China inaomboleza wahanga wa COVID-19 nchi nzima

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
China leo imefanya maombolezo ya nchi nzima kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona. Bendera za taifa zimepepea nusu mlingoti nchi nzima pamoja na kusitisha shughuli zote za burudani.

Siku hii ya maombolezo iliambatana na kuanza kwa sherehe za kila mwaka za kuwakumbuka mababu wa zamani nchini China.

Sherehe za leo zilianza kwa nchi kukaa kimya kwa muda wa dakika tatu, ili kuomboleza waliofariki, wakiwemo wafanyakazi wa afya waliokuwa mstari wa mbele na madaktari.

Magari, treni na meli zilipiga honi na sauti za ving'ora zilisikika hewani. Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine walitoa heshima zao za kimya mbele ya bendera ya taifa mjini Beijing.

Zaidi ya watu 3,000 China bara walifariki dunia kutokana na COVID-19.
 
Huu ugonjwa naona China tu ndio waliuwezea, kwa maana idadi ya waliokufa ni ndogo sana kwa idadi ya waliopona.

Nikiangalia nchi nyingine kama US, Ufaransa, Italy, Uingereza na Spain, naona kinyume sana. Wanaokufa ni kama nusu au theluthi ya waliopona hadi sasa.

Mpaka napata mashaka kuwa mtu akiupata, chance za kupona ni ndogo mno. Mungu atupitishe salama kwa kweli.
 
Safe journey 🙏 to our beloved deceased ones. These moments were so unexpected
 
Back
Top Bottom