beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Hayo yamezungumza na Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania Bw, Abass Irovya ambapo amesema mpaka sasa tayari wamekwisha kamatwa wahamiaji haramu 162 na watanzania 15 wanaowasaidia wahamiaji hao kuishi nchini.
Bw. Irovya amesema kuwa kati ya makosa waliyokuwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na kufanya kazi bila vibali maalum, wengine walikuwa wanaishi bila pasipoti za mataifa yao huku wengine wakiwa hawana shughuli maalumu wanazofanya nchini.
Aidha ameongeza kuwa kati ya watanzania hao 15 waliokamatwa ambao wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo la kuwasafirisha wahamiaji hao haramu, kuwahifadhi pamoja na kutumika kutengeza hati bandia za kwa ajili ya kuwapatia wageni pasipoti za Tanzania.
Chanzo: EATV