Chitanda ajiunga na CCM

Chitanda ajiunga na CCM

Huwezi kufanya kazi ya CCM Ukajiita Chadema tukuache-Tundu Lissu.Wamerudi nyumbani walipotoka, kazi waliyotumwa imewashinda waende wapi?
 
[h=2] Swahiba wa Zitto atimkia CCM [/h] Wednesday, January 22 2014, 7 : 59
[h=1]ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi ambaye hivi karibuni alitangaza kuachia wadhifa huo, Ali Chitanda, ametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alifikia uamuzi huo juzi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za udiwani wa Kata ya Namikango, Wilaya ya Nachingwea.
Alisema licha ya kuamua kuhamia CCM, pia aliahidi kukifanyia chama hicho kampeni katika mikutano yake yote itakayoifanya wakati wa kampeni iliyoizindua hadi atakapohakikisha kiti hicho cha udiwani kinarejea CCM.
"Nimekuwa kwenye vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini tatizo la CHADEMA kinaendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi inayojali masilahi ya viongozi wachache, hivyo ndugu zangu wananchi naomba msikiunge mkono chama ambacho hakifuati masilahi ya watu hasa maskini,” alisema Chitanda.
Akizungumza baada ya kutambulishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe, Chitanda aliwataka vijana wanaokimbilia CHADEMA kuanza kujiuliza kabla ya kufikia uamuzi wa kujiunga na chama hicho.
"Chama hicho kimepoteza mwelekeo kutokana na viongozi wachache kukifanya chama hicho kuwa ni taasisi binafsi," alisema amekitumikia kwa miaka 10, sasa ameamua kuondoka.
Aliongeza kuwa; “Kati ya watu ambao wamekaa muda mrefu na kushika nyadhifa mbalimbali kwenye vyama mbalimbali vya upinzani kuanzia NCCR-Mageuzi hadi CHADEMA, nimeamua kuachana na vyama hivyo baada ya kubaini kuwa ni mali ya wachache kwa masilahi yao.”
Kauli hiyo ya Chitanda iliungwa mkono na Akwilolmbe ambaye kabla ya kurejea CCM aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF na baadaye kuwa pia Naibu katibu mkuu wa CHADEMA na kuamua kuachana na vyama hivyo kwa kile alichosema kuchoshwa na vitendo vya ubinafsi. Chitanda inadaiwa alikuwa mmoja wa marafiki wa karibu wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Zitto Kabwe, ambaye hivi karibuni alivuliwa wadhifa huo.
Chitanda alitangaza kujiuzulu wadhifa wake mkoani Lindi siku chache mara baada ya Zitto, kuvuliwa wadhifa wake kutokana na kudaiwa kufanya uasi ndani ya chama hicho.[/h]

habari za kitaifa › majira



[h=3]

[/h]
 
Hiyo shule yenu kiboko yaani mlikuwa mnalishwa kiapo kila wiki!shule ya msingi nimeanza wakati wa utawala wa Rais Nyerere na kumaliza wakati wa Utawala wa Rais Mwinyi sijawahi kushuhudia kitu kama hicho labda mlikuwa mnakula viapo shuleni kwenu tu.

Kwa posti yako tu unaonyesha ni dogo uliyesoma zama za waziri Mungai+Kawambwa ambapo kila shule kinatumia kitabu chake zama hizo lililoanyika mtwara ndilo lillokua Mwanza.......!
 
Huyu chitanda alikuwa ni panya aliyekuwa akiishi nyumbani kwa binadamu wakati makazi yake halisi ni vichakani au kwenye mashina ya katani...Mla rushwa yeyote hawezi kukaa CDM Labda kama atakuwa amekuja kutarii tu.

Ameona awahi mapema asije akagundulika kuwa alikuwa ni miongoni mwa-waliokuwa wanavuta mlungula toka kwa mbunge wa mahakama! Aende anafikiri JK atamchagua kwenye u-DC?
 
maneno ya mkosaji hayo mbona hukusema wakati ukiwa ndani ya cdm. wewe uliamua kuchukua hela basi kaa kimya wacha kutokwa povu haikusaidii njaa imekuponza.
 
Chitanda yuko sahihi kabisa tena ameona mbali,tatizo kubwa la upinzani hasa CDM viongozi wameonesha unafiki mapema sana,ZZK amefumbua macho ya wengi.Wengi wa waliokua wanachama wa chadema ikiwemo na mimi mwenyewe eidha wamekihama chama nakuhamia vyama vingine au wamebaki kua raia wakawaida bila kushiriki siasa
 
Ni sawa, ana uhuru wa kufanya hivyo, anaweza kutumia sababu yoyote, lakini ni nani mwenye maslahi binafsi. Vizuri, labda huko atafanikiwa.
 
Chitanda yuko sahihi kabisa tena ameona mbali,tatizo kubwa la upinzani hasa CDM viongozi wameonesha unafiki mapema sana,ZZK amefumbua macho ya wengi.Wengi wa waliokua wanachama wa chadema ikiwemo na mimi mwenyewe eidha wamekihama chama nakuhamia vyama vingine au wamebaki kua raia wakawaida bila kushiriki siasa

m4c pamoja daima ndiyo habari ya watz wazalendo kwa sasa!!!!
 
Acha hizo Lua, mbona hata hao wenye makengeza walimuona na kukubali? Kumbuka Muasisi wa SACCOS (makengeza), Mzee wa kuutupa Dubai Makengeza. Chitanda ni Jembe.
 
Back
Top Bottom