Chochote kinachompotezea mtu muda huonekana kizuri.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,548
3,459
Katika zama ambazo kumeibuka vitu vingi vinavyoweza kumpatia mwanadamu uraibu wa kupoteza muda ni zama tunazoishi. Uzoefu wa kawaida wa maisha unaonesha mambo yanayopoteza muda wa watu kwa visingizio au sababu mbalimbali kuongezeka mara dufu Duniani.

Siyo jambo la ajabu leo kumkuta mtu anaangalia picha za ngono masaa matatu na ukimuuliza taratibu atakuambua anajisikia vizuri, ameshazoea hivyo au hawezi kuacha. Si hivyo tu karibu kila mtu leo ana jambo linalompotezea muda tu. Hapa ndipo inapokuja dhana ya kilevi siyo mvinyo au pombe tu kwa sababu leo karibu Kila kitu kinaweza kutumika kumpotezea mtu muda wake.

Tunaidhia Duniani mara moja tu na jambo la ajabu zaidi na kinaloumiza kulipokea ni ukweli kuwa muda wetu haurufi nyuma, unakwrnda mbele kwa kasi na hatari zaidi ni kuwa kasi hiyo ni kama inaongezwa au inawekewa vihatarishi zaidi kutokana na hatua za maendeleo ya kibinadamu.

Tatizo kubwa linalobainika ni kwamba pale mtu anaposhtuka kuwa amepoteza muda tayari anakuwa ameshachelewa. Kushtuka kwa mtu kuwa amespchelewa au amecheleweshwa huwa ni uhalisia uliochelewa "delayed reality". Baadhi ya sababu za kuchelewa ni:
  1. Upatikanaji wa Taarifa: Huenda taarifa au habari kuhusu jambo fulani zikawa hazipatikani kwa wakati au mtu akapata habari baadaye.
  2. Mabadiliko katika Muktadha: Muktadha au hali inaweza kubadilika, hivyo kufanya mtu afahamu jambo baadaye wakati hali zinabadilika.
  3. Ukosefu wa Uwezo wa Kutabiri: Wakati mwingine, haiwezekani kutabiri au kufahamu mambo mapema kutokana na ukosefu wa habari au muktadha muhimu.
  4. Kuwepo kwa Vipingamizi: Vipingamizi vya kibinafsi au kimazingira vinaweza kuzuia mtu kufahamu mambo mapema.
  5. Kuchelewa kwa Habari: Kuna nyakati ambapo taarifa husambaa au kufikia mtu baada ya muda fulani, hivyo kuchelewesha ufahamu wake.
  6. Ukosefu wa Ushirikishwaji: Kutohusishwa katika mchakato au kutengwa kunaweza kusababisha kuchelewesha kwa ufahamu wa mtu kuhusu jambo.
Mambo yanayomchelewesha mtu aghalabu humpa mtu ukanda wa kujifariji "comfort zone". Kuishi siyo kujifariji kwa sababu maisha ni halisi. Kujifariji ni sawa na kutumia dawa za kumtuliza tu maumivu na si kuondoa maumivu. Vitu vinavyochelewesha huweza kumfanya mtu kuigiza kuishi badala ya kuishi.

Uhitaji mkubwa unaozaa umasikini wa mtu ni zao la upotevu unganifu wa muda "cumulative loss of time". Ikiwa Wazazi walipoteza muda ni dhahiri upotevu huo utabebwa na vizazi vyao halikadhalika vizazi vikipoteza muda upotevu huo ndiyo ninaouita upotevu unganifu "cumulative loss of time".

Nimeupokea kwa uchungu ukweli huu uliotamkwa na Kiongozi mmoja hapa nchini kuwa Taifa letu lipo nyuma miaka tisini (90) ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea. Ukweli huu umenifanya nione athari za upotevu unganifu wa muda siyo tu kwa Taifa langu ila pia jamii, familia na mimi binafsi.
 
Back
Top Bottom