China yashinda shambulio la kimtandao la Marekani dhidi ya “Saa za Beijing”

China yashinda shambulio la kimtandao la Marekani dhidi ya “Saa za Beijing”

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
169
Reaction score
287
VCG111598777908.jpg
Mamlaka ya usalama wa taifa la China hivi karibuni ilifanikiwa kuzima jaribio la kushambulia Taasisi ya Huduma ya Wakati ya China. Kulingana na matokeo ya uchunguzi yaliyotangazwa, shambulio hilo lililotoka kwa Shirika la Usalama la Kitaifa la Marekani (NSA), lilimekuwa likilenga miundombinu muhimu ya China ya kutoa huduma za “Saa za Beijing”.

Taasisi ya Huduma ya Wakati ya China iliyoko Xi'an, mkoani Shaanxi, inatoa huduma za saa zenye usahihi wa hali ya juu kwa sekta muhimu zikiwemo mawasiliano, fedha, umeme, uchukuzi na ulinzi wa taifa. Ikiwa mfumo muhimu ya kimiundombinu, huduma za taasisi hiyo zikikwama, zitasababisha athari mfululizo, kama vile kukatika kwa mawasiliano, kukatika kwa mfumo wa fedha, kukatika kwa umeme na kukatizwa kwa usafiri. Lengo kuu la washambuliaji lilikuwa kulipua “mabomu ya mtandao” kwa mbali katika wakati maalum, ili kuleta vuguru kubwa nchini China.

Shambulio hilo la kimtandao kwa mara nyingine tena limefichua mkakati wa kimwamba wa mtandao unaotekelezwa kwa muda mrefu na NSA na Cyber Command ya Marekani. Mwaka 2017, Marekani iliinua hadhi ya Cyber Command kuwa Makao Mkuu ya 10 ya Kivita, na kuorodhesha wazi miundombinu muhimu ya nchi nyingine katika malengo ya kushambulia.

Lakini kabla ya hapo, China na Marekani zilihimniza kwa pamoja kuanzisha Kanuni ya Mtandao, na kuunga mkono makubaliano yaliyofikiwa na wataalam wa Umoja wa Mataifa kwamba, nchi yoyote haiwezi kuchukulia miundombinu ya nchi nyingine kama lengo la mashambulizi ya kimtandao. Pia viongozi wa nchi hizo mbili waliahidi kutoshambulia miundombinu ya nchi nyingine kwa njia ya kimtandao. Hata hivyo, Marekani sasa imekiuka ahadi yake na kushambulia miundombinu muhimu ya China.

Wakati Marekani inapofanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kimtandao dhidi ya nchi mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na China, inaendelea kueneza uongo wa “tishio la China”, na kupaka matope China kwa kusema inafanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya nchi nyingine, na hata kuwekea vizuizi makampuni ya China kwa kisingizio cha kufanya mashambulizi ya kitandao.

China kufanikiwa kuzuia shambulio la kimtandao la Marekani kunadhihirisha kwa jamii ya kimataifa nia yake na uwezo wake wa kulinda usalama wa kimtandao. Kama nchi kubwa ya kimtandao yenye uwezo na ya kuwajibika, China siku zote inatetea kutumia mtandao kwa njia ya amani, na kupinga aina zote za mashambulizi ya kimtandao. China inaona kuwa kujenga mtandao wenye amani, usalama, uwazi na ushirikiano, kunafuata maslahi ya nchi zote dunian
 
Back
Top Bottom