China yahusishwa kuchochea ujangili mbugani Tanzania

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, 10 October 2012 21:57

Mwandishi Wetu

BAADHI ya mataifa ya Mashariki ya mbali ikiwamo China yamedaiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa vitendo vya ujangili katika mbuga za wanyama nchini kutokana na nchi hizo kuruhusu biashara ya pembe za ndovu.

Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa mbali na China mataifa mengine ni yanayochochea biashara ya pembe ni Hong Kong, Japan na Korea Kusini.

Mbali na kuwapo kwa hali hiyo, Serikali imesema pi inafahamu mtandao wa kimataifa unaolizalisha silaha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kijangili kwenye mbuga za wanyama nchini.

Nyalandu alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi wa hahari jijini Dar es Salaam kuzungumzia pamoja na mambo mengine, kongamano la utalii linalotarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Arusha.

"Sisi tumefanya mapitio tukabaini vyanzo vya tatizo hili…tumegundua wateja wengi wa meno ya tembo wanatoka China.
"Kila msichana nchini China anavaa cheni iliyotengenezwa kwa meno ya tembo na matokeo yake, imepandisha gharama ya kilo moja ya meno hayo kutoka Dola 100 hadi Dola 1,000, hivi vyote ni vichochezi," alisema na kuongeza:

"Hebu fikiria, China yenyewe ina watu zaidi ya bilioni 1, sasa jumlisha na wateja wengine kutoka Japan, Korea Kusini, Hong Kong na nchi zingine za Mashariki ya mbali."

Kutokana na ukubwa wa tatizo nilo, Nyalandu alisema Serikali imeuomba upya Umoja wa Mataifa kuuza akiba yake ya meno ya tembo yaliyotaifishwa ili kupata fedha za kuimarisha ulinzi kwa lengo la kumaliza tatizo hilo la ujangili.

"Tukifanikiwa azma hiyo tutahitaji kupata ushirikiano wa karibu toka Jumuiya za Kimataifa wakiwamo polisi wa kimataifa ‘interpol' na nchi wahisani ili kukamata bidhaa zake yakiwamo meno ya tembo yaliyosafirishwa kimagendo," alisema.

Nyalandu alisema kuwa vitendo vya ujangili vinaendelea kuwa tishio kwa
mali asili ya taifa hivyo kunahitajika mkakati wa kukabiliana nao.

Naibu Waziri Nyalandu alikiri ugumu uliopo wa kukabiliana na wimbi la vitendo vya kijangili ambao alisema unaziandama karibu nchi nyingi za Afrika, lakini alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuusambaratisha mtandao huo kwa vile wahusika wake tayari wanatambulika.

" Serikali inafahamu mitandao yote inayojihusisha na biashara haramu ya ujangili. Tunawafahamu wale wanatumika kuingiza silaha nchini na kufanya uhalifu.

Lakini pia tunafahamu nchi duniani ambako meno haya ya tembo yanaenda na jinsi gani yanaenda na tumeiomba dunia tushirikiane katika hili," alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema kuwa tatizo la ujangili wa meno ya tembo haliwezi kukabiliwa na nchi moja kwani limechukua sura ya kimataifa hivyo ni wajibu wa kila nchi kushirikiana na taifa lingine kufifisha hujuma zinazoendeshwa na mitandao hiyo.

"Nenda Kenya hali ni ile ile, sasa sisi tunasema kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko tayari kukabiliana na ujangili huu na tunaomba wenzetu pia tushirikiane," alisisitiza Nyalandu.

Naibu Waziri Nyalandu alisema kuwa mkutano wa kimataifa uliofanyika huko Doha chini ya mwamvuli wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii (UNTO) ulizima jaribio la Tanzania kuuza meno hayo ya tembo, lakini sasa Serikali inakusudia kutumia kikao kijacho kitakachofanyika Bangkok kupenyeza ushawishi wake ili iruhusiwe kuuza meno hayo.

Wakati huohuo Wizara ya Mali ya asili na Utalii itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 15 mwaka huu.

Kongamano hilo ambalo litahusu usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi ya taifa na linatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 412 kutoka mataifa 40 ya Afrika.

THURSDAY, OCTOBER 11, 2012
MINISTER KAGASHEKI IN USA

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki meets Mr. Dan Ashe, the Director of US Fish and Wildlife Service in Washington DC.

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki addressing the Business and International Conservationists in a Lunch Meeting organized to him by the National Fish and Wildlife Foundation whereby he had an opportunity to present various conservation challenges in the country and the way forward.

Tanzanian delegation led by the Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (third left) and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli (third right) in a group picture with Lila Helms (fourth left) who is a Professional Staff Member of the US Senate Committee on Appropriations at US Senate Capitol Hill.

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (fifth right) leading a Tanzanian delegation in a discussion with the US Deputy Secretary, Department of the Interior Mr. David Hayes (in the middle) and his delegation (seating on the left). A delegation from Tanzania includes (right-left) Suleiman Saleh, official with the Tanzanian Embassy in Washington, Director General of Tanzania Wildlife Research Institute Dr. Simon Mduma, Acting Director of Wildlife Paul Sarakikya and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli.

THURSDAY, OCTOBER 11, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG

Wameenda USA kuomba MSAADA wa kuokoa PEMBE ZA NDOVU ???
Ziko NYINGI PIA Tanzania wanataka kuziuza na kuna WORLD BAN... Wachina Wanatumaliza kimya kimya...
 
jana waganda pia walikuwa wanalalamika tembo wanauliwa sana na wanasema kuna wachina wengi wanaousika na hiyo biashara ya pembe za ndovu,na wakaonyesha tembo wengi waliouawa,uganda wanasema wana tembo 5,000 na wachina wameingia kwa kasi kufanya ujangili
 
Wednesday, 10 October 2012 21:57

Mwandishi Wetu

BAADHI ya mataifa ya Mashariki ya mbali ikiwamo China yamedaiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa vitendo vya ujangili katika mbuga za wanyama nchini kutokana na nchi hizo kuruhusu biashara ya pembe za ndovu.

Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa mbali na China mataifa mengine ni yanayochochea biashara ya pembe ni Hong Kong, Japan na Korea Kusini.

Mbali na kuwapo kwa hali hiyo, Serikali imesema pi inafahamu mtandao wa kimataifa unaolizalisha silaha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kijangili kwenye mbuga za wanyama nchini.

Nyalandu alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi wa hahari jijini Dar es Salaam kuzungumzia pamoja na mambo mengine, kongamano la utalii linalotarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Arusha.

"Sisi tumefanya mapitio tukabaini vyanzo vya tatizo hili…tumegundua wateja wengi wa meno ya tembo wanatoka China.
“Kila msichana nchini China anavaa cheni iliyotengenezwa kwa meno ya tembo na matokeo yake, imepandisha gharama ya kilo moja ya meno hayo kutoka Dola 100 hadi Dola 1,000, hivi vyote ni vichochezi," alisema na kuongeza:

"Hebu fikiria, China yenyewe ina watu zaidi ya bilioni 1, sasa jumlisha na wateja wengine kutoka Japan, Korea Kusini, Hong Kong na nchi zingine za Mashariki ya mbali."

Kutokana na ukubwa wa tatizo nilo, Nyalandu alisema Serikali imeuomba upya Umoja wa Mataifa kuuza akiba yake ya meno ya tembo yaliyotaifishwa ili kupata fedha za kuimarisha ulinzi kwa lengo la kumaliza tatizo hilo la ujangili.

"Tukifanikiwa azma hiyo tutahitaji kupata ushirikiano wa karibu toka Jumuiya za Kimataifa wakiwamo polisi wa kimataifa ‘interpol’ na nchi wahisani ili kukamata bidhaa zake yakiwamo meno ya tembo yaliyosafirishwa kimagendo," alisema.

Nyalandu alisema kuwa vitendo vya ujangili vinaendelea kuwa tishio kwa
mali asili ya taifa hivyo kunahitajika mkakati wa kukabiliana nao.

Naibu Waziri Nyalandu alikiri ugumu uliopo wa kukabiliana na wimbi la vitendo vya kijangili ambao alisema unaziandama karibu nchi nyingi za Afrika, lakini alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuusambaratisha mtandao huo kwa vile wahusika wake tayari wanatambulika.

“ Serikali inafahamu mitandao yote inayojihusisha na biashara haramu ya ujangili. Tunawafahamu wale wanatumika kuingiza silaha nchini na kufanya uhalifu.

Lakini pia tunafahamu nchi duniani ambako meno haya ya tembo yanaenda na jinsi gani yanaenda na tumeiomba dunia tushirikiane katika hili,” alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema kuwa tatizo la ujangili wa meno ya tembo haliwezi kukabiliwa na nchi moja kwani limechukua sura ya kimataifa hivyo ni wajibu wa kila nchi kushirikiana na taifa lingine kufifisha hujuma zinazoendeshwa na mitandao hiyo.

“Nenda Kenya hali ni ile ile, sasa sisi tunasema kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko tayari kukabiliana na ujangili huu na tunaomba wenzetu pia tushirikiane,” alisisitiza Nyalandu.

Naibu Waziri Nyalandu alisema kuwa mkutano wa kimataifa uliofanyika huko Doha chini ya mwamvuli wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii (UNTO) ulizima jaribio la Tanzania kuuza meno hayo ya tembo, lakini sasa Serikali inakusudia kutumia kikao kijacho kitakachofanyika Bangkok kupenyeza ushawishi wake ili iruhusiwe kuuza meno hayo.

Wakati huohuo Wizara ya Mali ya asili na Utalii itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 15 mwaka huu.

Kongamano hilo ambalo litahusu usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi ya taifa na linatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 412 kutoka mataifa 40 ya Afrika.

THURSDAY, OCTOBER 11, 2012
MINISTER KAGASHEKI IN USA

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki meets Mr. Dan Ashe, the Director of US Fish and Wildlife Service in Washington DC.

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki addressing the Business and International Conservationists in a Lunch Meeting organized to him by the National Fish and Wildlife Foundation whereby he had an opportunity to present various conservation challenges in the country and the way forward.

Tanzanian delegation led by the Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (third left) and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli (third right) in a group picture with Lila Helms (fourth left) who is a Professional Staff Member of the US Senate Committee on Appropriations at US Senate Capitol Hill.

Minister for Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki (fifth right) leading a Tanzanian delegation in a discussion with the US Deputy Secretary, Department of the Interior Mr. David Hayes (in the middle) and his delegation (seating on the left). A delegation from Tanzania includes (right-left) Suleiman Saleh, official with the Tanzanian Embassy in Washington, Director General of Tanzania Wildlife Research Institute Dr. Simon Mduma, Acting Director of Wildlife Paul Sarakikya and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli.

THURSDAY, OCTOBER 11, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG

SI ndio mnawaita comrades.Sasa ngoja wawapin down muone jinsi watakuwa wakiwaua wote wanaotaka ondoa utawala wao.
 
Gazeti la Dailynews limesema Wameenda kuomba Msaada huko; naona yule BEPARI mwenye zile hoteli kwenye MBUGA kawalazimisha, na unajua anawajengea serikali Uwanja wa NDEGE wa KIMATAIFA...

Sasa tutaona ipi ina NGUVU.... TAZARA AU ... INTERNATIONAL AIRPORT
 
mimi kama mhifadhi siungi mkono kuuzwa meno ya tembo.....

Tunayo MENGI KWELI; Hizo Dolla zingesaidia VIONGOZI wetu wazidi KUKATA MBUGA za KUSAFIRI zaidi NJE ya NCHI... Kuliko kuyachoma kama International Law Inavyotaka...
 
Ubaya hatujakutana na ANY CONGRESS MEMBERS; from either side either HOUSE; Hata Any Secretary anayehusika na WILDLIFE ni VIWATU wa CHINI CHINI TU; Wakati sisi tumetuma UJUMBE MZITO na labda tumeomba kwa MUDA MREFU HIYO PHOTO-UP...
 
Gazeti la Dailynews limesema Wameenda kuomba Msaada huko; naona yule BEPARI mwenye zile hoteli kwenye MBUGA kawalazimisha, na unajua anawajengea serikali Uwanja wa NDEGE wa KIMATAIFA...

Sasa tutaona ipi ina NGUVU.... TAZARA AU ... INTERNATIONAL AIRPORT

TAZARA YA NINI?Tukiomba tazara tutaishia hapo kwa faida ya mchina kwenda chukua shaba,pengine na Zambia ila tutalipa wote.Tukiomba Airport watajenga halafu pia kwa vile hawapo tayari iachia tazara wataijenga tuu kwa masharti yasiyotubana.Na masharti yakiwa mazuri tutakula faida kwa ushuru na kutumia kwa hivi vipande vilivyo ndani kwetu.

Kwa ujumla tumeingia katk mawimbi tukiwa na watu kama dhaifu lazima tupate kizunguzungu n amkorogo mkubwa tukija tua ktk mawimbi salama tunadaiwa sana na waliotuingiza katk mawimbi na wanaojaribu tutoakoa.
 
Ni nini hatima ya rasilima wanyama pori ikiwa idadi ya wanyama wanaouawa kwa siku moja tanzania ni 37 hususani tembo na faru
 
China thread bashing as usual...
Hawa wapuuzi tu,kama tatito lina-originate China kwanini wasiende huko badala yake wanaenda US (yaani wanataka kugombanisha the world's 1st and 2nd largest economies:becky:). Kwakweli serikali ya magamba ni janga kuu. Polisi wanatoroisha nyara za taifa, meli za katibu mkuu zinabeba na kutorosha nyara za taifa leo hii mnakimbilia nchi ya nje kwenda kuomba msaada jinsi ya kudhibiti.....
 
China ni janga nafikiri kwenye misitu pia huko hapatakuwa salama. Hawana standard zozote wachina. Wakuaribie nchi yako iwe jangwa, wamwage sumu hewani na kwenye mito utajiju. Yaani nchi zetu hizi kufanya biashara na wachina ni kujitakia matatizo kwa maisha ya vizazi vya hapo baadaye kwani ni kipofu mkubwa kuongoza kipofu mdogo. Wote hakuna wa kumsaidia mwenzake.
 
Viongozi wa tanzania wana-uchu na rushwa wanayopewa na wachina, hawaangalii tena masilahi ya nchi. Nakukumbuka dikteta Mobutu aliitimua kampuni moja(ya kigeni) ya ujenzi wa barabara ambayo ilijitolea kujenga barabara bure, kumbe maeneo waliochagua kujenga hizo barabara kulikuwa na madini mengi, kumbe jamaa walikuwa wanachimba mchanga wanausafirisha kwenda kwao, baada ya wananchi kushtuka Mobutu ilibidi awaamuru waondoke warudi kwao.
 
Back
Top Bottom