Chikomo asili yake wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chikomo asili yake wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bazobonankira, May 28, 2009.

 1. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau wa Forum,

  Heshima kwenu nyote!! Sina uhakika kuwa kwa kuwasilisha swali langu hapa nitaweza kupata ufafanuzi ama nitakwaza maslahi ya baadhi ya watu fulani fulani. Pamoja na wasisasi nilio nao, dhamira yangu inanituma kuweka swali hili mahala hapa na kutarajia michango yakinifu.

  Katika pita pita zangu hapa na pale, nimepata kukutana na mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa John Chikomo. Sikupata kumjua kabla, mpaka hapo nilipokutana naye.

  Kisha akaendelea kujitambulisha ya kwamba anaongoza taasisi/chama kinachojihusisha na mazingira hapa nchini.

  Baada ya utambulisho huo nilibaki na maswali kadhaa, ambayo nilipojaribu kumdadisi hakupenda kuzungumzia katu! Kati ya maswali ya msingi niliyojiuliza ni kuwa:

  Je, Chikomo ni jina kutoka maeneo gani hasa hapa Tanzania? Kwa maana Chikomo kadhaa niliopata kuwasikia wote wanatoka kati ya Zimbabwe na Malawi.

  Kama ni kweli ninavyohisi (inategemea na wadau watasema nini kuhusu majina haya), ni kwa vipi raia wa kigeni kuongoza harakati za taasisi ya mazingira yenye kutetea maslahi yetu?

  Naomba kuwasilisha hoja!
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Asili yake Mtwara
   
 3. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #3
  May 28, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi! Ila wasiwasi wangu ni kuwa usijekuwa umechanganywa na majina ya kina Chupaki, Chukurubu, Chiatu etc sababu yanaanza na "CH".

  Kwa mbali nahisi hivyo. Ila kama si kwa sababu hiyo, again, nashukuru.
   
 4. nkawa

  nkawa Senior Member

  #4
  May 28, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unachotaka kujua kama huyo bwana ni mtanzania au la? Yaweza kuwa Chikomo ni Majina ya Zimbabwe sawa, lakini ni raia wa Tanzania!!!!!! si ana haki?
   
 5. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  May be you should check these, then you will be in a position to imagine where my doubts are coming from

  Freeman Otto Chikomo - Zimbambwean Proffessor
  Tawanda Chikomo - Zimbabwean Poet
  Mushaka, A., Chikomo - Zimbabwean Resercher on Agroforestry
  Willie Chikomo - Zimbabwean Boxer
  Late Joseph Chikomo - Former Financial Gazette's board member and prominent businessman
  Herbert Philemon Chikomo - Anglican Reverend in Zimbabwe
  Abel Chikomo - Zimbabwean Journalist
  Ronald Chikomo - Zimbabwean footballer playing for Gaborone United

  Wadau, those people above are just a few Zimbabweans I can refer to. Kama kuna mwenye orodha ya Watanzania wenye ubini huu (surname), please tusaidiane.

  Nawasilisha hoja
   
 6. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #6
  May 29, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naanza kuamini ya kwamba hisia zangu juu ya swala hili kuwa ni sahihi. So far, hakuna anayeweza kubisha, based on reference up there, ya kwamba Chikomo by all common sense ni Zimbabwean.

  Sasa hoja itokanayo, sheria za nchi na kanuni zinasemaje kwa raia wa kigeni kuongoza taasisi ya wazawa?

  I am still curious!
   
 7. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyo John Chikomo unayemsema mazingira, namfahamu sana, ni accountant by profession. Ninachojua mimi ni Mmakonde kwa kabila, sasa kama ame originate Zimbabwe hiyo sifahamu, ila sidhani hata kama huko Zim anapajua. Labda generation zake 3 au 4 zilizopita ndio zilitoka huko.
  Amesoma Tambaza na Mtwara alikotoka, yawezekana huyo babu yake mzaa babu, mzaa babu ndio alitokea huko na kuishia Mtwara. Huyo utamuita Mzim?
  Mimi nafikiri yeye kua mwanaharakati wa mazingira haina mjadala maana ni mtanzania wa kuzaliwa hapa na si wa kuhamia, waliohamia LABDA
   
 8. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #8
  May 29, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Under reasonable doubts, we all know Joseph Kabila, President of DRC, that he schooled here and even attanded National Service with some comrades here. He could have climbed his ladder here and even become a powerful political entity in our country - for mojority assumung he is a Tanzanian (based on fact that he schooled here). He was, is and will not be a Tanzanian.

  And to be frank, we have some serious loopholes here. What you are saying could be true or NOT. Too good to be true though
   
 9. c

  chikuta Member

  #9
  Jun 1, 2009
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi Hodi wenzangu,

  Nimekuwa nikifurahishwa sana na mada pamoja na mijadala mbalimbali inayoendeshwa katika forum ya Jamii. Ingawa siku zote nimekuwa msomaji tu, sasa nimeamua kujiunga rasmi. Naamini nitapokelewa vyema na wadau wote.

  Kwa kuanza na hili la jina la Chikomo, mashaka waliyonayo baadhi ya wachangiaji hata mimi ninayo.

  Kwa asili mimi ni mmakonde wa Mtwara. Nimezaliwa na kukulia huko. Nafahamu vyema maana na asili ya majina ya kwetu. Kusema kweli sijapata kuona wala kusikia jina la namna hii kule. Sidhani na nasema siamini kuwa ni jina la kwetu.

  Yawezekana tu kuwa mtu anatumia fursa ya jina kufananafanana kinamna na majina ya kusini ili kutimiza malengo yake anayoyajua mwenyewe. Ikiwa kuna mtu mwingine yeyote anayefahamika kwa jina hilo na anatoka Kusini naomba mwenye kufahamu atuhabarishe sote.

  Vinginevyo itabidi tu tusubiri busara za wadau wa uhamiaji watusaidie katika hili.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe uliyeanzisha thread shida yako ni kabila la Chikomo au uraia wake? Naona kuna kitu hapa unataka kukianzisha..kama unatatizwa na uraia wa Chikomo au lolote nenda kwenye mamlaka husika. Hapa jamvini huu ni upupu.
   
 11. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Unajua haya majina wa watu wa Ntwara huwa na prefix ya CH kwa asilimia kubwa. Mfano Chipoku, chikalumbe, chimae, Nankochokocho nk. Isipokuwa majina yanaingiliana hasa unapoitafuta asili kwa sababu wote ni wabantu hata kama ni wa Zimbabwe au Malawi (Chiume).
   
 12. c

  chikuta Member

  #12
  Jun 1, 2009
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naanza kupata wasiwasi na baadhi ya wachangiaji juu ya uwezo wao wa kuchangia hoja. Ikiwa kila mwenye kutatizwa na jambo lolote hapa angeamua kuwa anaenda mahakamani, bila shaka hii forum ingekuwa na post 2 tu kila mwezi!

  Naamini hapa ni mahala huru pa kujadili mada mbalimbali, ilimradi tu unayechangiia aidha uwe umevutiwa ama kuguswa na mada husika.

  Kusema kuwa "hapa jamvini huu ni upupu" pia unaniacha na kajiswali lengine, je unawasha baadhi ya watu ukiwemo wewe au unamaanisha ni hoja isiyojadilika?

  Ni vema kueshimu maoni ya baadhi ya watu. Naamini ikiwa mtu hauko iterested na mada inayojadiliwa, ni vema ama kutoisoma au kuisoma na kisha kuendelea na mada nyingine ambazo ungeweza kuchangia positively.

  HAbari ndiyo hiyo!!
   
 13. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #13
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Abdul,

  LAbda unisaidie kidogo, unaposema kuna jambo nataka kulianzisha, ni lipi hilo? Tafadhali soma vizuri pasipo na haraka my very first post on this subject labda utaelewa.

  However, if at all kina hisia unazopata ni vema uziweke wazi.

  Hoja hujibiwa kwa hoja na si kuambiana watu kuwa waende mahakamani.

  Otherwise baadhi yetu tutaanza kuhisi kuwa unatumika na mshukiwa kujihami!!
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni vema hivyo ulivyoanza kuwa na wasiwasi, na naona umechelewa sana. Tena ningependekeza uanze kwanza kujijengea wasiwasi wewe mwenyewe kwa kushindwa kuona issues.

  Kwa ufupi,hakuna mtu aliyekatazwa kuuliza anapotatizwa,(hata hivyo sina na sihitaji mamlaka ya kuzuia watu kutoa maoni yao) ila huyu mleta thread inaonekana ana ka-ishu fulani na Bw.Chikomo kama sio unfinished business .Ukiangalia muelekeo wa tenzi za mleta hoja utagundua hili.Sasa kama huwezi kuliona hili, inabidi uanze si tu kuwa na wasiwasi na uchangiaji hoja wa wengine bali wa uelewa wako duni.

  This is not new. Say something we don't know.
  Ni upupu kwa maana kuwa thread ina-irritate jamvi na kulifanya lisikalike,hii ni kwa kwa jinsi nionavyo, na hili ni jamvi huru, kama ulivyosema, sivyo?

  Sijasema siko interested ndugu, niko interested na ndio maana nimempa msaada wa fikra huyu ndugu mleta hoja(refer post uliyoinukulu). Pia heshima sio kukubaliana na kila kitu kinachokuja hapa jamvini.
   
  Last edited: Jun 1, 2009
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Need I say more?
   
 16. K

  Kitoto Akisa Member

  #16
  Jun 1, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bazo ninachoona hapa una muhukumu moja kwa moja Chikomo kuwa sio raia wa Tanzania! umeliza watu wanao mfahamu wamekupa majibu kuwa huyu jamaa ni raia, haijarishi ni raia wa kuzaliwa au wa kuandikisha. Mbona wapo watanzania wengi tu ambao majina yao yahana asili ya Tanzania, hebu niambie majina kama Meley Bhalaboo, Subash Patel, Chavda, Meghji, kassam na mengine mengi, asili yake wapi hapa Tanzania? lakini tunajua wote hao niliowataja ni watanzania.
   
 17. c

  chikuta Member

  #17
  Jun 1, 2009
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, mimi kwa namna moja naweza kukubaliana na wewe kabisa. Naanza kuliona tatizo kwa Abdul, maana majibu yake yamejaa jazba.

  Hoja ya msingi ya Bazo naona bado haijajibiwa kinagaubaga.

  Respect...
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndg unakubaliana na Kitoto ktk lipi? Maana alichosema kinafanana na hoja ya msingi niliyoileta.

  Naona umeshindwa kuona issues na kuzielewa, hivyo basi nashauri waachie wenye macho wazione na kuzifanyia kazi, kama umeshindwa kuziona issues hainitatizi kwamba ulichoona ni jazba. Sawasawa?
   
 19. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #19
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na ndio maana kabisa, tangu mwanzo nilihisi kuna maslahi ya watu yataguswa hapa!!

  Tutaona mengi... Lol
   
Loading...