunga na marsOrbiter kutathmini hali ilivyo katika sayare hiyo.


Source:BBC Swahili
 
Big up to Indians. They really deserve to be congratulated after succeeding to orbit Mars on their first attempt. This is very amazing, demonstrating a very high degree of engineering Excellency.

At this speed, India and China will overtake US and dominate the scientific world in the near future
 
Kwa kuwa hakuna namna ya kuthibitisha, hata wakisema wametua Juani ni sawa tu.. Malaysia Airline jet mpaka leo haijulikani ilipo, ila sayari Mars wanajua ilipo , sawa tu, kweli Bollywood imepiga hatua kubwa sana looh ... !!
 
Hivi india sio ndo taifa la kwanza kufika mars?.
 
Kwa kuwa hakuna namna ya kuthibitisha, hata wakisema wametua Juani ni sawa tu.. Malaysia Airline jet mpaka leo haijulikani ilipo, ila sayari Mars wanajua ilipo , sawa tu, kweli Bollywood imepiga hatua kubwa sana looh ... !!

Mswahili tu ndiye hana uwezo wa kuthibitisha, lakini uncle Sam kule Marekani anajua hili.
 
Kwa kuwa hakuna namna ya kuthibitisha, hata wakisema wametua Juani ni sawa tu.. Malaysia Airline jet mpaka leo haijulikani ilipo, ila sayari Mars wanajua ilipo , sawa tu, kweli Bollywood imepiga hatua kubwa sana looh ... !!

Kina faida gan wakati nchi yao ina watu wengi wenye umaskin wa kutupwa?
 
kinachoponza nchi yetu ni ujasiriamali wa misemo ya kiswahili mf"stadi yakinifu inafanyika" "mchanganua unaendelea"maneno ya ki "k" "k" nisiyoyapenda kweli kweli || EBU LOWASSA AJE AONDOE HII MISEMO WATANZANIA WAMEICHOKAAA! EBO!
 
Back
Top Bottom