ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
Siku ya alhamisi utawala wa bwana Trump kwa Mara ya kwanza tangu uingie madarakani umeidhinisha mauzo ya silaha kwa Taiwan zenye thamani ya dola bilion 1.42 ($1.42 billion).
Hatua hiyo imepingwa vikali na China ambayo inaichukulia Taiwan kama sehemu yake.Siku ya ijumaa msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lu Kang alisema kwamba kwa mauzo ya silaha kwa Taiwan, Marekani imekiuka haki zake kimataifa. Lakini Marekani yenyewe imejitetea kwamba mauzo hayo ya silaha kwa Taiwan ni kwa ajili ya kujilinda yenyewe.
Mauzo ya silaha hizo yanajumuisha makombora ya kuharibu rada/mizinga ya kutungulia ndege (anti-radiation missiles), baadhi ya vifaa kwa ajili ya mfumo wa kulinda anga wa SM-2 (SM-2 missiles), makombora ya kurushwa toka angani na kushambulia ardhini (air to ground missiles) ,silaha za kushambulia meli na nyambizi (torpedoes) pamoja na msaada kwa ajili ya early warning radars.