❮SEHEMU YA 67❯
TULIPOISHIA..<<<
Basi baada yakumaliza kufanya maombezi katika jiji
la Kampala nchini Uganda, atimaye ndege
mahalumu kabisa toka nchini Canada ilifika Entebbe
International Airport nakutusubiri hapo. Tulifika
uwanja wa ndege mapema alfajiri nikaiona ndege
kubwa yenye maandishi ubavuni mwake yanayo
someka
AIR CANADIAN WORSHIP
Tukatazama usoni Jofu alafu kila mmoja akauvuta
mdomo wake pembeni nakutengeneza tabasamu
changa. Zikafanyika taratibu kadhaa hapo kisha
tukaingia ndani ya ndege iyo kubwa sana tayari kwa
safari ya kuelekea ulaya au America ya kasikazini.
____ENDELEA NAYO___
Tulipopaa tu angani nikamwambia Jofu;
❛Jofu Nasikitika kukwambia kuwa sirudi tena
Tanzania au nyumbani.. ❜
Kisha machozi yakaanza kunitoka, kwakuwa tulikuwa
tumekaa seat moja basi Jofu akanikumbatia huku
akiniambia;
"Upo sahihi kabisa Mama hakuna sababu yakurudi
tena nyuma kuna nini cha maana kilicho baki
kwanza zaidi ya maasi na maovu yanayofanywa kila
siku twende Mama twende tukamtumikie MUNGU ili
tuishi maisha ya furaha na amani.!!"
Safari ilikuwa ndefu sana na kilicho saidia ni
kwamba hii ndege ilikuwa ni special kwa safari za
nchi nne tu yani ikitoka Dar es salaam inaweka
kituo Ethiopia, ikitoka hapo inatua Egypt (Misri)
baada ya hapo inakuja Turkish alafu ndio inakuja
Emirates (Dubai) ikiluka hapo ndio moja kwa moja
mpaka Toronto au Ontario Canada.
Izo ndio route za hii ndege ivyo hakuna kusimama
simama ovyo njiani kama daladala.
Safari ilikuwa ndefu sana maana toka Dar mpaka
Toronto kwa usafiri wa ndege inatumia masaa 16
na dakika 26. Kwaiyo kwakuwa tulitoka saa moja
asubuhi ivyo Canada tunaingia kesho yake saa 4:00
asubuhi ambayo kwa masaa ya America itakuwa
sijui muda gani uenda ikawa usiku.
Ayo yalikuwa ni maongezi yetu Mimi na Jofu wangu,
Mimi nilianza kusinzia baada yakuluka toka Turkish
wakati Jofu yeye alikuwa kavaa headphones
anaendelea kusikiliza wimbo wa Fanuel Sedekia
Manukato.
Nikawa namsikia akijaribu kuigizia kuuimba uo
wimbo, ikabidi nimwambie;
"Jofu una sauti nzuri na yenye kuvutia, yavaa uanze
kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji tukifika
huko Canada.!!"
"Nashukuru kwa ushuuda wako, itabidi nifanye
mazoezi sana maana uimbaji sio kazi ndogo."
"Ni kweli, ila ukimshirikisha Mungu utaweza na
itakuwa kazi lahisi sana.!"
Basi safari ikaendelea huku ma afisa wa ndege
wakipita huku na huko wakijaribu kuangalia usalama
wa abiria wao. Yeye Jofu alikuwa busy tu na kuigizia
uo wimbo, msikie kidogo;
Verse: 1.
Umeweka wimbo, kinywani mwaangu,
Bwana uliniumba, ili nikwabuudu
Nakuabudu nakuabuduu..
******
Chorus: ×2
Wewe uketiye juuu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato,
***
Weeweeee, wewe uketiye juu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato.
Verse: 2.
Wewe ni Niko ambaye n iko,
Milele iliyopita, na milele ijayo,
Sioni chakukulisha moyo wakooo,
Badala yakukuabudu mtakatiiiifuu.
Chorus:
Wewe uketie juu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato.
Kama sadaka ya Aberi,
manukato.
Kama zaburi ya Daudi,
manukato.
Manukato, manukato, manukatoooh
Manukato
Aleluyaah Aleluyaah Aleluyaaaaah
Manukato
Nakuomba bwana wimbo huu, ukawee, manukato
Manukato, manukato, manukatooohh!
Manukato
Aleluyaah Aleluyaah Aleluyaaaaah
Manukato.
"Woow Jofu uyoo, akika lazima umwimbie Mungu
kabisa yani.!"
Nilimwambia Jofu baada yakumaliza kuimba uo
wimbo wa Fanuel Sedekia kama ulivyo, Jofu alikuwa
akitabasamu tu huku akinitazama.
Mwanzo nilipenda sana hii safari ya ndege lakini
tulipofika anga la juu zaidi nilianza kuogopa
japokuwa sio sana maana ata nikifa sawa tu Sababu
nipo na Yesu moyoni mwangu ivyo siogopi kifo,
maana kufa ni lazima nakuishi ni bahati.
"Mmh! Jofu kumbe America ni mbali ujue mpaka
numechoka kukaa yani.!"
Nilimwambia Jofu kisha akajibu;
"Pole Mama, subiri muhudumu akipita nimweleze ili
walau utembee tembee kidogo, sababu naona
system inaonyesha bado kuna miles kadhaa ndio
tufike Toronto..!!"
"Kwani Jofu, unajua umbali wa toka Dar mpaka
huko Toronto tuendako..?"
"Ndio najua, kwanini nisijue sasa wangu!?"
"Niambie basi na Mimi.!"
"Sawa, toka Dar Tanzania, mpaka Toronto Canada
kuna umbali wa 7,967miles ambazo ni sawa na
12,821Kilometers ni palefu sana.!"
"Mmh! Ongera yako bwana"
Basi baada ya mwendo mlefu na kmya kikuu
kuitawala ndege yote atimaye tuliamka wote na
taarifa ya kwanza kabisa alikuwa ni salam kisha
tukaambiwa tumefika nchini Canada ivyo tukae
tayari tufunge vyema mikanda yetu maana ndege
inaenda kutua sasa.
Baada ya ndege kutua tulitelemka huku
tukisalimiana hali ya hewa ilikuwa ni baridi sana,
nikatazama mbele ya jengo kubwa nikaona
maandishi Toronto Pearson International Airport.
Nikamuuliza Jofu kuwa kumbe bado kufika Canada
maana hapa ni Toronto, ila Jofu akcheka kisha
akasema hapana hapa ni Canada na huu mji wao au
Main City kama vile sisi kule Tanzania Dar, Arusha,
labda na Mbeya.
Tulifika salama kabisa nchini Canada na baada ya
mwezi mmoja tukiwa chini ya Pastor Stefansson
ambaye kwa hapa Canada waumini wamempa jina
la The Second Jesus (Yesu wa pili) jina ambalo
yeye ulikataa katu katu kabisa maana anaamini
kuwa Hakuna wakufanana na Yesu, hakuna
wakufanana naye..!!
Basi tulifunga ndoa na siku ya kwanza kufanya
mapenzi na Jofu yani toka nipone huwezi amini
kabisa maana nilijishangaa kuona kuwa nimerudi
kuwa bikra kabisa yani jamani kweli MUNGU
mkubwa aisee...mume wangu mwenyewe ambaye
ni Jofu alishangaa kabisa akabaki kaduwaa tu
baada yakuona damu kibao huku nyuzi nyuzi za uke
Wangu zikikatika yani inaonyesha ni bikra original
kabisa tena ambaye sijawahi ata kujiosha na vidole