Chimbuko la MASAIBU yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chimbuko la MASAIBU yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msanii, Dec 20, 2009.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wanabodi, mtaniwia radhi kwa heading kali niliyotumia ila kwa mtazamo wangu ni kwamba sisi kama Taifa tumeikimbilia LAANA badala ya NEEMA kutokana na hulka yetu sisi WATANZANIA. Nikivuta kumbukumbu za malengo ya uhuru kwamba tuweze kujiongoza (kujitawala?), kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo (kuelekea mafanikio) yetu pia na kustawisha TAIFA lenye UTU, MSHIKAMANO, AMANI, UPENDO na kila jema. Lakini kabla ya kufikia hata nusu muongo (decade) tumekishwa fahamu jahazi linapoelekea, tena linaelekea katika pwani isiyo matarajio yetu na vizazi vijavyo. Kama hatutaamua sasa kwa ajili ya vitukuu vyetu basi watajikuta wanaishi mchangani na kujenga kwenye matope. Tumekiuka hata ile misingi tuliyowekewa na waasisi wa Taifa letu ambao walisukumwa na UZALENDO na si kwa KUKUBALIKA wala KUFAHAMIANA. Ole nasema Ole tena OLE iwe ole wajivuni ninyi.

  Viongozi wetu ambao hivi sasa wamegeuka kuwa watawala (directors and managers) wamekwishasahau wimbo wa UHURU ni Maendeleo, yaani pamoja na kwamba uhuru haukui ila uhuru unapaswa kuendelea kwani kukoma kwa uhuru ni kujiingiza chini ya nyapara la utumwa tena lisilo na huruma. Tumepoteza mavazi yetu mtoni (uozo) na sasa tunatembea utupu huku tukisifia mavazi ya kufikiria na dhahabu za madhania pamoja na vikuku alinacha. Furaha yeni ni kuwepo madarakani lakini nawaambia laana inawafuata huko huko hamtakuwa na amani mioyoni mwenu mpaka mwisho wa pumzi zenu, ndo maana mnatumia resources na gharama kubwa sana kujihalalishia kuwepo hapo mlipo. Endeleeni kuchuma kutoka kwa maskini na matajiri mkidhani mtasitirika. Pia endeleeni na huo mwendo wenu wa majibu ya KEJELI kwa masuala ya msingi. Nadhani hiyo ndo CODE of ethics mliyojiapiza kufa nayo kama tai shingoni.

  Twende kwenye hoja tuache hizo blah blah hapo juu ziwe kama porojo tu!

  Baada ya wavamizi (mataifa ya ulaya enzi za mapinduzi ya Viwanda) kugundua kwamba kuna bara lenye utajiri usiomithilika na watu wake wanaishi katika ustaarabu wa ushenzi (is that true?) waliamua kuelekeza macho yao kwa bara hili jeusi ili kuweza kujipatia mahitaji muhimu ya viwanda na ukuaji wa uchumi wao. Kabla ya kuligawa bara la Afrika 1884-1885 Berlin, tulikuwa tayari (sisi waafrika) chini ya HIMAYA yao kwa zaidi ya miaka 400. Kilichotuponza ni ukarimu wetu na bashasha zetu za kupenda ‘new friends' na kukirimu wageni (jambo jema hili). Tulipofungua malango yetu waliingia na kupitiliza hadi jikoni na kuanza kujipakulia wapendavyo na kwa ujazo wautakao wao. Wakati wanaligawa bara letu hawa wazungu walijua wazi kwamba hawa washenzi wa ushenzini lazma watajitawala. Hivyo wakatumia kila mbinu kuua na kupoteza mifumo ya tawala zetu za ushenzi (kwa mujibu wa wazungu) pia wakatufundisha kustaarabika (suti na tai) badala ya kuvaa enviro-friendly cloths za magome na animal hides. Wakatulazimisha tuamini kwamba tiba zetu za asili ni UCHAWI (hehe mpaka muarobaini? Walah), tukaaminishwa elimu yetu ni ya kishenzi hivyo wakatuletea mfumo (BORA) wa elimu kutoka kwao ambapo tulipaswa kusoma mitaala ambayo chimbuko lake ni wao wenyewe. Tunasoma bila kujua kwamba tunazama kwenye tafakuri za mtu au watu maalumu waliowateua wao kwamba ndiyo baba wa taaluma Fulani hivyo wameua uwezo wetu wa uvumbuzi na utafiti. Quotes maarufu ni za kwao na watazichukua quotes zetu pale tu zinapoendana na ustaarab wao. Hivyo waliweka mfumo ambao hata tukijiongoza/jitawala wataendela kupata walichokitaka kutoka kwetu (malighafi na nguvukazi). Hatuna CHETU wanachojivunia lakini wametuloga sisi ambapo tunavutiwa 90% ya mazagazaga yao.Hivi juzi tumepata first born wetu nyumbani kwangu ambapo ugomvi mkubwa na shemeji yenu ni kwamba anataka mtoto aitwe jina linaloweza kutamkika (Mramba na ideology zake za Uwanja wa ndege wa Nyerere). Eti tukimwita motto Nyarugusu ataonekana kama mchuuzi wa samaki na watamtania, tukimwita Fahari anasema atakuwa mswahili sana….. gadem! Hivyo hata majina yetu hayafui dafu mbele ya ustaarab wa wazungu. Naomba nisiwachoshe sana na insha, ila naomba uchukue muda utafakari haya niliyosema hapo juu yanahusiana vipi na hali halisi tuliyonayo?? Najua wengi wenu mmesoma kitabu cha Animal Farm au Shamba la Wanyama Ibura. Nguruwe walibadilisha wimbo uliokuwa unasema miguu mine ni bora, miguu miwili ni mibaya, wakaongeza uimbike kuwa miguu mine ni bora na miguu miwili ni bora zaidi. Walijaribu kujivua asili yao na kutaka kustaarabika kama binadamu waliyemfukuza shambani. Tulipowaondoa wakoloni halafu tukaanzisha na kujiunga na jumuiza zao tukidhani tunaweza kustaarabika zaidi yao katika ulimwengu wao ndipo tulianza kufanya makosa. Tulipaswa kwanza kujitathmini na kujenga mfumo wetu (system) ambao ungetuwezesha kufikisha malengo ya mipango yetu ya ustawi. Tulipaswa kudharau imaginary boundaries walizoweka miaka ya 1884 na kama kulikuwa na ulazima tuweke mipaka mipya kwa wataopenda kujitenga lakini tungekuwa na Afrika moja. Hii ingewezekana kwa kuunganisha nchi zilizojikomboa na kila nchi inayokombolewa utumwani inakuwa ni sehemu ya taifa huru la Afrika. Lakini wazungu walijua kwamba tukinusishwa harufu ya fedha na ukwasi feki watatuwini. Angalia sasa tunapewa misaada ambayo ingawa asilimia 60 inarudi kwao kwa mlango wa nyuma lakini hicho kiduchu kinachosalia kinaliwa na wanajua kinaliwa halafu hawaachi kutoa misaada (fresh loans) wakijua itatugawanya na tutashindwa kusimamia vyema. Wameweka vyombo vya kusimamia uchumi vya kwao chini ya himaya zao huku wakitupangia sisi nani wa kujiunga naye na nani wa kumtenga. Gadem.
  Kwa hali hii Naapa, nawaambia watanzania wenzangu hatutafika kamwe kwenye maendeleo na ustawi bora, hata tukichagua viongozi wenye msimamo wa SIMBA (samahani wapenzi wa yanga) hawataweza kufikia lengo au hata kupiga hatua moja, kwani tumezoea sisi kwenda kujitambulisha kwao na wao wala hawaji kujitambulisha kwetu ingawa sisi ni MUHIMU sana kwa uhai wao. Tukitaka kuendelea ni muhimu sana kufanya yafuatayo:-
  1.Kukataa misaada na mikopo yao
  2.Kuiwezesha serikali kufanya BIASHARA
  3.Kuunganisha nguvu katika kuipa nguvu elimu na tafakuri zetu
  4.Kusimamisha operesheni zao zote za kiuchumi humu kwetu mpaka tutakapojipanga vyema
  5.Kujenga mfumo bora wa mitaala itoe elimu-tendaji na si elimu ya msingi (wa banda bovu)
  6.Kuunganisha bara la afrika kwa mfumo wa kikanda au lote jumla ili kuondoa fikra za kibeberu kwamba wanaweza kutugawanya.

  Katika point ya pili nimesema serikali kupiga bizness, ni ukweli usiopingika kwamba mataifa tajiri yalifanya biashara kwa mafanikio kwa miaka zaidi ya 800, wakajenga mfumo bora wa kusimamia na kukusanya mapato halafu sisi ambao hata miaka 100 bado tunaambiwa kwamba ni marufuku kufanya biashara na tunakubaliana nao, tunapiga makofi na toothpicks mdomoni tukitoka ktk makongamano-dhifa. Tangu lini mzee akishakuwa kibogoyo hawezi kula nyama aweze kupiga veto ya kuzuia nyama isipikwe home ambapo kuna watoto wenye mataya kama ya simba (ops! yanga sorry again)? Kama wao wameshakuwa vibogoyo watuache sisi tuendele kuvunja mifupa ili tukifika ktk umri wao tuwe na protini za kutosha. Wanatunyanyapaa huku directors wetu wakisema huo ndo mfumo wa dunia.
  Halafu ninyi madairekta mkishakwiba hela zinazotoka kwao mnarudisha kuzificha ktk benki zao, wanawaumbua kila kukicha na hamkomi. Kweli sisi tumelaanika.

  Nimeongea kwa ujumla najua wakulu mtazama ndani zaidi ya hapa. (Last time mlinisifia sana ila leo naomba inputs zenu tufanye nini?)

  Guys, we are NUTS and ndivyo TULIVYO – (Nyani Ngabu) endapo hatutataka kwa DHAMIRA kujinasua katika mtego ungali haujakaba sana shingo zetu.
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hii ni kweli kabisa
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Msanii, well uliyoyaongea yana ukweli lakini mimi naona tatizo letu kubwa ni kwamba hata baada ya kugundua tumekwama bado tunaendelea kufanya yaleyale, mipango ile ile, viongozi walewale. In reality nik kwamba "If we don't change we will remain the same"
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  well said mkuu
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  hivi laana ni nini?
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu siamini kama hujui maana ya laana.
  Kuna kamusi za kiswahili zinapatikana bwelele katika kila mkoa nchini tanzania.
  Jitahidi kujielimisha katika hilo shekhe
   
 7. M

  Mokiwa New Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena...
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Umeniwahi mkuu, nilikuwa najiuliza swali hili hili.

  Muandishi kaweka kichwa kuhusu laana halafu hata hajaielezea laana ni nini, na kama anaongelea laana literally au allegorically.

  Kama anaongelea laana literally mimi siamini katika this primitive thinking.

  Kama anaongelea allegorically, well, the allegory is based on mythology, which is not to say it cannot be instructive.

  Kwingine naona kama ameshindwa kuweka wazi objective zake na kuwa consistent, maana naona kama anawablast wazungu na kuja na african pride, back to the roots and all that jazz, halafu ana conclude na miafrika ndivyo ilivyo, haeleweki, hana consistency.

  Nilitegemea mtu anayewablast wazungu na mwenye african pride aone past the shallow simplicity of "miafrika ndivyo ilivyo".
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  you have said it WELL
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ndo laana yenyewe hiyo
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Uvivu wa kusoma inaweza kuwa ni sababu ila pia kuelewa hoja ni ni other ishu.
  Ukisoma kwa makini utajiweka ktk mstari sahihi wa kuelewa cha kuchangia.

  Pole pole tutafika
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Bado viongozi wetu wapo ktk fungate la uhuru.
  sisi tnawaangalia tu!
   
Loading...