China na Urusi zalaani sera ya Nyuklia ya Marekani

China na Urusi zalaani sera ya Nyuklia ya Marekani

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
7,476
Reaction score
9,654
50c39d85bb017e02149d84293133a445.jpg

China imeelaani vikali na kuiomba Marekani iachane na fikra zake za Vita baridi baada ya Marekani kusema kwamba inataka kupanua mpango wake wa nyuklia kwa kuunda mabomu madogo ya Nyuklia.

b9a480faf39a98c3e14775e1550f116f.jpg

Marekani inasema kwamba silaha za nyuklia ilizonazo sasa zinaonekana ni kubwa sana kustahili kutumika na sasa inataka kutengeneza mabomu madogo. Urusi imelaani vikali mpango huo.
Silaha hizo ndogo hazina nguvu sana lakini zinaweza kusababisha madhara.

Sera hiyo pia inapendekeza kuunda makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kupenya kwenye ulinzi wowote wa anga,ukarabati wa nyambizi baadhi zikiwa na mabomu hayo madogo ya Nyuklia, kurudishwa kwa Meli zenye makombora ya Nyuklia, kuundwa kwa silaha zaidi ya kurushwa kwa njia ya anga.

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imeilaumu Marekani kwa kusambaza Vita na kusema kwamba itachukua hatua zipasazo kuhakikisha usalama wa Urusi huku waziri wake wa Mambo ya nje Sergei lavrov akitaja kusikitishwa pakubwa na mpango huo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran nae ameulaani mpango huo akiutaja kwamba unaipeleka Dunia kwenye maangamizi.

Marekani imezitaja Urusi,China,Iran na Korea kaskazini kama tishio kwake.

Tangu kwenye kampeni za Urais Trump aliahidi kuongeza nguvu za nyuklia za Marekani ambazo alisema kwamba uwezo wake ulikua umepungua na kuwapa faida washindani wake wakubwa China na Urusi.

US wants smaller nukes to counter Russia
 
THE STATUS-6 known as KANYON
Is a purported nuclear-powered and nuclear-armed unmanned underwater vehicle developed or being developed by the Russian Federation. It would supposedly be able to deliver a
thermonuclearcobalt bomb of up to 100
megatonnes against enemy's naval ports and coastal cities.
It is designed to create a tsunami wave up to 500 metres (1,600 ft) tall, which would radioactively contaminate a wide area on an enemy's coast with cobalt-60 , as well as being immune to anti-missile defense systems[/b] such as anti-ballistic missiles , laser weapons, and railguns that might disable an ICBM or a SLBM.
Hiki ndicho kinachomnyima USA raha RUSSIA anahisiwa katengeneza nyambizi drone ambayo ina kombora likifanikiwa fika kwenye ufukwe wako basi ile mbinu ya vita ya strike first utaishia kuisoma vitabuni!.
 
Huo mpango wa drone ya Russia USA ndo waliubumburua lakini Urusi mpaka leo bado hajakiri hadharani.
Unafahamu maana ya Nuclear Triad!?
Yaani ukiharibu hizo ports bado kuna ICBM,Kuna bombers na bila kusahau Submarines.

Marekani Wana nyambizi 16 za Ohio...Kila nyambizi moja inabeba makombora 24 ambapo kombora moja linabeba vichwa 8-12 vya Nuclear vyenye 475kiloton kila kimoja. Ndo maana wanasema hawawezi tumia silaha kama hizo [emoji115]maana ni maangamizi makubwa.

Na sera yao inasema lazima kuwe na nyambizi nne kila siku (24/7) ambazo zinakua mahali tofauti Duniani ili Kama wakishambuliwa ghafla nyumbani bhas zile nyambizi zinarudisha majibu,hivyo si rahisi kwa wao kushambuliwa bila kushambulia.
 
Kaamua kujifcha nyuma ya NK, Russia na China, yeye kama anaboresha aboreshe tu aache kelele, na wenzie wakija ku upgrade silaha zao asipige kelele tu.

Yeye anaboresha wakat huo huo anakataza adui zake wasiwe na Nuclear, unafikiri ukimwambia NK asitengenze Nuclear atakuelewa..? hahah

Wala uwezo wake ulikua haujapungua sema alizidiwa akili na Russia tu
 
Wao wanamiliki na wamataka kuziboresha alafu kiduku akimili inakua matatizo...
 
Huo mpango wa drone ya Russia USA ndo waliubumburua lakini Urusi mpaka leo bado hajakiri hadharani.
Unafahamu maana ya Nuclear Triad!?
Yaani ukiharibu hizo ports bado kuna ICBM,Kuna bombers na bila kusahau Submarines.
Russia either waliamua kwa makusudi kuionyesha dunia hiyo plan au bahati mbaya lakini marekani alikua anahisi tu maana picha za kwanza zilitoka Televisheni ya Russia na sio kwamba USA aliivumbua plan hiyo!.karudie source uone taarifa ilianzia wapi.
Marekani Wana nyambizi 16 za Ohio...Kila nyambizi moja inabeba makombora 24 ambapo kombora moja linabeba vichwa 8-12 vya Nuclear vyenye 475kiloton kila kimoja.
Naijua USA ana zana nyingi lakini hii KANYON ya mrusi ni drone submarine very small ina maana zikiwa mass produced halafu zinaelekezwa port zote za marekani nakwambia 100 megaton ya cobalt New York tutaisimulia vitabuni ndio maana hiyo silaha ni The last resort yani mrusi atakapoamua mbwai mbwai!.
Na sera yao inasema lazima kuwe na nyambizi nne ambazo zinakua mahali tofauti Duniani ili Kama wakishambuliwa ghafla nyumbani bhas zile nyambizi zinarudisha majibu,hivyo si rahisi kwa wao kushambuliwa bila kushambulia.
Kuna sera ya kivita inaitwa strike first/first strike atakayekuwa wa kwanza kushambulia ana chance kubwa ya kushinda vita thats y ili kuicounter hiyo doctrine USA na USSR walianzisha MAD policy!..
Pia Russia ana sera yake ya Dead man's hand/Fail safe yani leo ukiinuke moscow kuna sensors zipo zikinusa mabaki ya fall out nchi adui wote jiandaeni kwa mvua ya mabomu maana inajiactivate automatic
 
Russia either waliamua kwa makusudi kuionyesha dunia hiyo plan au bahati mbaya lakini marekani alikua anahisi tu maana picha za kwanza zilitoka Televisheni ya Russia na sio kwamba USA aliivumbua plan hiyo!.karudie source uone taarifa ilianzia wapi.
2a1d60bedddcc1ff8db2a7e2916a4648.jpg
397630cec2ebb3de9475cf37f6ac5e82.jpg

Naijua USA ana zana nyingi lakini hii KANYON ya mrusi ni drone submarine very small ina maana zikiwa mass produced halafu zinaelekezwa port zote za marekani nakwambia 100 megaton ya cobalt New York tutaisimulia vitabuni ndio maana hiyo silaha ni The last resort yani mrusi atakapoamua mbwai mbwai!.

Hiyo drone imeelezwa kwenye taarifa za Siri za Pentagon ambazo zilileak bahati mbaya,na hakuna mwenye uhakika Kama ni kweli au ni Marekani inatumia mwanya huo kuongeza silaha zake za nyuklia Kama anavyoitumia NK kuongeza masilaha yake makali pale kwenye Peninsula ya Korea.
Kuna sera ya kivita inaitwa strike first/first strike atakayekuwa wa kwanza kushambulia ana chance kubwa ya kushinda vita thats y ili kuicounter hiyo doctrine USA na USSR walianzisha MAD policy!..
Pia Russia ana sera yake ya Dead man's hand/Fail safe yani leo ukiinuke moscow kuna sensors zipo zikinusa mabaki ya fall out nchi adui wote jiandaeni kwa mvua ya mabomu maana inajiactivate automatic
First strike ni sera tu ambazo nchi imejiwekea nchi nyingine hawana mfano Israeli,hawasubiri kushambuliwa ndo washambulie Ila wao wanafanya pre-emptive strike...Kama nilivyokueleza huko juu kwamba ili kuhakikisha nchi inajibu mashambulizi ipasavyo waliamua kuanzisha kitu kinaitwa Nuclear Triad yaani ikitokea adui kashambulia ngome zote za ICBM bhas submarines ambazo zipo Baharini zitajibu mashambulizi au Ndege(bombers) ambazo zipo kambi mbalimbali duniani. Na ni nchi nchi 6 tu zenye hiyo ambayo Tunaita Nuclear Triad ambazo ni US,Russia,China,UK,France and India.
 
Russia either waliamua kwa makusudi kuionyesha dunia hiyo plan au bahati mbaya lakini marekani alikua anahisi tu maana picha za kwanza zilitoka Televisheni ya Russia na sio kwamba USA aliivumbua plan hiyo!.karudie source uone taarifa ilianzia wapi.

Naijua USA ana zana nyingi lakini hii KANYON ya mrusi ni drone submarine very small ina maana zikiwa mass produced halafu zinaelekezwa port zote za marekani nakwambia 100 megaton ya cobalt New York tutaisimulia vitabuni ndio maana hiyo silaha ni The last resort yani mrusi atakapoamua mbwai mbwai!.

Kuna sera ya kivita inaitwa strike first/first strike atakayekuwa wa kwanza kushambulia ana chance kubwa ya kushinda vita thats y ili kuicounter hiyo doctrine USA na USSR walianzisha MAD policy!..
Pia Russia ana sera yake ya Dead man's hand/Fail safe yani leo ukiinuke moscow kuna sensors zipo zikinusa mabaki ya fall out nchi adui wote jiandaeni kwa mvua ya mabomu maana inajiactivate automatic
Hyo dead Man hand ya Urusi mbona hata Marekani Wana kitu kama hicho kinaitwa AN/DRC-8 Emergency Rocket Communication(ERCS) System. Inafanya kazi kama huo mfumo wa Urusi.
 
Back
Top Bottom