Chikito wa Ferre Gola hicho kipaji kasomea?

Chikito wa Ferre Gola hicho kipaji kasomea?

japo ni mwana wenge musica bcbg mwenzangu na nimefurahi kukufahamu ila napenda nikurekebishe kidogo sehemu fulani mkuu. hivi unaposema jb mpiana ana dharau utamweka wapi mopao mokonzi koffi olomide? dharau kwa wakongo ni kama vile chupi na tako na ili uliamini hili waangalie tu hata hawa wacongo tulionao hapa bongo akina nyoshi, patcho mwamba na christian bella. katika hili naomba ututake radhi sisi pro-jb mpiana. a.k.a ya motopamba siyo tusi kama ulivyoaminishwa bali maana yake ni mvaaji mzuri na anayevutia na ndiyo maana utaona kila wakati wa onyesho la " live " jb mpiana akiwa tu anapanda jukwaani utawasikia marepa wake mahiri gentamycine lisomo na cellulaire vanga wanamtaja sana kwa kuita " moto pamba " halafu yeye jb mpiana anazishika zile nguo zake na kuwaringishia watu na hufanya hivi hasa hasa kushindana na adui yake mkubwa kimuziki koffi olomide. kuhusu jb mpiana kuwaita na kuwadharau masikini unatukosea tena adabu wafuasi wake kwani uliza congo nzima ni mwanamuziki gani mwenye kikosi maalum cha kuwatunza wanamuziki ambao baadae huja kuwapandisha katika bendi ya wakubwa na wengine huwauza katika bendi nyingine na jb mpiana si tu anakaa nao bure bali mara nyingi shows zake nyingi za ndani ya congo huwatumia sana hawa jamaa na hili kundi au hiki kikosi huitwa p.p.u na humu wametoka watu wengi sana kwa mfano huyu repa cellulaire vanga ametoka huko, kuna mpiga solo mmoja wa sasa wa wenge bcbg ambaye ni moto wa kuotea mbali anaitwa shevchenko patou solo na dogo mmoja muimbaji anaitwa nono fuji ambao wapo wenge bcbg huku mwingine akiwa ni repa mahiri wa sasa wa koffi olomide anaitwa gesac ambaye zamani alikuwa repa wa felix wazekwa. kuhusu huyo mkongoman huko kampala kumwita motopamba na kutaka kukupiga ni kwamba kaa ukijua kuwa hakuna nchi ambayo kuna ukanda na ukabila kama congo na jb mpiana ni mluba huku koffi akiwa ni mmanyema na werrason ni mbwiti na tambua kuwa congo nzima kimuziki inagawanywa na hawa wanamuziki wakubwa watatu wa kizazi hiki cha kati hivyo kuna uwezekano mkubwa huyo uliyemuuliza akawa ni mfuasi wa either koffi au werrason. mwisho chai ngenge hakuondoka wenge bcbg kwa sababu ya jb mpiana bali alikuwa na bifu na mpiga drums na naibu mkurugenzi wa bendi aitwae serge mignon maniata kwa kuwa wote walikuwa wanatembea ( wanambandua ) mcheza shoo mmoja mzuri na maarufu aitwae virginie bokassa. una lingine mkuu?

Duuu!! Saluti kwako mkubwa
 
Badala ya French......kwa nini tusijifunze kilingala.......pona nini......makambo ezali minene......?.......sala noki.....nakotunatuna........le SIDA......mwasi kitoko.........

Hahahaaaa!! Tokomonono na nzima Preta.😛
 
Badala ya French......kwa nini tusijifunze kilingala.......pona nini......makambo ezali minene......?.......sala noki.....nakotunatuna........le SIDA......mwasi kitoko.........

unajua maana ya mwasi kitoko? kwa heshima na taadhima kama wewe ni mwana dada basi naomba nikupe heshima ya kukuita mwasi kitoko ikimaanisha mdada mzuri ( beautiful lady ).
 
nikiwa namjibia tu pacha wangu gentamycine aliyepumzishwa kilazima ni kwamba uliyoyaandika hapo ni sahihi kabisa ila kuna nyimbo umezitaja hapo imebidi nitokwe na machozi na kulaumu kwanini wenge bcbg ilisambaratika. nyimbo kama love airline, liberation, serge palmi wenge bcbg walitulia. kwenye bendi yoyote ukiwa na mtu kama titina alcapone le grand prete ambaye alikuwa ni drummer mkuu huku katika solo guitar akiwepo burkina faso mboka liya ambaye kwa sasa anayepatia kupiga solo lake ni kijana mmoja aitwae cain madoka ambaye shughuli yake inajulikana katika wimbo wa evelyn wa bendi nzima ya loketo chini ya aurlus mabele na kuna watu muhimu mkuu hapo juu umewasahau nao ni mpiga keyboard maarufu theo bindens ambaye kwa sasa amerithiwa na wapiga vinanda wawili wakali waitwao cedric gezeula na geremi kitubu na ukitaka pia kujua moto wa hawa jamaa wawili tafuta live dvd ya wenge bcbg halafu sikiliza wimbo uitwao le baron. katika safu zote za uimbaji umepatia kuwataja ila lazima tukubali kuwa viwango hutofautiana na hapa nisimung'unye maneno wenge bcbg ya sasa inasimamiwa vizuri sana na huyu kiongozi wa wanamuziki ndani ya bendi nzima ya bcbg mhadhiri wa lugha wa chuo kikuu cha kinshasa aitwae jules kibens molongeshi ambao wengi wenu mnamuita le professer ambapo kwa kifaransa inamaanisha mwalimu kutokana na yeye kuwa mwalimu wa university. huyu jules kibens kazi yake aliianza katika album ya internet, anti terro na ya kipe ya yo kwani huyu ndiye hurekebisha nyimbo zote za wenge bcbg, nani aimbe mstari gani, atamke matamshi gani na sauti ikaeje. kwa wale tuliohudhuria ujio wa wenge bcbg dar walipopiga pale leaders club mtakubaliana na mimi. mwisho kabisa nitakuwa namkosea hata mwenyezi mungu nisipomtaja makamu mkurugenzi wa bendi ya wenge bcbg na ambaye pia kwa sasa ndiye mpiga drums mkuu aitwae serge mignon maniata. utamu wote wa nyimbo za wenge bcbg unaanzia kwa huyu jamaa na ndiye kipenzi mkuu wa rais wa bendi ya wenge bcbg jean bedele tshituka mpiana na ukiona mwanamuziki yoyote wa wenge bcbg amefukuzwa bendini basi ujue serge mignon maniata ndiyo kasababisha. kwa mfano hata kuondoka kwa waimbaji mahiri chai ngege na djino equalizer kulitokana na huyu mpiga drums. jb mpiana hamwamini mtu yoyote zaidi ya huyu serge mignon maniata na hata mic ya kuimbia hukaa nayo yeye na maji ya kunywa ya jb mpiana huyu jamaa ndiyo huyatunza. katika upande wa kughani ( kurapu ) au wenyewe wakongo huita atalaku kwa kifaransa husema animateur kwa sasa ndani ya wenge bcbg hakuna ubishi kuwa gentamycine lisimo na mwenzake cellulaire vanga ndiyo injini ya wenge bcbg huku vijana wengine chipukizi akina pajo na bin laden nao wakija juu. mkuu ukiitaja tu wenge bcbg basi ujue umegusa mshipa wangu wa fahamu ulio timilifu kwani nahisi hata girlfriend wangu simpendi kama ninavyoipenda hii bendi ya wenge musica bcbg.

Mkuu pamoja sana, mimi kwenye USB yangu muda wote nakula Wenge.
Hivi mkuu, sijakusoma kwani Album ya Internet ilitoka kabla ya Toujours Humble na Titanic? Maana Jules Kibens yumo kwenye Album ya Titanic, angalia wimbo wa Champion Kapangala, na lakini pia angalia kwenye wimbo wa Mohamed Kaniasi album ya TH, yumo pia.

Chuki nyingine kumuhusu Mignon ni ule ukweli kwamba, hawa watu ni ndugu, yaani JB Mpiana wana undugu, nadhani ni mtu na binamu, so ukijumlisha jamaa anajua fani na hivyo JB Mpiana anamuamini, wengi wanapatwa na wivu! Ila mkuu hukunipa mrejesho kuhusu G7.

Ila Wenge ya JB Mpiana naona kama imepoa sana siku hizi, haina jipya. Ukisikiliza Wenge ile ya Walayi Danico,48 Heures Gecoco, Jeanpy Pipina, Omba, Liberation, Ndombola Remix, Papito Mbala Remix, ilikua ni hatari tupu!
 
hizo albums zote jules kibens alikuwa anashirikishwa tu katika nyimbo na hakupewa meno yote kwani alikuwa chini ya nguli na kijana ambaye hadi leo jb mpiana anamlilia alain mpela " afande " na jules kibens kaja kuibuka baada ya alain mpela kuondoka na kupewa meno ambapo sasa ni mkuu wa wanamuziki wote katika bendi, mtunzi mkuu, mhariri mkuu na mpanga miziki mkuu yote ya nyimbo za sasa za wenge musica bcbg. unasema kuwa wenge musica bcbg ya sasa haina tena makali yake labda wewe siyo mwana wenge bcbg na hufuatilii vilivyo miziki ya congo. nakupa task leo mtafute mtu yoyote wa congo hata hawa waliopo hapa dar kuwa sasa hivi congo kuna mtindo gani ambao umebamba? lazima tu watakuambia kuwa sasa congo huwaambii kitu mbele ya huu mtindo wa " mbunda " na " rota rota " na kukupa zaidi kazi ya wenge musica bcbg za hivi karibuni tafuta albums hizi kipe ya yo ( ikimaanisha hayakuhusu ) na quest le probleme ( tatizo lako ni nini? ) halafu nakuomba zisikilize kwa umakini mkubwa sana nyimbo za " voiture " katika album ya kipe ya yo na wimbo wa " claude itoma " katika album ya quest le probleme kisha utakuja kunipa mrejesho humu.
 
unajua maana ya mwasi kitoko? kwa heshima na taadhima kama wewe ni mwana dada basi naomba nikupe heshima ya kukuita mwasi kitoko ikimaanisha mdada mzuri ( beautiful lady ).

Ha ha.....thx mkuu......ila hapo nilipoandika........le SIDA mwasi kitoko.......umepata picha ya nilichotaka kusema........?........
 
Jibu ni ndiyo. Wakati ule wa miaka ya 1996/1997 wakati Wenge iko juu full music, iliingiza Vijana na kuwapika vilivyo. Miongoni mwao ni Ferre Gola. Muda mfupi baadae Wenge ilipovunjika kuwepo Wenge ya JB Mpiana na Wenge Maison Mere, Ferre Gola aliamua kwenda kwa Werasson(Wenge Maison Mere). Baadae kidogo Aimelia Lyese Demingongo aliyebakia Wenge Music ya JB Mpiana alijiunga na Maison Mere, na hapo akampa majukumu makubwa kuliko aliowakuta. Tendo hili lilimkera sana Ferre Gola na kusema Aimelia Lyese hana lolote la kuwazidi, hivyo akaamua kujiondoa Wenge Musica!

Asante, lakini pacha wako kaandika kuwa ferre katoka kwa olomide. Ndio maana nikaja na mswali haya. Mimi napenda sana nyimbo za kikongo za taratibu ndo maana nawazimikia sana olomide, ferre na fally.
 
Ha ha.....thx mkuu......ila hapo nilipoandika........le SIDA mwasi kitoko.......umepata picha ya nilichotaka kusema........?........

mwanamke mzuri na ugonjwa wa ukimwi. sida kifaransa ni ukimwi.
 
hizo albums zote jules kibens alikuwa anashirikishwa tu katika nyimbo na hakupewa meno yote kwani alikuwa chini ya nguli na kijana ambaye hadi leo jb mpiana anamlilia alain mpela " afande " na jules kibens kaja kuibuka baada ya alain mpela kuondoka na kupewa meno ambapo sasa ni mkuu wa wanamuziki wote katika bendi, mtunzi mkuu, mhariri mkuu na mpanga miziki mkuu yote ya nyimbo za sasa za wenge musica bcbg. unasema kuwa wenge musica bcbg ya sasa haina tena makali yake labda wewe siyo mwana wenge bcbg na hufuatilii vilivyo miziki ya congo. nakupa task leo mtafute mtu yoyote wa congo hata hawa waliopo hapa dar kuwa sasa hivi congo kuna mtindo gani ambao umebamba? lazima tu watakuambia kuwa sasa congo huwaambii kitu mbele ya huu mtindo wa " mbunda " na " rota rota " na kukupa zaidi kazi ya wenge musica bcbg za hivi karibuni tafuta albums hizi kipe ya yo ( ikimaanisha hayakuhusu ) na quest le probleme ( tatizo lako ni nini? ) halafu nakuomba zisikilize kwa umakini mkubwa sana nyimbo za " voiture " katika album ya kipe ya yo na wimbo wa " claude itoma " katika album ya quest le probleme kisha utakuja kunipa mrejesho humu.
Mdau mmoja wa Wenge aitwae Gent.... simuoni akichangia mada yoyote, kulikoni mdau
 
Ok, nimekusoma! Ila kwangu early Wenge baada ya Werrason kujitenga nakusudia Album hizi:

Titanic
TH
Internet
Zenith na Olympia Live Concert
Zilikua Album ambazo unajua Vijana wako Imara.

Kipe ya Yo, Ant Terror et al zimejitahidi(kwa maoni yangu binafsi) lakini mmmh,bado kimtindo!

Kuna wimbo sikumbuki ni Album gani lakini za miaka kadhaa kuna kibao kinaitwa Ezau, nacho ni moto
 
Mdau mmoja wa Wenge aitwae Gent.... simuoni akichangia mada yoyote, kulikoni mdau

nasikia kuwa yupo likizo hadi tarehe 8, January 2016 ila kwa taarifa zake zaidi si vibaya ukamuuliza rafiki yake mkubwa humu Mwanadada aitwae @nifah atakuwa na taarifa zake zaidi kwani hata mimi nafanya kubahatisha tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom