China na bidhaa feki

matata200

Member
Apr 5, 2011
9
2
Nilikuwa naomba mawazo yenu. Linapokuja swala la bidhaa feki yaani (counterfeit goods), watu wengi tunanyooshea kidole China. Na hii imeharibu sana image ya China kwa kuharibu fikra za watu kwamba kila kitokacho China ni feki. Ukweli ni kwamba China inasupply ulimwengu mzima na kwa mjibu wa tafiti inaelekea wanatengeneza bidhaa zinazozidiana ubora. Zile za soko la Ulaya na Marekan bora zaidi na za nchi ya dunia ya tatu duni. Kwa Tanzania nini tunaweza kufanya kuepukana na tatizo hili kama walaji(consumers), na serikali ifanye nini. Kuna wadau huwa wanapendekeza kugomea bidhaa za China, hii inawezekana bila athari yoyote? Nawasilisha
 
mkuu

wenye matatizo ni sisi wenyewe .... kuna usemi unaosema cheap is expensive

ngoja nikwambie .... wafanya biashara wetu wanakwenda china na sample za bidhaa halafu wanataka watengenezewe kwa bei nafuu .... mchina haachi pesa nyuma anafyatua order kutokana na budget yako .... tatizo ni la consumers kutaka bidhaa za bei ya chini ....

hapo ndipo counterfeit products zinapozaliwa
 
Back
Top Bottom