China waanza kuifunga WhatsApp

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427

​

CHINA: Mtandao wa WhatsApp umeingia kifungoni nchini China ukiifuatia na Instagram, Twitter, Facebook, Gmail, Snapchat na Pinterest.

WhatsApp imeanza kufungiwa taratibu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa taasisi inayoratibu masuala ya mitandao duniani, Open Observatory of Network Interference (OONI).

Mtandao wa Shirika la Utangazaji CNN unaripoti kuwa katika miezi ya hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikipatikana kwa shida.

Mtandao huo ulianza kufungiwa taratibu wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa chama tawala cha Communist, utakaoanza Oktoba 19 mwaka huu.

Kwa kawaida nchi hiyo hudhibiti matumizi ya mtandao katika kipindi cha uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

China inatumia mtindo wa Great Firewall katika kudhibiti matumizi ya intaneti ambayo hujumisha sera na teknolojia.

Chanzo: Mwananchi
 
Yaani ni balaaa litakuwa msiba Kila Kona ya inchi ,njaa si kitu kidogo
   
 
Mawazo potofu....DIKTETA UCHWARA NDO ANAWEZA KUFANYA HIVO. Upinzani walikuwa wanapata taarifa za ufisadi wa ccm toka 1995 kwa kutumia mitandao...KWA NCHI KM YETU INAYOONGOZWA NA WASHAMBA ITAKUWA HASARA KUFUNGIA MITANDAO NA HATUTAKUBALI
 
wanatumia WECHAT kwa sasa,kama unabishara nao download iyo appl
 
TCRA wanasubiri nini kuifungia whatsapp Tz?
Unataka watu stress zetu zikaishie wapi.....huko ktk mastatus ya whatsapp ndo kuna vita ya kila aina watu maugonvi yote tunahamishia kwenye status za whatsapp halafu ww unataka ifungiwe tutake radhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…