Siku Nyingine Jitahidi Usidanganye Watu Kwani Kuna Watu Humu Miziki Ya DRC ( Zamani Zaire ) Wana Lala Na Kuamka Nayo. Kwanza Huyo Chikito Wako Sasa Ana Mwaka Ameshatoka Ktk Bendi Hiyo Ya Ferre Gola, Pili Huyu Anaimba Sana Mid Baritone Wakati Chai Ngenge Anaimba High Suprano Na Kujibu Swali Lako Kuwa Je Amesomea Muziki au Hapana Jibu Ni Kwamba Huyu Dogo Hajasomea Muziki Ila Tokea Akiwa Mdogo Alikuwa Akipenda Sana Kuimba Na Hasa Kuiga Sauti au Uimbaji Wa Wanamuziki Wa Congo Na Kuna Wakati Ferre Gola Alipojiengua Tu Kutoka Kwa Koffi Na Kuanzisha Bendi Yake Siku Moja Alifanya Show Ndipo Wakati Anaimba Akasema Anatafuta Vijana Wenye Vipaji, Watundu Wa Kuimba Na Wanaojua Kucheza Ndipo Wakajitokeza Vijana Hapo Kama 15 Hivi Ambapo Ferre Gola Aliwapa Kila Mmoja Nafasi Ya Kuimba Ndipo Shughuli Ya Chikito Ilipoonekana Hapo Na Bila Ajizi Akalamba Ajira Kwa Ferre Gola Ambapo Sasa Akawa Anaongozwa Kuimba Hadi Alipokaa Sawa Huku Akionekana Kama Kivutio Kikubwa Cha Mashabiki Wa Ferre Gola Na Kupewa Hadi Cheo Cha Vice Directore De Ochestre Wa Bendi. Na Kipindi Hicho Hicho Tu Chikito Alipokuwa Sasa Anawika Ndipo Akatokea Tajiri Mmoja Congo Anaitwa Didier Kinuani Le Comparable Na Kuamua Kumnunulia Nyumba Kubwa Tu Ya Kifahari Pale Kinshasa Lakini Muwajuavyo Wacongo Wakishapata Tu Jina Huwa Hawakai au Hawadumu Ktk Bendi Na Mwaka Jana Tu Dogo Kajiengua Na Sasa Anafanya Yake. Anaiga Mifano Ya Kaka Zake Akina Mukeba Kalonji a.k.a Bill Clinton Rapa Maarufu Wa Wenge Maison Mere Ya Werrason, Tutu Caludgi a.k.a Le Kalunjiste Rapa Na Mwalimu Wa Marepa Karibia Wengi Wa Bendi Nyingi Kubwa Za Congo Na Ambaye Ndiyo Alikuwa Rapa Kiongozi Wa Bendi Ya Wenge Musica BCBG Ya JB Mpiana, Fally Ipupa, Ferre Gola na Ndugu Alain Mpela a.k.a Afande ( Kaka Mtu ) Aliyekuwa Mwimbaji Mwandamizi Wenge Musica BCBG Na Bouro Mpela ( Mdogo Mtu ) Ambaye Nae Alikuwa Mwimbaji Mwandamizi Quarter Latin Ya Koffi Olomide. Cha Kushangaza Kati Ya Wote Hao Waliojifanya Kujiengua Na Kunzisha Bendi Zao Waliofanikiwa Ni Fally Ipupa Na Ferre Gola Pekee Huku Bill Clinton Akijikongoja Lakini Kwa Waliobaki Ni Tia Maji Tia Maji. Chikito Nae Atakuja Kujuta Kujiengua Wakati Alitakiwa Bado Akomae Kimuziki. Ni Hayo Tu!
Kaka, big up. Unaujua music wa Congo na siyo mbaya nikiamini wewe ni team JB Mpiana au Werasson. Mimi binafsi ni team JB Mpiana. Katika rap za Congo, Tutu Kaludji ni moto wa kuotea mbali. Hata hivyo nikiri tu kuwa kuna rapa wa General Defao,(Nkonzi wa Ngozi- Sorry spelling),huyu jamaa nae,alikua mkali balaa.
Leo nitawataja watu kama 6 hivi ambao ni Icon ya JB Mpiana baada ya Wenge Original kuvunjika, pia tutajikumbusha japo kwa majina Wenge Original.
Tukianza na Wenge baada ya kuvunjija, tutumie vibao vitatu:
1. Papito Mbala Version 2(Remix)
Hapa kuna majina makubwa haya:-
JB Mpiana, Aimelia Lyese Demingongo, Alain Mpela(Afande),Jules Kibens(Le Prefesseor),Chai Ngenge,Rio.
2. Internet,Le Spoi'r de Chicago, Love Airline(Vibao vya Album Internet)
JB Mpiana, Genta, Rio, Chai Ngenge, Fi Care, Jules Kibens, Mignon,Alain Mpela, Titina Alcapone, Burkinafaso.
3.Tour Eiffel, Likala moto, Baracuda, Serge Palm, Liberation
Aimelia Lyese,JB Mpiana,Alain Mpela,Chai Ngenge, Titina Alcapone, Burkinafasso,Jules Kibens,Mignon.
Hao ndiyo Wenge baada ya kusambaratika.
Tujikumbushe Wenge ya Mwanzoni ilikuaje?
Ngiama Noel Makanda(Werrason),Didier Masela, Adolph Dominguez,JB Mpiana, kwa uchache kabisa. Yapasa kujua tu kwamba JB Mpiana hakua ni mtu wa kwanza kuleta idea ya kuunda bendi, bali wazo lilitolewa na Didier Masela, Werrason na baadae Adolphe Dominguez ndipo baadae akaja JB Mpiana wa Tshituka( Mume wa Amida Shatur na binti yao Dayida)
Ila mdau, naomba unipe updates, kwa nini bendi ambayo miaka ile ya 1999-2000, ilikuja kuwatisha Wenge Musica na Extra Musica, bendi hiyo ni Group lililokua linaitwa G7,ambayo ilitisha kwa vibao na midundo ambayo siyo mchezo, lakini je kwa nini haikudumu? Mdau nifafanulie ilikuaje ilikufa ghafla vile?