Chimbuko la kabila la Wairaq

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
WAIRAQ au Wairaki ni kabila kubwa linalozungumza lugha jamii ya Wakushi na linalopatikana Mkoa wa Manyara wilaya za Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha katika wilaya ya Karatu.

Watu wa kabila hilo wana uhusiano wa asili na makabila ya Gorowa, Burungi na Alawa ambao wanaishi katika wilaya za Babati na Kondoa. Historia kwa njia ya simulizi za makabila inasema chimbuko la Wairaqw linatokana na kizazi cha watu wa kale walivyokuwa wakiishi eneo la Mesopotamia, Iraq.

Vita ya mara kwa mara ilisababisha watu hao kuhama makazi yao ya asili katika karne ya nne hadi ya sita baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw walivuka bahari ya Sham kwa mashua na kutua Ethiopia ambako waliishi kwa muda kisha kuendelea kuhama kuelekea Kusini Magharibi kupitia bonde la ufa kando ya Ziwa Victoria na kuweka kambi eneo waliloona ni salama.

Kwa kuwa ni watu wasiopenda vita waliendelea kuhamahama wakikimbia vita vilivyoruka sehemu mbalimbali walizojaribu kuweka kambi. Walipita njia ya kati kupitia Iramba Mkoa wa Singida Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa ambapo walikutana na mapambano ya Wahehe, Wangoni na Wazimba.

Hali hiyo iliwalazimu kubadilisha njia na kurejea kuelekea Kaskazini hadi sehemu ya Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay na kuishi eneo hilo huku wakijishughulisha na ufugaji na kilimo kidogo. Hata hivyo ilitokea kutokuelewana kati yao na watu wa kabila la Wabarbaig jambo lililosababisha vita.

Ingawa walikuwa waoga wa vita walikuwa na silaha za kujihami dhidi ya vita. Walitumia mikuki na mishale ya asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zana zinazotengenezwa kwa kutumia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali kama tofali.

Hata hivyo Wairaq walishindwa vita na kukimbilia karibu na mlima Hanang kisha wakagawanyika wengine wakaelekea mlima Dabil hadi Guser na Gangaru ambapo walifanya maskani. Wairaq walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqw waliotawaliwa na Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwa Yaabusmo.

Kila mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopenda kushirikiana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; “Walikuwa na waganga wa kiasili waliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.

Simulizi zinasema kuwa Wairaq walikuwa na kiongozi maarufu kwa jina la Haymu Tipe ambaye aliongoza msafara kupeleka watu wake katika eneo salama tulivu ili kukidhi kiu yao ya kuishi kwa amani na kujenga jamii yenye upendo na mshikamano.

Haymu alifika sehemu yenye ziwa na inasemekana kuwa alimuagiza mtumishi wake maarufu kwa jina la Moya kuhamisha ziwa ili watu waweze kupata eneo la kutosha. Moya alitii amri ya kiongozi wake kisha kutumia uganga kuhamisha ziwa kwa kutupa mshale katikati ya ziwa hilo.

Inadaiwa kuwa mtumishi huyo alipofanya hivyo ziwa lilihama pamoja naye hadi katika bonde la ufa ambapo hivi sasa linajulikana kama Ziwa Manyara na ila Wairag wanaliita “Tlawta Moya” kwa lengo la kudumisha jina la Moya. Baada ya ziwa kuhama kiongozi huyo aliendelea kuishi hapo na watu wake na kuendelea kutawanyika katika maeneo ya Muray, Kuta, Amoa, Kainam, Suum, Datlaa, Tsaayo Wilaya ya Mbulu.

Baadaye Wairaqw wakatawanyika taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makao makuu yao mpaka leo. Baadhi ya mila na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudi kama matumizi ya kondoo katika jamii.

Wajihi na rangi ya Wairaq ni kielelezo kuwa asili yao ni Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati kwa kuwa wanafanana zaidi na watu wa Afrika Kaskazini kuliko wabantu na Wamasaai ambao wanaishi jirani na Wairaqw.

Hata hivyo Wairaqw wameingiliana na kuoana na makabila ya jirani ya kibantu hivyo kupoteza rangi iliyokuwa inawatofautisha na wabantu. Hivi sasa baadhi ya watu hawana tofauti na wabantu na wanaweza kutofautisha kwa lugha ya kipekee yenye matamshi ya semitiki na kushi hivyo kulifanya kabila la Iraqw kuwa na lugha tofauti kabisa na makabila mengine.

Pia katika lugha yao kuna maneno yanayofanana lugha ya Kiarabu. Mfano wakati Wairaq wanatumia neno maai wakimaanisha maji Waarabu hutumia neno maa. Joto kwa lugha ya Kiiraq ni hame wakati kwa Kiarabu ni hami. Neno moja kwa Kiiraq ni Wak na kwa Kiarabu ni wahed.

Maneno mengine yanayoshabihiana na aning kwa Kiiraq wakati kwa Kiarabu ni ana ikiwa na maana mimi. Neno “gumu” kwa Kiiraq ni gawit wakati Kiarabu ni gawi. Kutokana na mifano hiyo ni wazi kuwa Wairaq wanaweza kusikilizana na Waarabu kuliko makabila mengine ya kibantu na Kinailoti. Wairaq wanajishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji.

Awali walitegemea nyama kama chakula chao kikuu. Walichinja mifugo na kuwinda wanyama pori ili kupata chakula cha kutosha. Kama ilivyo kwa makabila mengine ya Kiafrika Wairaq walitumia zana duni kukabiliana na changamoto za maisha. Walichuna nyama kwa kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu.

Mapishi yao yalitokana na moto unaopatikana kwa njia ya kupekecha mti maarufu kama Bui na Daha ambapo ulipekechwa hadi moto utokee. Hata hivyo waliacha kutegemea nyama kama chakula kikuu na badala yake walianza kula vyakula vinavyotokana na nafaka hasa baada ya kuanza kujishughulisha na kilimo cha mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa kunde.

Nafaka zilihifadhiwa kwenye ghala za asili maarufu kama Kuntay ambazo zilizotengenezwa kwa vinyesi vya ng’ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu ya vinyesi vya ng’ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa na wadudu. Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika sasa.

Nafaka hizo zilisagwa kwa kutumia jiwe la mkono na unga uliyopatikana ulitumika kupikia ugali mlaini maarufu kama Xwante. Ugali huo unafanana na uji uliopoa. Nafaka hiyo pia hutumika kutengenezea pombe ya asili ambayo hutumika kama viburudisho wakati wa sherehe mbalimbali za kimila.

Uchumii wa jadi wa Wairaqw unategemea ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali za kilimo na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali au mifugo kwa vifaa au zana. Hata hivyo hivi sasa Wairaq wamebadilisha baadhi ya mambo katika mfumo wao wa maisha na wanatumia fedha kufanyabiashara mbalimbali.

Kama ilivyo kwa makabila mengine Wairaq wanamila na desturi zinazowatofautisha na makabila mengine hasa katika malezi ya watoto, ndoa, mavazi, ngoma na mfumo mzima wa maisha ya kila siku. Kwa mujibu wa Wairaq mtoto wa kike na wa kiume anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema ya kuishi na jamii.

Kina mama ndio wenye jukumu la kufundisha watoto wa kike jinsi ya kuishi na mume, kutunza familia na mbinu za kukabiliana na maisha ya kisasa. Mtoto wa kiume hufundishwa na wanaume na mafunzo hayo husisitiza umuhimu wa kuwa na maadili mema, upendo na mshikamano katika jamii na mbinu za kujitegemea na kukabiliana na changamoto mbalimbali kama mkuu wa kaya.

Wairaq ni miongoni mwa makabila ambayo awali yaligoma kuwapeleka watoto wao shule kwa hofu kwamba elimu kutoka mataifa ya magharibi yatasababisha watoto wao wapotoka au kuacha mila na desturi zao.

Hata hivyo hivi sasa wamepata mwamko wa kupeleka watoto shule ingawa bado kuna wazazi ambao wanazuia watoto wa kiume kwenda shule ili waweze kufanya kazi hasa kuchunga mifugo wakati watoto wa kike wanaozeshwa wangali na umri mdogo ili wazazi waweze kuongeza kipato kwa njia ya mahari. Wairaq walitumia utaratibu wa asili kudumisha amani katika jamii.

Wale waliokosa walifikishwa katika mahakama za kijadi ambapo adhabu zilitolewa kwa taratibu za mila kwa kuzingatia aina na ukubwa wa kosa. Kabla ya kutoa hukumu makosa yote yaliyotokea katika jamii hujadiliwa na baraza la wazee linalojumuisha wanawake na wanaume ambao hutoa maamuzi ya busara.

Kama ilivyo katika mahakama za kisasa, Baraza la usuluhishi la wa wazee wa Kiiraq lilitoa fursa kwa mkosaji kujieleza na kujitetea kabla ya kutoa hukumu. Kama mtuhumiwa ni mwanamke basi wanawake walipewa nafasi ya kujadili kosa husika na kama mkosaji ni mwanamume wanaume walijadili kwanza kabla ya kuwashirikisha wanawake kutoa uamuzi wa pamoja kiisha adhabu kutolewa na jamii nzima.

Watuhumiwa waliopatikana na makosa yaliyothibitika walitozwa faini ya kimila maarufu kama “Dohho” au waliagizwa kulipa fidia kwa mlalamikaji. Watuhumiwa waliokana mashtaka hata kama kuna ushahidi walipewa adhabu ya kutengwa na jamii nzima.

Pia kwa kesi ambazo hazina ushahidi mlalamikaji na mlalamikiwa waliapishwa ili kuthibitisha kuwa yote aliyosema ni sahihi. Ikiwa mtu alisema uongo laana ilimpata hivyo ilikuwa ni nadra sana kwa mtu kuapa uongo kwa kuwa laana ilimshika yeye na kizazi chake. Wairaqw walitumia mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali.

Mizizi hiyo ilichemshwa au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa na inasemekana kuwa mgonjwa akishakunywa dawa hiyo alipona baada ya muda mfupi. Kama ilivyo kwa makabila mengine Wairaq wana utajiri wa historia ya utamaduni, mila na desturi ambazo zinaiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yenye urithi mkubwa wa tamaduni na mambo ya kale.

Wairaq wana aina mbili ya ngoma za asili. Mosi ngoma ya ndani yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wa kike anapoolewa au wa kiume anapooa. Nyimbo maarufu kama Mudeli huimbwa wakati wa harusi kwa lengo la kumpongeza bwana harusi na bibi harusi, na nyimbo hizo huimbwa na wanawake.

Ngoma ya pili maarufu kama Gilo huchezwa nje eneo la wazi na huchezwa kila mwaka wakati wa mavuno kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu. Wakati wa kuweka sherehe ya shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombi maarufu kama Slufay pamoja na Giriyda.

Giriyda ni nyimbo maalumu ya kuomba mambo mazuri na kuepusha mambo mabaya. Pia nyimbo maarufu kama Sibeli ni maalumu kwa akinamama kwa lengo la kutoa shukrani kwa Mungu. Mavazi ya asili ya Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili ya shuka, sketi au khanga.

Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi la kike lilikuwa sketi na shuka ndogo mithili ya khanga. Pia wanaume na wanawake walivaa viatu vilivyotengenezwa na ngozi. Hata hivyo utamaduni wa kuvaa nguo za asili umeanza kupotea na hivi sasa idadi kubwa ya Wairaq wanavaa nguo za kawaida.

C&P kutoka FB
FB_IMG_1611901657952.jpg
 
Naas lowale khaen! Umesahau kitu kimoja ambacho watu hudhani tofauti, dada zetu ni wazuri mno. Japo wametoka katika familia zenye dhiki. Hii imekua fimbo ya kuwachapa kwa kuwatumia na kuwaita Malaya. Wenginee ni wanyonge na hufanywa hivi kwa kua ni wanawake tu!

Enyi wazee wangu mliolala makaburi ya mama isara ijazeni mishipa yangu ujasiri, nitumeni Kama mlivyomtoa sadaka Moya, nitieni nguvu napokata tamaa kwa upepo mwanana wenye kuupuliza moyo Kama upepo wa tlawta Mundi. Nilisheni Kande zuri na maziwa matam yaliyo ndani ya qumi pale napokuwa usingizini nikiwa nimechoshwa na malimwengu. Turudishieni nguvu ya kiutawala tuweze kupakumbuka kwetu japo kweli tupo ng'ambo tukiyasaka maisha"
 
Wambulu. Ndo nn,,,mada Ni wairaqw,,,we unasema wambulu,,,hakuna kabila la wambulu elewa Hilo kwanza
Sawa ndio hao hao tu, huku kwetu tunawaita Wambulu...najua baadhi hamlipendi lakini pole.

Hata Butcher yetu ya Kitimoto hapa Mtaani Mmiliki wake tunamuita "MBULUU".......Butcher ameiandika "saita bucha".
 
Hii stori ya kutoka Iraq itakuwa siyo kweli bali ni coincidence tu ya jina. Wairaq ni Southern cush, wale wa Ethiopia wakiwa nothern cush. Walikuwepo hapa Africa ya mashariki kabla hata ya sisi wabantu.

Kama kweli walitoka huko badi hata lugha na DNA ingeonyesha.
Kwani wewe unauhakika DNA haikufanyiwa majaribio? Jina Iraq wala haina uhusinao na IRAQ ya nchi maana wao similizi zinasema waliyoka kabla hata hiyo nchi haijaitwa IRAQ. IRAQ zamani inaitwa Babeli au Babiloni au Mesopotamia.
 
Back
Top Bottom