China yapinga vikali mauzo ya silaha za Marekani kwa Taiwan

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,418
9,599
a670fd1b4ede7fa02a23f0e4b80a01e1.jpg

Siku ya alhamisi utawala wa bwana Trump kwa Mara ya kwanza tangu uingie madarakani umeidhinisha mauzo ya silaha kwa Taiwan zenye thamani ya dola bilion 1.42 ($1.42 billion).
Hatua hiyo imepingwa vikali na China ambayo inaichukulia Taiwan kama sehemu yake.Siku ya ijumaa msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lu Kang alisema kwamba kwa mauzo ya silaha kwa Taiwan, Marekani imekiuka haki zake kimataifa. Lakini Marekani yenyewe imejitetea kwamba mauzo hayo ya silaha kwa Taiwan ni kwa ajili ya kujilinda yenyewe.

428427c51f31119208bc17b997e5ad82.jpg

Mauzo ya silaha hizo yanajumuisha makombora ya kuharibu rada/mizinga ya kutungulia ndege (anti-radiation missiles), baadhi ya vifaa kwa ajili ya mfumo wa kulinda anga wa SM-2 (SM-2 missiles), makombora ya kurushwa toka angani na kushambulia ardhini (air to ground missiles) ,silaha za kushambulia meli na nyambizi (torpedoes) pamoja na msaada kwa ajili ya early warning radars.
 
Ndo maana nasema siku zote hawa China warembo tu hawana ishu yyte.
Wanabwekabweka km vitoto vya kike no action .

Hapo cha msingi ingiza jeshi , pondaponda wote wanaozingia then unaitanfazia dunia Taiwan ni sehemu ya China , full stop.
 
Mh!, kunani m US na haya mauzo ya silaha? Juzi kazimwaga M. East.

Za business man in da white houz!
Aiseee yani mwaka huu (mwaka wa 1 wa Trump) Marekani imeuza silaha nying saanaa kupita miaka 8 ya Obama... Kwanza ni Saudia Dola billion 110
Pili Qatar Dola billion 12
Tatu India juzi hapa Dola billion 2+ km sikosei
Nne Taiwan Dola billion 1.42
Nyinginezo.....kweli Trump ni mfanyabiashara
 
Aiseee yani mwaka huu (mwaka wa 1 wa Trump) Marekani imeuza silaha nying saanaa kupita miaka 8 ya Obama... Kwanza ni Saudia Dola billion 110
Pili Qatar Dola billion 12
Tatu India juzi hapa Dola billion 1.5+ km sikosei
Nne Taiwan Dola billion 1.42
Nyinginezo.....kweli Trump ni mfanyabiashara

Na India ndani?!
Tehe!, Pakistan hajalalamika kama hawa wengine?

Trump mwisho lakini amempita mpaka Obama halafu unajua hana mwaka bado ndani ya nyumba.
 
sasa mkuu ulitaka China afanyaje
Inachotakiwa kukifanya China ni kuwatia adabu km si kuwapondaponda viongozi wate wa Taiwan wanaojifanya vichwa ngumu.

Baada ya kuwasagasaga then unautaarifu ulimwengu kuwa kwanzia sasa Taiwan ni moja ya mikoa ya China . mbona walimwengu tutakuelewa tu.

Nashangaa wanaleta ngonjera za kike .

Muige mrusi alivyofanya pale Crimea .
 
Ndo maana nasema siku zote hawa China warembo tu hawana ishu yyte.
Wanabwekabweka km vitoto vya kike no action .

Hapo cha msingi ingiza jeshi , pondaponda wote wanaozingia then unaitanfazia dunia Taiwan ni sehemu ya China , full stop.
Au hawakumuona mrusi alichofanya pale Ukraine!?

China anatuaibisha bhana.

Hahah!, eti anatuaibisha. Unapenda ugomvi Nyamai..
 
Na India ndani?!
Tehe!, Pakistan hajalalamika kama hawa wengine?

Trump mwisho lakini amempita mpaka Obama halafu unajua hana mwaka bado ndani ya nyumba.
Yah juzi hapa Yule PM wa India alkua Washington, wakaweka saini mkataba wa mauzo ya drones 22 aina ya Predator kwa India. Dili thamani yake no $ 2-3 billion.

f90dab5ba0dfcb621df4358ebcb3aa22.jpg
Predator drone
 
Aiseee yani mwaka huu (mwaka wa 1 wa Trump) Marekani imeuza silaha nying saanaa kupita miaka 8 ya Obama... Kwanza ni Saudia Dola billion 110
Pili Qatar Dola billion 12
Tatu India juzi hapa Dola billion 2+ km sikosei
Nne Taiwan Dola billion 1.42
Nyinginezo.....kweli Trump ni mfanyabiashara
Hata sisi tunajivunia kuwa na rais Mwalimu.
sasa hivi watoto wote wanakaa kwenye madawati, walimu wamejaa mashuleni yaani hali niz nzuri sana.
 
Inachotakiwa kukifanya China ni kuwatia adabu km si kuwapondaponda viongozi wate wa Taiwan wanaojifanya vichwa ngumu.

Baada ya kuwasagasaga then unautaarifu ulimwengu kuwa kwanzia sasa Taiwan ni moja ya mikoa ya China . mbona walimwengu tutakuelewa tu.

Nashangaa wanaleta ngonjera za kike .

Muige mrusi alivyofanya pale Crimea .
Waige Tanganyika alichofanya kule visiwani
pemba na unguja
 
Yah juzi hapa Yule PM wa India alkua Washington, wakaweka saini mkataba wa mauzo ya drones 22 aina ya Predator kwa India. Dili thamani yake no $ 2-3 billion.

f90dab5ba0dfcb621df4358ebcb3aa22.jpg
Predator drone

Kweli mtafutaji. Mpaka mtu unashangaa kama vile kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Back
Top Bottom