Chimbuko la Panya road & Vigodoro !!

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Kwema mazee?

Kama hujawahi kutembelea sehemu za uswahilini hasa mitaa ya Mabibo,Manzese na Kigogo jijini Dsm basi umepitwa na mambo mengi ya kufurahisha maishani! Ni sehemu zenye visa,vituko na mikasa ya kila aina. Ni sehemu zinazokaliwa na idadi kubwa ya walalahoi!

Kuna vilabu vya mataputapu na pombe haramu ya bongo, Huwezi kuvuka nyumba 5 bila kukutana na genge! Pia nyumba za kupanga za maeneo haya ni full vituko baina ya wapangaji wenyewe kwa wenyewe au na mwenye nyumba.. Je wajua kwamba sehemu za uswahilini Manzese,Kigogo na Mabibo ndio chimbuko la panya road na vigodoro?

Panya Road.
Hakuna ambaye hajawahi kuwasikia vijana wa panya road, ni vijana wanaofanya uhalifu mitaani kwa kutumia silaha za jadi km mapanga,visu,mondo,bisibisi n.k. Panya road wamejipatia umaarufu mkubwa hapa Tanzania kutokana na kulitetemesha jiji la Dar es salaam kwa matukio yao ya uhalifu. Panya road chimbuko lao ni uswahilini sehemu za Kigogo,Mabibo na Manzese kutokana na ugumu wa maisha!

Pindi wakivamia mtaa hutembeza kichapo cha nguvu na kupora nyumba kwa nyumba, duka kwa duka. Baada ya kuwa tishio kwa maisha ya watu Jeshi la Polisi lilianzisha operesheni ya kuwasafisha panya road na kufanikiwa. Salute kwenu mabalozi wetu (panya road) mmetutangaza sana watu wa Uswaz!!!


Kigodoro. Ngoma tamu ya kigodoro mayo imebamba sana na kwa kipindi kirefu. Watu wa uswahilini wanapenda starehe bwana si umeambiwa raha jipe mwenyewe!

Kigodoro pia imeasisiwa smaeneo ya Manzese, Mabibo na Kigogo... Usishangae hata Diamond katokea pande za Manzese Tandale!

Huku uswahilini kucheza kigodoro ndio mwake, kigodoro uendana pamoja na watu kunywa mataputapu, kupuliza fegi na bangi, kuibiana pamoja na kufanya uhalifu!

Kulikuwa na utaratibu wa kuweka mkesha kigodoro huku uswahilini mfano Mabibo kwa Bibi Cheche kila mwisho wa mwaka na watu kujiachia kwa raha zao!! Kamanda Kova aliamua kupiga marufuku kigodoro. Chezea watoto wa Uswazi wewe?
ee97e9c8696946b19e37e46129ca96d5.jpg
afe69c5549ea51b6fadccbdca3804e28.jpg
3584312b2a4416ff0c1fce33e29eb8bf.jpg


***Mtu kwao***

The Bitoz
 
Dah maeneo ya kigogo mburahat sitasau vibaka walivo Nikabaki na kusepa na begi mixer kunitia panga wenyewe wnkwmbia kumkata mtu ngozi ni kumtoa k*ma
Mtoa mada pia usisahau maeneo mengine yaliyochachawa ni kiwalani na vingunguti duuh jangwan nako kuna vichwa vibovu kama sio vilivopinda
 
Vigodoro si mchezo, maana nina music intertainment unaitwa kwa uwezo music nimeuweka hapa kigogo Luhanga, (mabibo matokeo) karibu na shule ya msingi kawawa, wakati ule kabla ya kupigwa marufuku Vigodoro ilikuwa full laana, naendaga tu madjs wakifunga music after that narudi home, maana
Haaa kumbe Team Kigogo mpo....umetisha
 
Dah maeneo ya kigogo mburahat sitasau vibaka walivo Nikabaki na kusepa na begi mixer kunitia panga wenyewe wnkwmbia kumkata mtu ngozi ni kumtoa k*ma
Mtoa mada pia usisahau maeneo mengine yaliyochachawa ni kiwalani na vingunguti duuh jangwan nako kuna vichwa vibovu kama sio vilivopinda
Mkuu Joto City kuna sehemu nyingi tu za Kiswaz lkn pande za Manzese, Kigogo na Mabibo ndo baba lao
 
Bitoz asante sana kwa hii post maisha ya wengi wetu yameanzia uswahili na mungu saidia tumekuja kuwa walezi bora wa familia zetu tukiwafundisha watoto wetu kwa mifano halisi ya maisha yetu ya nyuma
 
Back
Top Bottom